Zitto aitisha Press Conference (Machi 22, 2015) Serena Hotel

Zitto aitisha Press Conference (Machi 22, 2015) Serena Hotel

Uweke hapa huo ushahidi wako!

Kama upo ushahidi basi ubandike hapa kwamba Kabwe alipokea hela kutoka usalama wa Taifa.
Unautunza wa nini huo ushahidi, unaupeleka kwenye national museum ya chama?


Msimamo gani huo wa siri za chama ambao Kabwe alienda kinyume nao, utaje!

Mbona mnaogopa kutaja? Mlikubaliana kupindua nchi halafu Kabwe akaenda kusema Usalama wa Taifa???



Okay, okay.

Kwa hiyo Kabwe amekisaliti chama kwa kuendesha gari la kifahari la Hummer ilhali anajipambanua na wanyonge wa nchi hii, huo ndio usaliti wake?

Umejuaje waliosikitika sana ni C.C.M. peke yake? Hakuna wabunge wa CHADEMA, kwa mfano, waliosikitishwa na kufukuzwa kwa Kabwe? Fuatilia kwa makini.

Kabwe hayuko Kamati ya Lembeli, angewezaje kusema yeye ndio ameongeza majina ya mawaziri kwenye ripoti ya Lembeli?

Na wala Kabwe hajasema "taarifa ya Lembeli ilikuwa shallow." Total lies. Mnashindwa kabisa kutoa a coherent and convincing indictment against the man. Umebandika nukuu za uongo.

Kabwe ana makosa mawili ama matatu. La kwanza li wazi, ni la kutaka kuwania uongozi wa chama bila ridhaa ya waasisi. La pili, alikiudhi sana chama na utawala wake pale alipovalia njuga suala la umiliki wa akaunti za nje ilhali wananchi hususan kupitia Tume ya Warioba waliona wakati umefika sasa kudhibiti umiliki wa akaunti za nje. Maadili ya Mwenyekiti wa chama yalichunguzwa kwa suala ambalo limeshikiliwa na kada wa chama, huu ulichukuliwa kama usaliti usio na mithili.

Lakini kosa la tatu, Kabwe alikuwa anakiabisha chama kwa kuwa mbunge peke yake anaekataa kubariki wasteful spending za fedha za serikali, hususan posho za kuhudhuria bunge ilhali kazi ya mbunge ni kuhudhuria bunge.

Mwenyekiti wa chama, kwa juhudi zake maishani na pia kwa urithi wa familia, ni mmoja wa watu wenye uwezo wa kifedha kuliko wote nchini, iweje hata yeye nae ashadadie posho za kukaa bungeni? Mwenyekiti ameonekana hana huruma na kodi ya Mtanzania, anadiriki hata kutumia fedha ya bunge kusafirisha mwanamke kwenda Dubai "kukamua," yani kula maraha. Kinachozungusha vichwa vya watu, hasa wale wa kawaida na wa madaraja ya chini mitaani ni kwamba iweje mtu wa kawaida nikiamua "kukamua" na kupumzika na mwanamke wa high maintanance ninamudu dola mia nne za kwenda Dubai (mia tatu nauli, mia moja chumba kwa kutwa ) kumpeleka mwanamke? Iweje Mwenyekiti wa chama ashindwe hadi atumie posho za safari na za kukaa bungeni ambazo Kabwe anazikataa?

Kabwe anawaaibisha viongozi wa chama anapojimbambanua kama mpiga vita dhidi ya wasteful spending ya fedha ya nchi. Haya yanaukera uongozi na ndivyo alivyokisaliti chama.

Umesahau chama kukaguliwa LEMA alisema alipaswa kukitonya chama kabla .
Yeye DJ alikataa KUB . Baadae akalizungukia chea mchaga wew
 
KIONGOZI Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameendelea kuwadanganya wananchi kuwa kufukuzwa kwake katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kumetokana na umakini wake wa kufuatilia "mambo yanayowakandamiza wanyonge."

Akihutubia mkutano wa hadhara mkoani Ruvuma, Zitto amesema baada ya kutambua baadhi ya viongozi wa CHADEMA hawataki kuwatumia wanyonge kwa kuwapigia kura na kujipatia ruzuku, yeye wenzake wengine wameamua kuanzisha chama kitakacho watetea wanyonge wakiwemo wakulima ambao nguvu zao zikiisha wanakufa maskini.

