Uchaguzi 2020 Zitto 2015 ulikataa UKAWA, why leo utake Coalition?

Zitto Kabwe ni Mwanasiasa mnafiki, mbinafsi, mwongo na mtu wa kumuogopa kama ukoma. Mara zote amekuwa akilenga mambo yanayompa maslahi binafsi na si umma mkubwa wa Watanzania.

Mwaka 2015 wakati Watanzania tukitaka mabadiliko ya kweli, na kuunda Coalition ya UKAWA Zitto alikuwa kinyume chetu kabisa, na hakutaka hata kushirikiana nasi. By that time chama chake hakikutaka kabisa kumpigia kampeni Mgombea wa CHADEMA aliyeviwakilisha vyama vya Upinzani chini ya UKAWA ndugu yetu Lowassa, na badala yake ACT-Wazalendo walisimmamisha mgombea wao Mama Anna Mghwira na kuzigawa kura za Upinzani. Aidha ACT-Wazalendo walisimamisha wagombea wao wa Ubunge na Udiwani na kuzigawa kura majimboni na kwenye Kata

Kwa kipindi chote cha 2016-2017 Zitto alikuwa totally kinyume na movements ambazo Wabunge wa UKAWA walizichukua wakiwa Bungeni; wakitoka nje, yeye alibaki ndani na hata kuwaponda mara nyingine

This time around ACT-Wazalendo wanataka Mgombea wanayemsimamisha wao, Ndugu Bernard Membe, aungwe mkono na vyama vingine vyote vya Upinzani. Wanataka kukiimarisha chama chao kuwa Chama kikuu cha Upinzani kwa mgongo wa Mgombea wao mmoja kwenye Uchaguzi Mkuu. Wanajua fika wakiungwa mkono na vyama vingine wanaweza ongeza idadi ya Wabunge kwani katika Bunge la 11 alikuwa Zitto peke yake, na hivyo kuongeza kiasi cha fedha wanachopokea kama ruzuku

Nitashangaa sana, CHADEMA iliyokuwa na Wabunge na Madiwani wengi ikiingia kwenye mtego uliotegeshwa na ACT-Wazalendo yenye Mbunge Mmoja na Madiwani kiduchu. That will be the offical death of Opposition in Tanzania.

NCCR na NLD walinufaika nini kwenye huo UKAWA?

Kwa ubinafsi huu kila chama kisimame kivyake na CCM itaondoka tu haiwezi kutawala milele nchi hii.
 
hata Wassira alishawahi kusema kabla ya mwaka 2015 Chadema itakua imeshakufa.
Wasira aliyasema haya na kubakia maneno matupu, vitendo ikawa hakuna. Kwasabb enzi hizo Kikwete alikuwa ameacha wanasiasa wafanye siasa.

Lkn enzi hii JPM anadeal na chadema kwa vitendo. Amedhamiria kuiua chadema na anatekeleza. Angalia chaguzi ndogo za wabunge Kinondoni, kule Kakonko, Siha, Longido.nk.

Angalia pia uchaguzi wa serikali za mitaa. Fungua macho pia uangalie kwann wabunge wa chadema wanakimbilia ccm. Unatapa wapi ujasiri wa kusema chadema haifi?
 
Nakusoma hata sikuelewi naona unacheka cheka tu, hivi kati ya Membe wa sasa na Lowassa wa 2015 yupi alikuwa na nguvu zaidi?

Wacha kujidanganya na huyo Membe, ni mwanasiasa wa kawaida kabisa, hana mvuto huo mnaolazimisha awe nao, na hata hiyo kanda ya kusini mnayojidai nayo bado ni kelele za mitandaoni tu, nendeni field mkajionee wacheni ndoto zenu.
Mimi sio shabiki wa Membe na sijawahi kumuelewa unaweza kunisoma kwenye thread za nyuma. Lakini kwenye medani za siasa Membe akigombea ACT obviously CDM ndio mtakuwa na wakati mgumu kuliko hata CCM. Ukweli Mchungu huu!
 
