Alisema serikali inapaswa kukiri kwamba, kuna Watanzania wengi waliomaliza darasa la saba, kidato cha nne na cha sita, walioko mitaani hawana ajira. Tusipoangalia watakuja kula sahani moja na sisi. Tusipowashughulikia," alitahadharisha Lowassa.
Kadhalika, alisema mipango mingi ya maendeleo nchini imekuwa haifanikiwi kutokana na serikali kutokuwa na msimamo wa kufanya maamuzi magumu
"Tatizo la nchi hii mnazungumza mambo hakuna utekelezaji. Tunazungumza, lakini discipline (nidhamu) ya (nchi ya) Malaysia na hapa (Tanzania) ni tofauti. Hapa kuna uswahili mwingi wa kukaa bila kutekeleza mambo, mnaamua hamtekelezi," alisema Lowassa
Alishauri kuwapo na chombo, ambacho kinaweza kufanya maamuzi magumu na yakawa magumu yanayotekelezeka kweli kweli.
Alisema tabia ya kujivika joho la kufanya maamuzi ya utekelezaji, lakini bila kufanya, ni kazi bure
"Tukikubaliana mambo yafanyike. Haiwezekani katika nchi kila mtu akawa analalamika. Kiongozi analalamika, mwananchi analalamika, haiwezi ikawa ni jamii ya kulalamika lalamika. Awepo mtu mmoja anayefanya maamuzi na anayechukua hatua," alisema Lowassa