Zitakuja nyakati tutatamani Magufuli arudi hata siku moja madarakani

  • Thread starter Mikocheni Junction
  • Start date
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Ukipita mitandaoni utaona baadhi ya vijana wanavyolalamika bila Sababu

Wanamlaumu Rais magufuli kwamba maisha magumu
Ati zile maisha magumu zimeripotiwa na Rais wetu mpendwa

Tuliobahatika kuishi awamu zote tano Tunajua Mambo yalivyo na yalivyokuwa

Sisi wengine tumejifunza somo la uvumilivu tulivumilia hali ngumu kipindi cha Nyerere kutokana na Nchi yetu chini ya Nyerere kuwapinga mabeberu kwa vitendo

Mabeberu walifanya kila hila kimkwamisha Nyerere ila Kwasababu tulijua Nyerere anachopigania tulimvumilia hatukutaka tuwe wasaliti Ndani ya nchi yetu na Alifanya kazi kubwa

Baada ya hapo walipita ma Rais watatu kabla ya magufuli na walifanya kadri ya wawezavyo kuijenga Tanzania ila alipokuja magufuli tulipiga magoti kumshukuru Mungu tulijua magufuli ni nani na anataka nini
Nilikuwapo pale uhuru wakati magufuli akiapishwa sio siri nilitokwa na machozi nilimwona pia kadinali pengo akiifuta mawani yake bila shaka alitokwa na machozi

Siku ile mvua ilinyesha sana sikumbuki maneno mengi ya magufuli ila nakumbuka mstari mmoja tu alisema NiTAANZA KAZI LEO LEO Hii sentensi iliniamsha Ari ya uzalendo ule niliouamini kutoka kwa Baba wa Taifa mwl.Nyerere

Moja ya ziara za kwanza kabisa ya magufuli ilikuwa ni pale BOT baada ya ziara alisema banki kuu ni kama haina fedha maana yake zilitembea na wahuni kutokana na upole wa kikwete

Tuliomwamini magufuli tuliendelea kumwombea tulijua nguvu ya mafisadi katika Nchi Hizi maskini ni kubwa sana tulijua mafisadi watutumia kila mbinu kumkwamisha ni kweli wengine walihamisha pesa zao wengine walifunga biashara wengine walifanya kila aina ya ufedhuli kuhakikisha magufuli anakwama

Lakini miaka minne baadae Mzee yupo imara zaidi maadui zake wapo hoi wengine waliamua kuonyesha hasira zao hadharani kwa kumhujumu

Mimi binafsi nafurahi mwenyezi Mungu kunijalia uhai kushudia maajabu ya awamu ya tano awamu iliyojaa uzalendo,kupenda wananchi wake na kupigania maslahi ya Nchi
Ni bahati mbaya sana kuna baadhi ya wanasiasa na watu wasio wazalendo wanakubali kutumika na mabeberu ila hawatafanikiwa

Mimi nitawasilimua wajukuu wangu uzalendo wa Huyu msukuma toka kanda ya ziwa aliyeamua kuitengeneza ile Tanzania ya Nyerere aliyoitarajia

Ahsante magufuli ipo siku wanaokubeza watatamani urudi Ikulu hata saa moja tu urekebishe Mambo
Kwani ni ngumu kupata Rais mwaminifu na mchapa kazi kama wewe
 
S

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Messages
1,423
Points
2,000
S

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2011
1,423 2,000
Asante mkuu umenifurahisha sana.

Any way turudi kwenye mada yetu. Ina maana kuwa Diaspora ni dhambi?

Hapana mimi hivi sasa niko hapa hapa kwetu Bongo ila nilikwenda ujerumani kusoma na nika bahatika kuishi huko mda mrefu sana nikifanya kazi. Kwa sababu nina familia yangu huko sometimes huwa naenda huko kutembelea watoto na wajukuu zangu.

