Zitto achukua fomu Kigoma mjini

Zitto achukua fomu Kigoma mjini

Zitto apiga tambo kuelekea bungeni

zitto.jpg

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT, Zitto Kabwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Safari ya mbunge wa zamani wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe kurejea bungeni imeanza rasmi baada ya kiongozi huyo wa chama kipya cha ACT-Wazalendo kuchukua fomu za kuwania kuongoza jimbo la Kigoma Mjini.

Uamuzi huo wa kulitaka jimbo hilo unathibitisha kauli zake ambazo amekuwa akizitoa kwa muda mrefu kuwa hatarudi tena Kigoma Kaskazini kwa kuwa alishawatimizia kila kitu na haoni sababu za kuwawakilisha tena wananchi wa eneo hilo.

Kauli yake iliibua ubashiri kuwa Zitto anataka kubadilishana jimbo na mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba, uvumi ambao aliukanusha akisema hadhani kama CCM inaweza kupata jimbo Kigoma.

Zitto, ambaye alijiondoa Chadema baada ya kukiuka katiba kwa kufungua mashtaka dhidi ya chama hicho, hakufanya mbwembwe wakati akienda kuchukua fomu kwenye ofisi za ACT Ujiji jana, badala yake aliita viongozi wa kata na matawi bila ya kutaarifu vyombo vya habari.

“Nimeamua kugombea ubunge wa Kigoma Mjini ili niwatumikie ndugu zangu ambao wamekuwa wakipata tabu katika kupigania haki zao za msingi ambazo walistahili kuzipata kama ilivyo katika mikoa mingine,” alisema Zitto alipoongea na mwandishi wa Mwananchi kwa simu.

“Nitakapokuwa mbunge wa Kigoma Mjini nitahakikisha barabara za mitaani zinapitika katika kipindi chote cha mwaka, nitahakikisha watu wanaacha tabia ya kulima mashamba katikati ya mitaa na makazi, lakini nitahakikisha kila mmoja anajiunga na mifuko ya kijamii ili kujiwekea akiba ya uzeeni pamoja na kupata huduma ya matibabu, elimu na nyinginezo zinazopatikana kwa kutumia mifuko hiyo.”

Mwenyekiti huyo wa zamani wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema bonde la Mto Luiche bado halijatumika ipasavyo kuzalisha chakula kwa wingi.

“Nakusudia kuibana Serikali ijenge skimu ya umwagiliaji maji ili wakulima walime kilimo cha mpunga kwa mwaka mzima bila kupumzika, jambo ambalo litainua uchumi wa wakulima na kuongeza chakula hapa Kigoma,” alisema.

Kuhusu umeme wa gridi ya Taifa, Zitto alisema lazima upatikane ili kusaidia jitihada ya ujenzi wa viwanda vya kusindika mazao ya uvuvi na kilimo kwa kuwa hivi sasa mji wa Kigoma Ujiji unategemea umeme wa jenereta ambao hauwezi kuendesha shughuli za viwanda, hali inayochangia mkoa kuendelea kuwa masikini licha ya kuzungukwa na rasilimali nyingi.

Katibu wa ACT wa Jimbo la Kigoma Mjini, Azizi Ally alisema Zitto alichukua fomu hiyo jana kwa malipo ya Sh100,000 mbele ya viongozi 72 wa kata na matawi kutoka jimboni humo.

“Kwa hali ya sasa Kigoma Mjini inahitaji kupata mbunge anayeweza kufuatilia mambo kwa kina ili kuleta maendeleo ya wananchi baadala ya yule anayekwenda bungeni kujifunza,” alisema Ally.

“Watu wanakabiliwa na kero mbalimbali kama ubovu wa barabara za mitaani, uhaba wa umeme wa uhakika unaoweza kuendesha viwanda vikubwa na vidogo, pamoja na wengi kufanya kilimo cha kujikimu zaidi.“

Zitto alitofautiana na uongozi wa juu wa Chadema uliomtuhumu kuwa alikuwa amefanya uasi na kwamba alishaanzisha chama kingine akiwa ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani na kusababisha avuliwe nyadhifa zote, ikiwamo ya unaibu katibu mkuu.

