Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 233
Zitto aenda kutibiwa Ujerumani
Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe, amekwenda Ujerumani kwa ajili ya matibabu baada ya kuzidiwa mwishoni mwa wiki akiwa bungeni mkoani Dodoma.
Akizungumza na Nipashe jana akiwa Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Zitto alisema atakaa nchini Ujerumani akiangaliwa afya yake kwa muda wa wiki moja.
Alisema hayuko katika hali mbaya sana na kwamba anasumbuliwa na uchovu wa kawaida tu, hivyo anaenda kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa afya yake.
Naumwa kidogo tu, hapa niko Airport naenda Ujerumani leo Siumwi saana.. Hii ni fatigue tu, alisema Zitto pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema katika ujumbe wake kwa mwandishi wa habari hizi.
Zitto aliugua ghafla juzi jioni ikiwa ni muda mfupi baada ya Bunge kupitisha muswada wa Sheria ya Madini.
Zitto (34) alipelekwa kwenye zahanati ya Bunge baada ya mjadala wa muswada wa madini ambapo alichukuliwa vipimo na kuruhusiwa kuondoka.
Waliomshuhudia Zitto akitoka ndani ya ukumbi wa Bunge walisema kuwa walimsikia akilalamika kuwa anasikia maumivu ya kichwa.
Akiwa nje ya ukumbi, Zitto alisalimiana na baadhi ya wabunge lakini baada ya muda alionekana akipepesuka na aliomba msaada kwa waandishi waliokuwa jirani naye ambao walimpeleka kwenye zahanati ya Bunge ambako alitibiwa.
CHANZO: Nipashe