Zitto Kabwe ni Mwanasiasa mnafiki, mbinafsi, mwongo na mtu wa kumuogopa kama ukoma. Mara zote amekuwa akilenga mambo yanayompa maslahi binafsi na si umma mkubwa wa Watanzania.

Mwaka 2015 wakati Watanzania tukitaka mabadiliko ya kweli, na kuunda Coalition ya UKAWA Zitto alikuwa kinyume chetu kabisa, na hakutaka hata kushirikiana nasi. By that time chama chake hakikutaka kabisa kumpigia kampeni Mgombea wa CHADEMA aliyeviwakilisha vyama vya Upinzani chini ya UKAWA ndugu yetu Lowassa, na badala yake ACT-Wazalendo walisimmamisha mgombea wao Mama Anna Mghwira na kuzigawa kura za Upinzani. Aidha ACT-Wazalendo walisimamisha wagombea wao wa Ubunge na Udiwani na kuzigawa kura majimboni na kwenye Kata

Kwa kipindi chote cha 2016-2017 Zitto alikuwa totally kinyume na movements ambazo Wabunge wa UKAWA walizichukua wakiwa Bungeni; wakitoka nje, yeye alibaki ndani na hata kuwaponda mara nyingine

This time around ACT-Wazalendo wanataka Mgombea wanayemsimamisha wao, Ndugu Bernard Membe, aungwe mkono na vyama vingine vyote vya Upinzani. Wanataka kukiimarisha chama chao kuwa Chama kikuu cha Upinzani kwa mgongo wa Mgombea wao mmoja kwenye Uchaguzi Mkuu. Wanajua fika wakiungwa mkono na vyama vingine wanaweza ongeza idadi ya Wabunge kwani katika Bunge la 11 alikuwa Zitto peke yake, na hivyo kuongeza kiasi cha fedha wanachopokea kama ruzuku

Nitashangaa sana, CHADEMA iliyokuwa na Wabunge na Madiwani wengi ikiingia kwenye mtego uliotegeshwa na ACT-Wazalendo yenye Mbunge Mmoja na Madiwani kiduchu. That will be the offical death of Opposition in Tanzania.

kwanza umeanza andiko lako kwa kunihukumu. Polisi wewe, mwendesha mashtaka wewe, Jaji wewe. Sio sawa.

leta uthibitisho kuwa Mimi au ACT Wazalendo ilikataa UKAWA. CHADEMA, kwa sababu zinazoeleweka na wala silaumu, ndio walikataa Ushirika na ACT. Sisi tuliomba kuingia UKAWA tukakataliwa. Tuna ushahidi wa barua tulizoandika kuomba kuingia UKAWA. Tukakataliwa. CHADEMA walitangaza waziwazi kuwa adui yao Mkuu sio CCM bali ni Zitto Kabwe. Hali ya wakati ule niliielewa. Nikasema haijalishi tutakutana mbele ya Safari kwani safari yetu ni moja.
Sasa CHADEMA na ACT tunaelewana, tunafanya kazi pamoja kwa maslahi mapana ya Taifa. CCM wanatumia watu wao kutaka kutugawanya. Mimi binafsi najua hila hizo na sitaingia huo mtego. Nina hakika Kuwa viongozi wa CHADEMA wanajua mtego huu na wao hawatauingia Pia.
Hatuwezi kuwa watumwa wa historia. Ni lazima tuwe na Ushirika ili kupambana na CCM. Sisi ACT tupo tayari na hatutakuwa kikwazo cha Coalition kamwe
 
Si ameshapata somo na yaliyojitokeza 2015,
Ukawa ilikuwa darasa zuri kwa wapinzani na Mwiba kwa CCm.
 