Naweza sema ujerumani kwa mimi pia ni nyumbani kama hapa Bongo na hasa Berlin.
Mawazo yako na speed sana. Unafiikiria vitu vikubwa sana kutatua mambo mepesi. Sina nia ya kuku embarass lakini nataka niseme issues nyingi zinakosewa na viongozi wetu. Hebu fikiria ni kazi ngapi zimepotea kwa chuki binafsi ya Jiwe dhidi ya Yusuf Manji. Manji through makampuni yake alikuwa anaajiri watu kwa maelfu. Mtu mmoja mwenye madaraka ana kisasi naye amemvuruga na Manji kafunga viwanda na ahughuli zake yuko Canada. Wanao suffer ni Watanzania waliokuwa wanafanya kazi kwenye makampuni yake.
 
Kitaturu

Kitaturu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Messages
5,056
Points
2,000
Kitaturu

Kitaturu

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2013
5,056 2,000
Uhuni wako wa mtaani usiuhsmishie hapa kama bangi zimekuchosha hamia kwenye ngada
Mjinga kabisa we
Ati yupo kutoa laana huyo mchumia tumbo

Apambane kuileta familia yake maisha bora
Usikae kufikiri kila mmoja anawaza mambo zako kichwani

Sisi ni wazalendo tupo imara kupigania wapotoshaji washindwe km wewe

Kazi ya magufuli inatambulika
Labda wapo radhia watoto wao wewe kuhudumiwa na magufuli wakiketi nyumbani bila kazi

Wajinga sana hawa
Nimekwoti baadhi ya majibu yako....

Unaonekana kupaniki sana mzee wangu uliyezishuhudia tawala za awamu zote tano Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na sasa Magufuli......

Nadhani hukutegemea andiko lako kutopata uungwaji mkono wa kiwango hiki kutoka kwa wajumbe wengi bila shaka......

Pole sana mzee wangu......

USHAURI:

Ukileta hoja, jaribu kufokasi kwenye lengo la hoja yako. Wanaojadili kistaraabu unawajibu kistaarabu....

Unaohisi wanakukejeli na wakitaka kukutoa kwenye mstari, usiwadharau bali wote hao onyesha appreciation kwa michango yao kwa ingalao ku - like comment zao.....

Si lazima uwajibu kama unadhani hakuna cha kujibu.....

Wewe waache hivyo hivyo, achana na tabia ya kurushiana vijembe na matusi eti tu kwa sbb mtu hajajibu upendavyo wewe....

Kinachonishangaza zaidi mimi, ni umri wako kuwa mkubwa kwani umejinasibu kuwa umeziona na kuziishi awamu zote za tawala za taifa hili kuanzia Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na sasa Magufuli....

Kwa hiyo ni wazi umri wako umekwenda kidogo miaka pengine si chini ya 60.....

Kwa mukutadha huu, kama unaanzisha mjadala na kisha kuusimamia kwa kujibu hoja za wachangiaji kwa staili na kwa kutumia lugha hii, napata shaka na busara na hekima yako....!!

Kwa maoni yangu, ni makosa sana kuwaita watu wanaotofautiana na mtazamo wako juu ya uongozi wa Magufuli kama Rais kuwa ni wajinga na aina nyingine za matusi....

Kama huwezi kuwa mvumilivu na mwenye subira, nakushauri usiwe na account zozote ktk social media vinginevyo utam- block kila mtu.....

Bahati tu kuwa hapa JF huna uwezo huo.....

Unachoweza kukifanya kwa ushauri wangu na kama huna ngozi ngumu ya kuvumilia kukosolewa, usianzishe mada (mjadala) wowote humu, vinginevyo utamtukana kila mtu.....

Sasa hiyo ni mbaya sana maana utadhihirisha na kujifunua wazi kuwa wewe ni mtu wa namna gani.....

Mpaka hapa mimi nimeshakuelewa na kukufahamu tayari. Kuwa wewe ni Mzee mwenye shida kidogo upstairs na unahitaji kusaidiwa....!!

Mimi ni kijana mdogo tu. Nikiwa na akili za utu uzima nikisoma sekondari nimeanza kuuona utawala wa Mkapa na kidogo nikiwa mtoto utawala wa Mwinyi. Lakini naweza kukushauri na uahauri wangu ndiyo huu...uzingatie.....