Amedai kuwa yeye ndiye aliyeibua hoja ya mkataba wa madini wa Buzwagi ambako waziri wa nishati na madini, alifutwa kazi; hoja ya kumng'oa aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa, Operesheni Tokomeza, wanaoficha fedha nje ya nchi na sakata la Escrow.

Amewataka wananchi wasiamini madai kuwa yeye ni ------- bali wawapime wabunge wao kwa kazi walizozifanya.

Hata hivyo, katika yote aliyoeleza Zitto hakuna hata moja ambalo ni kweli.

Mathalani, hoja ya mkataba wa Buzwagwi, iliibuliwa na gazeti la kila wiki la -----------; katkka sakata la Buzwagwi, kinyume na madai yake, hakuna waziri hata mmoja aliyefutwa kazi.

Aliyekuwa waziri wa nishati na madini, Nazir Karamagi ambaye alisaini mkataba huo nchini Uingereza, alifutwa kazi 18 Februari 2008, kutokana na kashifa ya maarufu ya Richmond.

Sakata la Richmond liliibuliwa bungeni na Kamati ya Nishati na Madini iliyokuwa chini ya aliyekuwa mbunge wa Bumbului (CCM), William Shelukindo.

Vilevile, kinachoitwa "Operesheni Tokomeza," kiliibuliwa bungeni na Christopher ole Sendeka, mbunge wa Simanjiro (CCM).

Kamati Kuu (CC) ya Chadema, ilimfukuza uanachama Zitto na wenzake watatu – Prof. Kitila Mkumbo aliyekuwa mjumbe wa CC na Samson Mwigamba aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho mkoani Arusha – kwa madai ya usaliti, kusingizia viongozi wakuu wa chama na kushirikiana na maadui wa chama.

Akisoma maamuzi ya CC, tarehe 22 Novemba 2013, mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu alisema, Zitto na genge lake wametuhumiwa kwa makosa 11 ya usaliti, yaliyotokana na "Waraka wa Mabadiliko."

Waraka huo ulioandaliwa na Mwigamba na Kitila, ulilenga kuteka chama na kukikabidhi kwa maadui wa chama wakiwamo watu kutoka Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).

Zitto ndiye aliandaliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho; naye akakiri kutaka kufanya mapinduzi ya uongozi kinyume na katiba.

"…baada ya kumsikiliza Dk. Kitila, Kamati Kuu imebaini kuwa mkakati huo haukulenga kumfanya Zitto kuwa mwenyekiti pekee, bali ulikuwa na malengo makubwa ya kukibomoa chama hicho," ameeleza Lissu.

Amesema, Zitto alikihujumu chama hicho na kushiriki kujitoa kwa wagombea wake wa ubunge katika majimbo ya Mpanda Mashariki, Musoma Vijijini, Singida Mjini na kuwa mwaka 2006, alipewa magari mawili na Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM).

Source: http://www.wavuti.com/2015/04/------------fact-check-zitto-kabwe.html

https://groups.google.com/forum/#!msg/wanaBidii/vPicLoneNxo/1Mt757BGu7kJ
 
A.yatollah Khameini Zitto Zuberi Kabwe eti sasa kapiga marufuku wanachama wa ACT USALITI wasiwaunge mkono UKAWA kutokana na wasiwasi wake kupoteza mamlaka makubwa aliyokuwa nayo kama A.yatollah Khameini.

 
Sasa hizo..............ndio nini? kwa asiejua na anataka kujua afanyaje.


Be realist bana and open
 
naona sasa ukawa mmeishiwa hoja imebaki ACT ndio mpinzan wenu mbona mazur yote unasema yamefanywa na wabunge wa ccm? bas tuwachague ccm kwa kuwa wacdm wanarob robu tu bungen hawana jipya.... kiukwel pamoja na kuwasifia hao ccm ukwel utabak pale pale kuwa hayo yametekelezwa na ZZK
 
Sasa hizo..............ndio nini? kwa asiejua na anataka kujua afanyaje.


Be realist bana and open

mkuu jf mods wamelifanya neno m.salilti kuwa kama tusi humu jamvini ili kumsitiri Zitto
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom