Kwa maoni yangu, safari ya Ujerumani ilikuwa imepangwa kabla. Haiwezekani mtu ajisikie vibaya Alhamisi, atibiwe zahanati a Bunge, Ijumaa aje Dar, Jumamosi huyoo Ujerumani.
Taratibu za kutibiwa nje ya nchi ni ndefu unless it is real emergence. Mhe. Zitto hakuwa na dharura ya kuhivyo kukimbizwa hospitalini Ujerumani, ila kwa vile safari ilikuwepo, na amejisikia uchovu, akaamua ngoja tuu akachunguzwe huko huko.
Kitu ambacho lazima tukubali, kwenye masuala ya tiba, Mjerumani ni mwisho!. Sisi tunawakumbatia Wahindi kwa kupeleka wagonjwa wetu India, sio kwa sababu ya ubora wa tiba, ni kwa sababu ya cheap service na bakhshis kubwa kubwa kila anayewapeleka biashara.