Asante, nakutakia kila la kheri
 
S

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Messages
1,423
Points
2,000
S

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2011
1,423 2,000
Nimekwoti baadhi ya majibu yako....

Unaonekana kupaniki sana mkubwa...

Hukutegemea andiko lako kutoungwa mkono na wajumbe wengi bila shaka, au siyo bwana?

USHAURI:

Ukileta hoja, jaribu kufokasi kwenye lengo la hoja yako. Wanaojadili kistaraabu unawajibu kistaarabu....

Unaohisi wanakukejeli, una - like comment zao kisha unawaacha hivyo hivyo bila kuanza kurushiana vijembe na matusi....

Kinachonishangaza zaidi mimi, ni umri wako kuwa mkubwa kwani umejinasibu kuwa umeziona na kuziishi awamu zote za utawala kuanzia Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na sasa Magufuli....ni wazi una umri wa miaka pengine zaidi ya 60.....

Kwa mukutadha huu, kama unaanzisha mjadala na kisha kuusimamia kwa kujibu hoja za wachangiaji kwa staili na kwa kutumia lugha hii, napata shaka na busara na hekima yako....!!

Kwa maoni yangu, ni makosa sana kuwaita watu wanaotofautiana na mtazamo wako juu ya uongozi wa Magufuli kama Rais kuwa ni wajinga na aina nyingine za matusi....

Kama huwezi kuwa mvumilivu na mwenye subira, nakushauri usiwe na account zozote ktk social media vinginevyo utam- block kila mtu.....

Bahati tu kuwa hapa JF huna uwezo huo. Unachoweza kukifanya kwa unziahauri wangu kama huna ngozi ngumu ya kuvumilia kukosolewa, usianzishe mada (mjadala) wowote humu, vinginevyo utamtukana kila mtu.....

Sasa hiyo ni mbaya sana maana utadhihiriaha na kujifunua wazi kuwa wewe ni mtu wa namna gani.....

Mpaka hapa mimi nimeshakuelewa na kukufahamu tayari. Kuwa wewe ni Mzee mwenye shida kidogo up stairs na unajitaji kusaidiwa....!!

Asante, nakutakia kila la kheri
Naamini huyu Mikocheni Junction ni kati ya wale wanaoitwa Buku 7 wa Lumumba. Wapo tayari kubisha na kutetea hata vitu vya kijinga ambavyo Serikali inafanya. Wanadhalilisha elimu zao kama wamesoma na heahima zao kwenye jamii. Kama hajakuelewa kwenye hiyo ushauri uliompa basi amekwisha.
 
M

mulaga

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2019
Messages
358
Points
500
M

mulaga

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2019
358 500
Nikuambie kitu kwa kifupi tu, wajerumani siku za nyuma wakati wa utawala wa Chancelor Gerhard Schroeder walijaribu kubinafsisha miradi mingi sana ambayo ilikuwa inasimamiwa na serikali yao.

Baada ya mda sio mrefu miradi mingi ilirudi tena mikononi mwa serikali. Unajua kwa nini? Kwasababu sekta binafsi ilitaka kuendesha hiyo miradi kwa mtindo wa " profit maximization" kitu ambacho hakikuwa rahisi kwa wawekezaji.

Ili kufanya hivyo walilazimika kuchukua baadhi ya hatua kama ku-reduce idadi ya wafanyakazi na kupunguza efficience au ufanisi wa Services ili ku-garantii ubora wa services. Matokeo yake serikali ilipata mzigo mkubwa wa kuwahudumia watu wake katika mahitaji muhimu kama energy, maji na huduma nyingine za kimaisha ikiwemo chakula na makazi.

Deutsche Bahn kwa mfano ni kampuni ambayo inatoa huduma za transport ya abria na mzigo kwa njia ya reli. Hili shirika liko to 100% chini ya serikali yao.