Mleta mada muongo au kumbukumbu zako ndogo sana. 2015 Zitto alikuwa anataka sana kuungana na UKAWA lakini wanachama wote mkamezeshwa sumu kuwaa ACT ni tawi la CCM. Matokeo yake hata pale alipofanikiwa kusimamaisha wagombea ubunge karibu majimbo yote ya Tanzania mkahoji kuwa haiwezekani kwa chama kichanga kusimamisha wagombea nchi nzima bila kuwa na back up ya CCM hivyo 2015 mlimuona ZItto ni CCM na Mbatia ndio upinzani halisi.
Nadhani matokeo mnayaona sasa nani CCM na nani mpinzani. Cha ajabu mnabaki na kauli kuwa ZItto hatabariki au kigeugeu ukiuliza ukigeugeu wake nini utasikia ni msaliti hakuna jibu lingine zaid.
Kila uchwao Zitto anataka muungano uwepo wa upinzani ili kushinda CCM lakini tatizo lipo CHADEMA mnajiona mnaimarika zaidi wakati mnazidi kupotea tu. Na hata katika suala la uchaguzihuu Zitto alishakubali kuungana na CHADEMA na pia Lissu awe mgombea wa urais, lakini CHADEMA mnampuuza. Nakumbuka alishawahi kushambuliwa sana Twitter kuhusu hilo na wale kina Yeriko Nyerere.
Sasa katika mazingira kama hayo mnataka mtu afanye nini? Ataendelea kukipigania chama chake tu nyie mnaozidi kuimarika kila siku endeleeni kuimarika tu.
 
Ni wazi kwamba ACT Wazalendo wamedhamiria kumsimamisha Bernard Membe kugombea Urais wa Tanzania na kuzigawa kura za upinzani bara za Lissu au Nyalandu.

Hivyo basi nashauri CHADEMA nao waweke mgombea Urais Zanzibar na wagombea uwakilishi na udiwani katika kila eneo huko visiwani Zanzibar ili kila mtu ashinde mechi zake.
Kwa hiyo tukose wote?
Mbona huzungumzii kura nyingine nyingi kuzipata tokea wana CCM wanao waunga mkono upinzani?
Kama ACT inatafuta uungwaji mkono Bara,wajitathimi upya.
 
Sasa CHADEMA na ACT tunaelewana, tunafanya kazi pamoja kwa maslahi mapana ya Taifa. CCM wanatumia watu wao kutaka kutugawanya. Mimi binafsi najua hila hizo na sitaingia huo mtego. Nina hakika Kuwa viongozi wa CHADEMA wanajua mtego huu na wao hawatauingia Pia.
Hatuwezi kuwa watumwa wa historia. Ni lazima tuwe na Ushirika ili kupambana na CCM. Sisi ACT tupo tayari na hatutakuwa kikwazo cha Coalition kamwe
Mkuu maneno umeyamaliza,
Nimefarajika kwa maelezo haya ,
Aluta continua,
Wasio taka Umoja wote huwa ni wachawi, wanaipalilia ccm ili kura zigawike na kuipa CCM ushindi laini.
Nakumbuka jimbo la ukonga,Mgombea wa Chadema ambaye nadhani alinunuliwa na CCm wakakomaa kugombea na mgombea wa CUF huku tukiwa tumekubaliana asimameme CUF pekeyake, wakazigawa kura pasu kwa pasu na kumpa CCM upenyo ambao haukustahiki.
Ytosha ,sasa tumejifunza, Tuanze Upya.
 
kwanza umeanza andiko lako kwa kunihukumu. Polisi wewe, mwendesha mashtaka wewe, Jaji wewe. Sio sawa.

leta uthibitisho kuwa Mimi au ACT Wazalendo ilikataa UKAWA. CHADEMA, kwa sababu zinazoeleweka na wala silaumu, ndio walikataa Ushirika na ACT. Sisi tuliomba kuingia UKAWA tukakataliwa. Tuna ushahidi wa barua tulizoandika kuomba kuingia UKAWA. Tukakataliwa. CHADEMA walitangaza waziwazi kuwa adui yao Mkuu sio CCM bali ni Zitto Kabwe. Hali ya wakati ule niliielewa. Nikasema haijalishi tutakutana mbele ya Safari kwani safari yetu ni moja.
Sasa CHADEMA na ACT tunaelewana, tunafanya kazi pamoja kwa maslahi mapana ya Taifa. CCM wanatumia watu wao kutaka kutugawanya. Mimi binafsi najua hila hizo na sitaingia huo mtego. Nina hakika Kuwa viongozi wa CHADEMA wanajua mtego huu na wao hawatauingia Pia.
Hatuwezi kuwa watumwa wa historia. Ni lazima tuwe na Ushirika ili kupambana na CCM. Sisi ACT tupo tayari na hatutakuwa kikwazo cha Coalition kamwe