Hata hivyo, wakati Chadema ikijiandaa kumjadili na pengine kumvua uanachama, Zitto alifungua kesi akitaka mahakama imuamuru katibu mkuu wa Chadema ampe nyaraka za mwenendo wa vikao vilivyomvua madaraka na kuomba amri ya kuzuia vikao hivyo visimjadili.

Katika hukumu ya kesi hiyo, mahakama ilitupilia mbali hoja zake, uamuzi uliotafsiriwa kuwa umefungua njia ya kutimuliwa kwake kwa kitendo cha kufungua kesi mahakamani kinyume cha katiba.

Mkazi wa Gungu mjini Kigoma, Zuberi Mrisho alisema ujio za Zitto kugombea Ubunge wa jimbo hilo utaamsha ari ya wananchi kujiandikisha kwa wingi katika Daftari la Wapigakura na kujitokeza kupiga kura tofauti na chaguzi zilizopita.

“Mwaka 2010 Vijana wengi hatukupiga kura hapa kwa sababu tulikosa imani na baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali, lakini kwa ujio wa Zitto sasa nina hakika wengi tutajitokeza kupiga kura ili tupate viongozi makini kwa maslahi ya mji wetu,’ alisema Mrisho.

Chanzo: Mwananchi

==========

My take;- Alisema majimbo ya Segerea, Ubungo na Ukonga wanamhitaji. Vipi kawasaliti hawa tena?

Si alisema anastaafu ubunge? Kweli madaraka matamu
 
Hahahahahahh.....

Kamkimbia Mnyika Ubungo? Kamkimbia Mdee Kawe?

Mtamkimbia Mnyika mmoja baada ya mwingine, alianza Nape, kakimbilia Mtama. Sasa ni NURU YA CHAMA kakimbilia Kgm Mjini? Hapo juzi alikuwa na mbwembwe nyingi oooh, nagombewa na Wananchi wa Ubungo, Kawe, Kahama, Shinyanga.....nk Maweeeeeeee kakimbilia Kigoma Mjini baada ya kuvurunda jimbo lake la Awali..!!!

Poleni wanakigoma Mjini ila si Mbaya anakuja mgombea wa UKAWA hapo mpeni ushirikiano.

BACK TANGANYIKA

Dada nakushauri wahi hospitalini kwani ugonjwa wako wa fistula unatibika, maana umepoteza network zote hujielewi.
 
si alisema 2015 harudi kugombea ubunge bali ataenda kuomba kura za urais
ukiwa mwongo inabidi uwe na kumbukumbu
 
Zzk akiacha tamaa ya fedha,madaraka,utoto na uchonganishi (ukiwemo uongo na uzushi) anaweza kuwa kiongozi mzuri hapo baadae.

Tamaa ya Zitto iko wapi? Utoto wa Zitto uko wapi? Uchonganishi wa Zitto uko wapi? Au maneno yote hayo yanakutokana kwasababu alitaka kugombea uenyekiti pale Chadema???
 
Siasa hizi za akina Zitto na Serukamba ni za kihuni sana!Wanajua majimbo yao hawakufanya kitu sasa wanahama wakitumia ukwasi walio jilimbikizia kuhadaa wapiga kura wapya!

Dr Mwakyembe nae anafikiria kuja Kawe sababu Kyela hawezi shinda hata kura za maoni ndani ya CCM na pia hawezi mshinda Abraham Mwanyamaki wa UKAWA

Dada hebu niambie Serukamba atagombea wapi? maana naona unaharisha tu kama bata.
 
Zitto apiga tambo kuelekea bungeni

zitto.jpg

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT, Zitto Kabwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Safari ya mbunge wa zamani wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe kurejea bungeni imeanza rasmi baada ya kiongozi huyo wa chama kipya cha ACT-Wazalendo kuchukua fomu za kuwania kuongoza jimbo la Kigoma Mjini.

Uamuzi huo wa kulitaka jimbo hilo unathibitisha kauli zake ambazo amekuwa akizitoa kwa muda mrefu kuwa hatarudi tena Kigoma Kaskazini kwa kuwa alishawatimizia kila kitu na haoni sababu za kuwawakilisha tena wananchi wa eneo hilo.

