Zitto aitibua CHADEMA

hatumtaki,asirudi huku,na kama anataka kurudi aache urafiki na Kitila
 

Sasa kumbe wao wanataka kumsamehe mtu ambaye hajaomba kusamehewa?
 
ikiwa CCM watashindwa kuisimamia Serikali, napenda kuona UKAWA wakiwa na waziri mkuu anayeitwa Zitto Kabwe.
 
Hey guys, let's get tired of this waste please, we should open a new chapter on this, disunity is no longer an issue!
 

Wote nyie wapenzi wa zitto iwe kwa kweli au kwa kuchochea mgogoro jamaa yenu alikosa na hawezi kuombwa msamaha,yy ndio anapaswa kuomba msamaha asipoweza aendee chama chote anachotaka, amekuwa kwenye siasa muda mrefu atakuwa anajua kuendesha chama cha siasa sio kuandikwa kwenye magazeti,kama anahekima basi ningemshauri aombe msamaha bado anayonafasi ya kutengeneza alipo bomoa.CHADEMA ndio chama pekee watu wote wanapewa nafasi ya kuonyesha uwezo wao.Ifike wakati watu wote tunaongea humu tuwe wakweli, wabunge wote wa chadema kuunga mkono kamati ya zitto ilitosha kuonyesha hakuna mtu mwenye chuki binafsi naye hatima ya zitto kisiasa iko mikononi mwake mwenyewe
 

hapo kwenye rangi mantiki ya hoja yako ni mfu ..tuseme haya isomeke ivo ulivotaka wewe tujiulize kwanza je bila kuiunga mkono kamati ya zitto wangefanya nini zaidi ya hilo? hao wabunge wako vilaza kama wewe trolly
 
thread ya kugombanisha, haina hata source ya uhakika!
 
nafiri hili yaishe yawekwe wazi kwani ilisikika kila kona ya mchi ili kweli ijulikane
 
Mwenyekiti nae anataka kutuaminisha hiki chama ni chake sasa, kwani kuna shida gani wakasameheana kujenga upinzani wenye nguvu, najua Zitto amejutia usaliti wake na sidhani kama atarudia tena, asamehewe tu.
zitto aweke masharti ni mkubwa kuliko chama???????????

hata slaa na mbowe hawawezi wakaiwekea masharti cdm
 
seriously umekaa chini ukaandika hivo....
 
Na wewe ni mpenda vurugu sana.Kundi lako hapo na wewe ni lipi?

CC😡pasco,
 
Ndugu wanajamvi,

Nikiwa kama mwanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA),napenda kutoa maoni yangu kuhusu maoni ya mmoja wa kada wa chama chetu ambaye yupo kwenye mgogoro na chama Mh Zitto Kabwe ambaye siku chache zilizopita alisikika akitaka yafanyike maridhiano kati ya pande mbili yaani CHAMA na YEYE Mh Zitto.

Sasa napenda kumtumia ujumbe huu wa wazi Mh.ZITTO.

Kwanza napenda kuongea bila chembe ya unafki wala kuegemea upande wowote kwamba Mh Zitto ni kati ya wanasiasa wenye mvuto sana katika medani za siasa za nchi yetu,
Pili Mh Zitto siyo tu kwa CHADEMA bali pia kwa taifa nzima mchango wake ni mkubwa sana katika ujenzi wa Taifa.

Lakini Zitto umekuwa na mgogoro na chama chako karibu mwaka mmoja sasa ,,lakini pia ukweli hautafichwa siku zote kwamba CHADEMA imemlea sana Mh Zitto kisiasa hadi political legacy aliyofikia kitaifa hata kimataifa,, ni wazi Mh Zitto bado yuko kwenye position yake kupitia CDM japo tayari wana mgogoro......

Pia napenda kupongeza msimamo wa Mh Zitto wa bado kuonesha interest ya kupenda siasa za mabadiliko huku akishindwa kuficha mapenzi makubwa aliyonayo kwa chama chake na upinzani kwa ujumla.....
Kinachonipa shida ni pale Zitto anapotaka kuabudiwa na chama huku akitaka endapo itabainika chama kina makosa basi aombwe msamaha hadharani na chama ambacho ni taasisi yenye zaidi ya wanachama Million 5 nchi nzima,, Je ni sahihi kweli Mh Zitto kuombwa msamaha hadharan na watanzania zaidi ya million 5????
Mh Zitto wew umekuwa kiongozi ndani chama hiki kwa muda mrefu sana, pengine niseme wew unazijua vizuri taratibu za chama hata kuliko mimi ninayeandika waraka huu,, Je ni sahihi wew kwa makusudi kupuuzia wito wa chama wa kuitwa mbele ya wajumbe wa kamati kuu kujibu hoja 11 ulizopewa uzijibu badala yake kwa makusudi ukapuuzia huo wito na kukimbilia mahakamani then leo unataka kuombwa msamaha na chama???
Mh Zitto kwa nini unapenda kuabudiwa?? Huoni hiyo ni dharau kwa Wanachadema ambao kwa nia njema wameonesha kukuunga mkono kumaliza tofauti zako na chama ili kuendeleza harakati za ukombozi??
Mh Zitto kwa jinsi ninavyofahamu uelewa wako kidogo napata wakati mgumu hivi ni kweli wewe ndio unahitaji chama ambacho ni taasisi ikuombe msamaha au umenukuliwa vibaya?? HAPANA,, Mh Zitto umeteleza tafadhali tafakari tena maneno yako,, unataka watanzania ambao unawategemea wakupe nafasi ya kuwaongoza leo wakupigie magoti?? Je hao wanachadema unaotaka leo wakupigie magoti wameshakusaidia kwa mambo mangapi?? Kuvuma kwako kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi si kwa ajili ya Watanzania ambao miongoni mwao ni wanachadema waliokuweka hapo ulipo???

HAPANA...... mh Zitto tafakari kaa chini umeteleza kiburi haitakusaidia.... Wewe ni nyota njema kwa ajili ya Tanzania tuitakayo ila kiburi chako haitakupeleka mbali.

MSIMAMO NA MAONI YANGU.

Naomba chama isije ikajichanganya kumwomba msamaha Mh Zitto,, itakuwa ni fedheha sana kwa chama changu yenye wanachama zaidi ya Mil.5 nchi nzima, pia ikumbukwe kwa mujibu wa katiba na kanuni ya chama hakuna mwanachama bora zaidi ya mwenzake,, wanachama wote ni sawa ila tumetofautiana kumajukumu....
Mwisho..... Namsihi Mh Zitto aachane na kiburi atumie hekima waondoe tofauti zao na chama na busara zitumike kwa pande zote.

Ahsanten sana

Nawasilisha

Gjhariohay.
 
Mkuu asante kwa maoni yako. Umekisogeza kisu kwenye mfupa.

Ulikuwa karibu ukiweke kabisa mfupani.

Ukitaka kukiweka kisu kwenye mfupa Kwa uzuri, soma tena katikati ya maneno hizo kauli zilizotolewa Kwenye magazeti kadhaa. Pia review ile kauli ya bungeni. Ndiyo utaelewa endapo gitaa lako umelipiga mahali sahihi.

Usiache pia kuwaambia kuwa Wana CHADEMA kwa sasa wako busy na uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji. Wako mapambanoni. Wako kwenye vita ya demokrasia wakikabiliana na njama za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kusikiliza maelekezo ya CCM ili chama hicho kipate ushindi wa chee mezani badala ya kufuata sheria.

Wakati makamanda wako mapambanoni wakipigiania demokrasia ya kijiji, wengine wako busy wakijaribu kubadili mwelekeo ili wawe topical kila wakati kunapokuwa na masuala ya muhimu.

Wanao muda wa kufanya hivyo Kwa sababu hawashiriki uchaguzi huu hivyo hawana cha kupoteza...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…