Haya ni maneno yako ndugu:

Hatuwezi kujiunga na UKAWA kwa kuwa CCM na vyama vingine hawana tofauti kwa sera, lakini ACT ni tofauti kwa kuwa inaheshimu miiko ya uongozi na kubwa zaidi chama chetu kinaongozwa na azimio la Tabora,”
 
Mlikataliwa kwa sababu mlikuwa Wabinafsi. Na ndiyo maana Chadema waliwaona nyie ni adui namba moja. Mwaka 2019 ndipo uliporuhisiwa kujiunga na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni baada ya kuanza kujiandaa kwa Movie hii tunayoiona sasa, na kumbuka wakati Mbatia akielezea kuruhusiwa kwako alisema sasa utapaswa kufuata taratibu zao tofauti na awali ambapo ulikuwa ujafanya kama unavyotaka. Na mostly ulitusaliti wapinzani wenzako kwenye movements kibao Bungeni. Chonde Chonde CHADEMA msiingie mtego huu mtanasa vibaya sana.
 
Ny

Nyie ndio mnaorudisha nyuma upinzain Tanzania. Sasa huyo Mbatia mliekubaliana nae yupo wapi sasa?CCM itaendelea kutawala kwa sababu ya wajinga kama nyinyi mnashindwa kuendana na wakati mmekuwa watumwa wa historia.
Mngeweza kuitumia combination ya Lissu na Zitto Kabwe hakika CCM ingepata wakati mgumu sana lakini kwa ujinga wenu bado mmelala tu mkiamini adui namba moja ni Zitto. Amkeni
 
Mimi sio shabiki wa Membe na sijawahi kumuelewa unaweza kunisoma kwenye thread za nyuma. Lakini kwenye medani za siasa Membe akigombea ACT obviously CDM ndio mtakuwa na wakati mgumu kuliko hata CCM. Ukweli Mchungu huu!
I wish huyo Membe agombee kupitia ACT halafu CDM wamuweke Lissu upate majibu yako, unaonekana huijui nguvu ya Lissu, huyo Membe labda kama angekuwa anagombea umoja wa mataifa ndio anafahamika.
 
Zitto Kabwe ni Mwanasiasa mnafiki, mbinafsi, mwongo na mtu wa kumuogopa kama ukoma. Mara zote amekuwa akilenga mambo yanayompa maslahi binafsi na si umma mkubwa wa Watanzania.

Mwaka 2015 wakati Watanzania tukitaka mabadiliko ya kweli, na kuunda Coalition ya UKAWA Zitto alikuwa kinyume chetu kabisa, na hakutaka hata kushirikiana nasi. By that time chama chake hakikutaka kabisa kumpigia kampeni Mgombea wa CHADEMA aliyeviwakilisha vyama vya Upinzani chini ya UKAWA ndugu yetu Lowassa, na badala yake ACT-Wazalendo walisimmamisha mgombea wao Mama Anna Mghwira na kuzigawa kura za Upinzani. Aidha ACT-Wazalendo walisimamisha wagombea wao wa Ubunge na Udiwani na kuzigawa kura majimboni na kwenye Kata

Kwa kipindi chote cha 2016-2017 Zitto alikuwa totally kinyume na movements ambazo Wabunge wa UKAWA walizichukua wakiwa Bungeni; wakitoka nje, yeye alibaki ndani na hata kuwaponda mara nyingine