Kauli yake iliibua ubashiri kuwa Zitto anataka kubadilishana jimbo na mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba, uvumi ambao aliukanusha akisema hadhani kama CCM inaweza kupata jimbo Kigoma.

Zitto, ambaye alijiondoa Chadema baada ya kukiuka katiba kwa kufungua mashtaka dhidi ya chama hicho, hakufanya mbwembwe wakati akienda kuchukua fomu kwenye ofisi za ACT Ujiji jana, badala yake aliita viongozi wa kata na matawi bila ya kutaarifu vyombo vya habari.

“Nimeamua kugombea ubunge wa Kigoma Mjini ili niwatumikie ndugu zangu ambao wamekuwa wakipata tabu katika kupigania haki zao za msingi ambazo walistahili kuzipata kama ilivyo katika mikoa mingine,” alisema Zitto alipoongea na mwandishi wa Mwananchi kwa simu.

“Nitakapokuwa mbunge wa Kigoma Mjini nitahakikisha barabara za mitaani zinapitika katika kipindi chote cha mwaka, nitahakikisha watu wanaacha tabia ya kulima mashamba katikati ya mitaa na makazi, lakini nitahakikisha kila mmoja anajiunga na mifuko ya kijamii ili kujiwekea akiba ya uzeeni pamoja na kupata huduma ya matibabu, elimu na nyinginezo zinazopatikana kwa kutumia mifuko hiyo.”

Mwenyekiti huyo wa zamani wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema bonde la Mto Luiche bado halijatumika ipasavyo kuzalisha chakula kwa wingi.

“Nakusudia kuibana Serikali ijenge skimu ya umwagiliaji maji ili wakulima walime kilimo cha mpunga kwa mwaka mzima bila kupumzika, jambo ambalo litainua uchumi wa wakulima na kuongeza chakula hapa Kigoma,” alisema.

Kuhusu umeme wa gridi ya Taifa, Zitto alisema lazima upatikane ili kusaidia jitihada ya ujenzi wa viwanda vya kusindika mazao ya uvuvi na kilimo kwa kuwa hivi sasa mji wa Kigoma Ujiji unategemea umeme wa jenereta ambao hauwezi kuendesha shughuli za viwanda, hali inayochangia mkoa kuendelea kuwa masikini licha ya kuzungukwa na rasilimali nyingi.

Katibu wa ACT wa Jimbo la Kigoma Mjini, Azizi Ally alisema Zitto alichukua fomu hiyo jana kwa malipo ya Sh100,000 mbele ya viongozi 72 wa kata na matawi kutoka jimboni humo.

“Kwa hali ya sasa Kigoma Mjini inahitaji kupata mbunge anayeweza kufuatilia mambo kwa kina ili kuleta maendeleo ya wananchi baadala ya yule anayekwenda bungeni kujifunza,” alisema Ally.

“Watu wanakabiliwa na kero mbalimbali kama ubovu wa barabara za mitaani, uhaba wa umeme wa uhakika unaoweza kuendesha viwanda vikubwa na vidogo, pamoja na wengi kufanya kilimo cha kujikimu zaidi.“

Zitto alitofautiana na uongozi wa juu wa Chadema uliomtuhumu kuwa alikuwa amefanya uasi na kwamba alishaanzisha chama kingine akiwa ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani na kusababisha avuliwe nyadhifa zote, ikiwamo ya unaibu katibu mkuu.

Hata hivyo, wakati Chadema ikijiandaa kumjadili na pengine kumvua uanachama, Zitto alifungua kesi akitaka mahakama imuamuru katibu mkuu wa Chadema ampe nyaraka za mwenendo wa vikao vilivyomvua madaraka na kuomba amri ya kuzuia vikao hivyo visimjadili.

Katika hukumu ya kesi hiyo, mahakama ilitupilia mbali hoja zake, uamuzi uliotafsiriwa kuwa umefungua njia ya kutimuliwa kwake kwa kitendo cha kufungua kesi mahakamani kinyume cha katiba.

Mkazi wa Gungu mjini Kigoma, Zuberi Mrisho alisema ujio za Zitto kugombea Ubunge wa jimbo hilo utaamsha ari ya wananchi kujiandikisha kwa wingi katika Daftari la Wapigakura na kujitokeza kupiga kura tofauti na chaguzi zilizopita.

