Zito abadili dini

Zito abadili dini

Nancy Tweed

Senior Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
123
Reaction score
3
Hayawi hayawi sasa yamekuwa. Hatimaye mbunge machachari wa kutoka Kigoma, muheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe ameamua kubadilisha dini yake kutoka kwenye uislamu kuelekea kwenye ukatoliki.

Vyanzo vya karibu na muheshimiwa Zitto vimeeleza kwamba, sababu ya bwana Zitto kubadilisha dini ni sababu binafsi na wala siyo za kichama kama inavyodhaniwa na wengi.

Inasemekana ndugu Zitto ana uhusiano wa kimapenzi na msichana wa kikatoliki ambaye ndiyo chanzo kikubwa cha muheshimiwa huyo kuachana na uislamu na kuwa miongoni mwa kondoo watakaookolewa na bwana yesu.

Kama ambavyo bwana yesu alisema kwamba "mimi ndiyo njia ya kuelekea kwa baba", inasemekana kwamba muheshimiwa Zitto amekubaliana na mpenzi wake wamwabudu Mungu kwa kupitia njia hiyo. Ingawa kuna miongoni mwa wakereketwa wa chadema wamesikika wakinung'unika kwamba hii ni janja tuu ya bwana Zitto ili aweze kukwapua madaraka ya juu kabisa ya chamahicho.

Chama hicho ambacho kina wafuasi lukuki katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha kimekataa kukanusha au kuthibitisha habari hizi.
 
Kama ni kweli naomba tuheshimu choice yake na let us let bygones be bygones..... Freedom of Choice...., Tuache kama akiamua atangaze basi atangaze mwenyewe... This has got nothing to do na maendeleo ya nchi yetu.
 
Ungeiandika kwenye page yake ya facebook au twitter Zitto angekuheshimu. Lengo lako hapa halina mshiko
 
ni mambo binafsi lakini kama kweli basi kwa kuchagua kukaa miguuni mwa Yesu, kachagua fungu lililojema sana ambalo hataondolewa kamwe! ooh God lead him in all your righteousness. amen
 
This has nothing to do with politics kama mleta hoja unavyotaka ieleweke watu tumeanza kubadili dini muda mrefu hata kabla ya CCM na CDM kuwepo, ikiwezekana omba Mods wabadili heading ya thread.
 
Kama Zito kaingia Ukatoliki sababu ya mwanamke, basi hakuwa na dhamira ya kweli ya kumfuata Yesu.
 
Imenenwa Mme ataachana na wazazi wake ataambatana na mkewe, nao watakuwa kitu kimoja.
 
Hii ni haki yake ya kikatiba. Kimsingi ni suala binafsi zaidi.
 
Freedom of Choice

It is freedom of worship...

Mwee dunia hii kwa udaku.Sina hamu.Kabadili dini lina na wapi. Kanisa gani limempokea?

Kwani hivi sasa Zitto anacheo cha chini? hivi Naibu Katibu Mkuu wa chama ni cheo kidogo? kiutendaji kinatofauti gani na Katibu Mkuu au Mwenyekiti? ni kuongoza vikao au status? does the three zinabadilisha status?
 
Kama hizi nguvu tungeziweka kwenye kuwapeleleza Dowans.... I Guarantee you tusingeibiwa.....
 
nancy we mzaramu?
au ulikuwa unasuka pindi ukiandika hii thread?
 
Sio mara ya kwanza kwa viongozi au watu mashuhuri duniani kubalisha dini/kuoa/kuolewa/kuchika n.k. Ni uchaguzi wake binafsi.

Hata alipochagua kuwa Muisilamu hatukumshauri au hatukuhusishwa. Nafikiri tusilikweze hili jambo kisiasa au kiitikadi...! Ni uamuzi binafsi kama mtu unavoamua kuoa au kuolewa tu...!

Hongera Zitto
 
Kuna jukwaa la maswala ya imani pengine ingefaa upeleke post yako huko.

Kujadili dini ya mtu hapa haina tija kwetu maana haina uhusiano na matatizo yetu ya msingi. Dini zimeendelea kuwa maficho ya udhalimu nchini mwetu. Kwa ZK kubadili ama kutobadili imani yake haiwezi kubadilisha udhaifu ama uimara wa uongozi alokuwa nao.

Mafisadi wote tunaowataja hapa wanakwenda makanisani na miskitini: Kama hiyo ingekuwa dawa tusilia na mafisadi nchi hii
 
Back
Top Bottom