Udom na udsm..nini mwagombania wakati msoto wa kitaa ni ule ule.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Ni kweli kabisa,
Kuna vitu vijana wengi hatuelewi:
Kila chuo nchini ni bora kulingana na nafasi yake;
Kama vijana lazima tuelewe kua ubora wa elimu yetu utaonekana kwa MSAADA WETU KWA FAMILIA NA JAMII ZETU TUNAMOISHI,
na sio majivuno na maneno yasiyo na maana;
Unakuta mtu anatembea anadunda barabarani kisa kasomea ... afu ukifika kwao, hakuna ata kitu kimoja watakwambia ichi alifanya fulan,
na wengine ndio kabisa ukifika kwao unakuta wazazi wao wanalala chini kisa hawana kitanda.
Vijana wenzangu tujitambue kua, ranking inayofanywa na mashirika inazingatia 9% academic kulingana na kwamba kila chuo kina Curriculum yake,
vigezo vingine ni pamoja na:
search engines
No. of professors etc ambavyo vingine vina uhusiano mkubwa sana na umri wa chuo.
na hata tafiti zinazofanywa ziko biases sana ndio maana hazitumiwi na serikali kwa jambo lolote.
Kiujumla vigezo vinavyotumika, wengi wetu hatuna tulichochangia na hasa undergraduates.
Lakini hata pakiwa na chuo bora zaid ya kingine: ikumbukwe binadamu wote ni sawa,
na kwa kuthibitisha hilo ndio maana ukifika chuo chochote nchini,
utawakuta wanafunzi waliotoka shule bora nchini: St Mary, St peter, & other Sts,
lakini pia utawakuta waliotoka shule za kata.
NA CHA AJABU ZAIDI NI KUA WOTE HAWANA UTOFAUTI.
NA PENGINE WALIOTOKA SHULE ZA KATA WANATOKA NA GPA & COMPETENCE NZURI SANA.
Kiujumla ndugu tufanye bidii katika hali yoyote tuliyopo,
haina maana kwa mwanafunzi kujugamba kua shule yake ni bora kitaifa uku yeye ana div.IV na mwingine shule aliyosoma ni ya mwisho kitaifa lkn yeye ana div.II/I.
Elimu tunayoipata vyuoni itusaidie kuziimarisha familia na jamii zetu. Pia itusaidie kuish vzr na watu sio kuwadharau wenzetu.
VERY SORRY KWA NILIYEMKWAZA.
Sent using
Jamii Forums mobile app