“Mwaka 2010 Vijana wengi hatukupiga kura hapa kwa sababu tulikosa imani na baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali, lakini kwa ujio wa Zitto sasa nina hakika wengi tutajitokeza kupiga kura ili tupate viongozi makini kwa maslahi ya mji wetu,’ alisema Mrisho.

Chanzo: Mwananchi

==========

My take;- Alisema majimbo ya Segerea, Ubungo na Ukonga wanamhitaji. Vipi kawasaliti hawa tena?

Teeeh,teeeh,njaa mbaya saaana,du huyo huyo zzk alishatangaza kuwa hauhitaji ubunge tena,leo tena baada ya kufanya evaluationa ya ziara ya kutafuta kuungwa mkono ktk mikoa zaidi ya 10, na kuambulia wanachama 700, amestuka!
 
Attachments

  • 1432377138032.jpg
    1432377138032.jpg
    5.3 KB · Views: 403
Inaonyesha unajua kuandika na kusomo tu yaan unataka alisema , ameombwa , kigoma mjini,segera kahama, ubungo,ukonga, sasa yeye amechagua kigoma mkoa wa nyumba kulingana na washauri wake , wew ulitaka ajigawe au

Atahama sana majimbo kwani na hapo kigoma mjini haambulii kitu zaidi ya namba za kiatu,huku ukawa wakizoa kura kibao
 
Tamaa ya Zitto iko wapi? Utoto wa Zitto uko wapi? Uchonganishi wa Zitto uko wapi? Au maneno yote hayo yanakutokana kwasababu alitaka kugombea uenyekiti pale CHADOMO??? Dada nakushauri acha ushabiki mavi maana huko nyuma unatumiwa vibaya na viongozi wa CHADOMO.

Mara uwaite wengine bila kuwa na uhakika na jinsia zao,mara matusi ya kishamba nk nk. Wewe ushaonyesha jukwaa hili sio saizi yako na hao ACT wanakituma uwasemee lazima na wao wana matatizo. Ngoja tuone kama utakuwa na maisha marefu ndani ya Home of GT
 
October mtakuja hapa kulalamika kuwa Usalama wa Taifa wameiba kura za Mnyika.

Usalama wa taifa hapa wameingiaje?unataka kusema 2010 aliposhinda mnyika usalama wa taifa hawakuwepo?shirikisha ubongo wako kufikiria la kuandika
 
Dada hebu niambie Serukamba atagombea wapi? maana naona unaharisha tu kama bata.

Hapa watu wana akili zao,acha utoto wa facebook na kujiandikisha kwako jana ingawa umebadili ID!!Andika kwa hekima pls na ficha upumbavu wako hapa!

Hauna adabu hata kidogo
 
Mkuu Pakachua taratibu basi, siyo kupakachua utafikiri uko kichakani na mambo yako yale. Hatuko Lindi hapa eboooooh

Siye mimi niliyesema nagombewa na wananchi wa Ubungo, Kawe, Shinyanga nk, Ni huyo. Kamanda wangu wa kale. Mimi nilitarajia kwamba atakwenda kule alikogombewa na Wananchi kumbe kumekuwa kugumu kwake? Sasa ikiwa nilichojadiri mimi hapo juu ndo kamasi sasa wewe hapa ubongoni mwako kuna nini? Ma.vi siyo?

Pakachua kwanza Akili kabla hujapakachua Mdomo...!!!

BACK TANGANYIKA
samahani mkuu unaelewa maana ya nk? kwanini huko nk kusiwe kigoma mjini?
 
Zitto kaenda kupambana kwenye jimbo la CCM angeenda kugombea kwenye jimbo la upinzani tungesikia lawama nyingi tu Zitto anauwa upinzani.

Mtoto kurudi kwa mzazi hakuna ajabu,kwani zzk karudi nyumbani na hilo jimbo ataachiwa ila bahati mbaya sana kwake UKAWA ndio inalichukuwa hilo jimbo,zzk asubiri ubunge wa viti maalumu.
 
Last edited by a moderator:
kuna kitu kimoja watu wengi hamjajua, huwezi kuzuia mvua
 
Back
Top Bottom