Hili sjirika sio tu linatoa service bali linajihusha na mambo mengi ya kiteknolojia. Majaribio mengi yanfanyika chini ya Deutsche Bahn iwe kwa faida au bila faida. Sasa niambie sekta gani binafsi iko tayari kufanya majaribio ya teknologia bila faida Tanzania?

Usi dream ndugu yangu. Ukiona vya elea ujue vimeumbwa.

Naomba mwuulize Mohamed Dewj kama yuko tayari kuwekeza kwa hao vijana walio tengeneza gari kwa kutumia baterii, usikie atakuambia nini.

Mnajua nyie wengi wenu mna maisha ya kasuku. Mkisikia jambo mtu amelitoa basi mna dakia bila kujiuliza ni kweli au sio? Inawezekana au haiwezekani?

Sekta bina is always destructive katika maisha ya community. Sitapenda kutoa maelezo mengi ukashindwa kusoma. Maana maelezo yangu nafikiri yanawachosha.

Naomba fanya uchunguzi wa kina wewe mwenyewe, ukiwa uko tayari na kama una maswali unaweza ukaniuliza tena.

Ulimwengu unahitaji sekta binafsi katika mfumo wa "Worker Cooperative" na sio capitalism kama hivi sasa. Sisi binadam tuna ung'ang'ania huo mfumo kwa sababu ya mazara, lakini ukweli wa mambo unatakiwa kubadilishwa haraka sana. Huko tunako kwenda utabadilishwa tu tutake tusitake.

Hizo mia tano tano za Magufuli zisikupe shida. Hata uwanaja wa ndege wa Chato usikubabaishe. Chato haishi Magufuli chato wako wa Tanzania. Ni vizuri wakiwa na kwanza wa ndege kwani hata wewe ilitaka unaweza kwenda uchi huko hakuna atakaye kufukuzwa.

Mmmmh! Wafanya biashara hawako Tanzania na Uganda tuna pia biashara haija anza na sisi. Hiyo ya ID Amini Dada kuwafukuza wahindi zilikuwa sababu zake binafsi. Nyerere haja fanya hivyo.

Naomba kama una nafasi basi wasikilize hawa waamerika wawili utajifunza mengi kuhusu sekta binafsi!
Nyerere alishawahi Fanya hivo kutaifisha biashara zifanywe na serikali umewahi sikia azimio La arusha,unayajua mashirika ya umma yako wapi sasa watu walisoma wakala hio nadharia ya serikali kufanya biashara inafaa Kwa jamii nyingine na si waafrica, mfumo wetu wa maisha atulazimishi kujituma hatuna nidhamu ya usimamizi wa mambo.Mashirika ya umma yalikufa Kwa kukosa usimamizi, ushindani, yakaendeshwa Kwa ruzuku badala ya faida yakawa mzigo ikabidi yabinafishwe.Kurudi kwenye makosa ya Nyerere ni matumizi mabaya ya kodi zetu itaishia kutoa ruzuku Kuendesha miradi inayofurahisha macho ya watawala huku ikiumiza wananchi.
 
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Sielewi kwa nini Rais Magufuli aweke reserve ya US Dollar bilioni sita ya nini? Hizo hela si angezitumia tu kwenye projects tofauti ambazo zitaisaidia nchi kupata maendeleo?
Hiyo sheria mkuu huwezi kutumia reserves
 
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Chato haijaendelezwa km mnavyodanywa kwenye media
Chato pa kawaida sana
Airport inayojengwa chato unafikiri ni milioni mbili?
Chato haina umuhimu kuendelezwa huku kuna sehemu nyingi Tanzania zenye population kubwa na rasilimali za kutosha, we niambie Chato ina nini cha muhimu sana kuwekewa airport kubwa? Labda kuna kitu sikioni. Tumegundua madini kule au?
 