This time around ACT-Wazalendo wanataka Mgombea wanayemsimamisha wao, Ndugu Bernard Membe, aungwe mkono na vyama vingine vyote vya Upinzani. Wanataka kukiimarisha chama chao kuwa Chama kikuu cha Upinzani kwa mgongo wa Mgombea wao mmoja kwenye Uchaguzi Mkuu. Wanajua fika wakiungwa mkono na vyama vingine wanaweza ongeza idadi ya Wabunge kwani katika Bunge la 11 alikuwa Zitto peke yake, na hivyo kuongeza kiasi cha fedha wanachopokea kama ruzuku

Nitashangaa sana, CHADEMA iliyokuwa na Wabunge na Madiwani wengi ikiingia kwenye mtego uliotegeshwa na ACT-Wazalendo yenye Mbunge Mmoja na Madiwani kiduchu. That will be the offical death of Opposition in Tanzania.

Wew naona 2015 ulikuwa chekechea na hivyo hujui politics zilivyokuwa 2015. Zitto hakukataa UKAWA, ni kwamba hakukaribishwa. Alitamka mara kwa mara kwamba anataka kujiunga lakini kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi hakukaribishwa.
 
Na hakukaribishwa kwa sababu alikuwa haaminiki, ni wajibu wake sasa kuthibitisha kwa vitendo imani kwa waliokuwa na shaka nae.
 
Mlikataliwa kwa sababu mlikuwa Wabinafsi. Na ndiyo maana Chadema waliwaona nyie ni adui namba moja. Mwaka 2019 ndipo uliporuhisiwa kujiunga na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni baada ya kuanza kujiandaa kwa Movie hii tunayoiona sasa, na kumbuka wakati Mbatia akielezea kuruhusiwa kwako alisema sasa utapaswa kufuata taratibu zao tofauti na awali ambapo ulikuwa ujafanya kama unavyotaka. Na mostly ulitusaliti wapinzani wenzako kwenye movements kibao Bungeni. Chonde Chonde CHADEMA msiingie mtego huu mtanasa vibaya sana.
We jamaa nimjinga sana, kwenye thread yako unasema alikataa kujiunga na ukawa, hapa una comment kuwa alikataliwa, sasa sisi wapenda mageuzi tukuelewe vipi?. Kama una agenda za ccm tunaomba uziache , Zitto alisema kabisa yuko tayari kwa ushirikianoo hata mgombea akiwa Lisu sasa tatizo lake liko wapi?.

Unajua watu wengine wenye mawazo kama yako niwajinga sana, hebu jichukulie wewe ni Zitto na upo katika nafasi aliyopo utaacha kujenga chama kisa utaonekana unatumiwa na ccm?.

Sisi tunachohitaji ACT & CDM washirikiane ili wagawe majimbo Kisha uraisi asimame Lisu tutawapigia Kura, Sasa kwa bahati mbaya wote hatuna uhakika kama Lisu atarejee kulingana na mazingira yaliyopo. Kwahio lazima vyama vyote iwe CDM au ACT kila chama kiendelee na mipango yake mpaka pale ushirikiano viongozi watakaporidhia uwepo. Huwezi kuacha kukiaandaa chama na uchaguzi kisa unasubiri kesho ambayo huifaham.
 
Wanasiasa wote ni wabinafsi.

Kipindi cha Ukawa, ilikuwabaliwa kwamba wagawane majimbo, kilichotokea, CDM ilisimamisha wagombea kwenye majimbo yaliyokuwa yamekubaliwa kuwa ya vyama washirika.

Nina uhakika, kama Membe angekuwa anaenda CDM, huu muungano ungepita, ila kwa sababu anaenda ACT, it's not happening.

Acha wagawane kura, CCM aendelee kuongoza.

Magufuli ameamua kwa nguvu zake kuiua CDM, CDM hawaamini mpaka pale watakapo chemsha kupata wabunge, si kwa uchache wa kura, bali kwa nguvu ya dola.
 
Back
Top Bottom