M

mulaga

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2019
Messages
358
Points
500
M

mulaga

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2019
358 500
Deni limedabo lakini kazi inaonekana. Si sawa na waliokopa halafu wakafanya mikopo hiyo mali zao na wake zao.
Hio miradi Kwa uchumi uliofungwa pesa kurudi ni ngumu,labda aruhusu pesa zizunguke sio kuzifungia
 
E

emmanuel mruma

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2017
Messages
1,171
Points
2,000
E

emmanuel mruma

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2017
1,171 2,000
kawaida mbona kuna watu wanatamani kikwete arudi ata siku 3 tu
 
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Huo ni mtazamo wako tu
Lkn makonda Kwenye swala la madawa ya kulevya amejitahidi kuyadhibiti
Mmekaa kusingizia mtandao wa madawa ya kulevya, hehehe, em niambie mtandao upi huo ambao Makonda aliukomesha? ulishawahi sikia hata mtu moja mkubwa kakamatwa toka hilo sakata lianze? Msiwe mnakuja na vitu ambavyo havina proof, makonda hajafanya chochote kudeal na wauza madawa, ni the same na kipindi cha nyuma tu, sanasana amekaa kutukana tu watu wazima kawageuza watoto wake.

Sisemi magufuli ni mjinga kukaa kimya, lazima ana sababu zake ndiyo, ila na wewe huwezi kaa ukadhani yeye ni smart kwa kukaa kimya, huwezi jua makonda ana nini cha kumfanya akae kimya, yaweza kua ni negative sio positive, au hata ikawa ni ego tu kua hapangiwi kitu na mtu, si mara ya kwanza anakurupuka kufanya jambo kwa sababu ya ego tu kujifanya kua yeye ndiye anajua kuliko mwingine nchi nzima.

Tatizo we ni sifia kila kitu, mmemgeuza jamaa kama mungu flani vile kua hana mapungufu. Kaa ukumbuke na yeye ni binadamu vilevile, ana feelings ka wengine, tena yeye ana hasira za kijinga sana kuliko mtu wa kawaida, ukitaka proof ingia online angalia hotuba zake karibia zote.
 
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Acha wivu wa kitoto mkuu tutambue uchapa kazi wa mh.Rais
Kweli tunatofautiana maono, yaani na huyu Magufuri unamfananisha na Nyerere na kumuita saint?? Hata shetani ameshituka alipoona maandishi yako, anyway kumbe wewe ni diaspora
 
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Ukiambiwa weka ushahidi utaleta au unabweka nyuma ya keyboard tu
Makonda alikuja kusambaratishwa waletaji madawa washindani na kutengeneza mfumo wa kuingiza madawa ya kulevya ya wapambe wake tu.
 
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Hata ndege ilikuwa kipaumbele cha ilani ya Uchaguzi mkuu
Sawa nakubaliana na wewe , maana hata walioendelea walipitia wakati mgumu sana kimaisha na kiuchumi kama nchi lkn je kipimo cha maendeleo ni nini kwani?

Maana hatuwezi sema tunaendelea au tutaendelea huku watu wanalia ukata kila kona. Angetuandaa saikolojikali kuwa jamani kwa situesheni hii hatutaweza kukamilisha yafuatayo na baada ya kufanya hili tutafanya hili ambalo lina tija kwa taifa na vizazi vijavyo

Sio tujikaze huku hatujui nini kinachoendelea mara zinanunuliwa ndege ambapo si uwekezaji wenye tija kwa taifa mara mia angejenga SGR nchi yote mastiglaz goji ambapo tunajua nishati ni muhimu na usafirishaji wa ndani ni muhimu pia
 
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Nyerere anaondoka madarakani Mimi kijana mdogo najitambua mkuu
Usibishe bila Sababu

Kama uchapa kazi wa magufuli unakuumiza roho hama nchi
Nenda zako huko, Nyerere akiwa Rais ulikuwa na umri gani? Na Mwinyi alipokuwa Rais ulikuwa unasoma wapi? Na Mr Clean alipokuwa Rais ulikuwa unafanyakazi wapi? Acha kutetea upumbavu kwa kuandika uongo wako. Brarifuuuuuu!!
 

Forum statistics

Threads 1,336,684
Members 512,696
Posts 32,547,592
Top