Zitakuja nyakati tutatamani Magufuli arudi hata siku moja madarakani

Nikuambie kitu kwa kifupi tu, wajerumani siku za nyuma wakati wa utawala wa Chancelor Gerhard Schroeder walijaribu kubinafsisha miradi mingi sana ambayo ilikuwa inasimamiwa na serikali yao.

Baada ya mda sio mrefu miradi mingi ilirudi tena mikononi mwa serikali. Unajua kwa nini? Kwasababu sekta binafsi ilitaka kuendesha hiyo miradi kwa mtindo wa " profit maximization" kitu ambacho hakikuwa rahisi kwa wawekezaji.

Ili kufanya hivyo walilazimika kuchukua baadhi ya hatua kama ku-reduce idadi ya wafanyakazi na kupunguza efficience au ufanisi wa Services ili ku-garantii ubora wa services. Matokeo yake serikali ilipata mzigo mkubwa wa kuwahudumia watu wake katika mahitaji muhimu kama energy, maji na huduma nyingine za kimaisha ikiwemo chakula na makazi.

Deutsche Bahn kwa mfano ni kampuni ambayo inatoa huduma za transport ya abria na mzigo kwa njia ya reli. Hili shirika liko to 100% chini ya serikali yao.

Hili sjirika sio tu linatoa service bali linajihusha na mambo mengi ya kiteknolojia. Majaribio mengi yanfanyika chini ya Deutsche Bahn iwe kwa faida au bila faida. Sasa niambie sekta gani binafsi iko tayari kufanya majaribio ya teknologia bila faida Tanzania?

Usi dream ndugu yangu. Ukiona vya elea ujue vimeumbwa.

Naomba mwuulize Mohamed Dewj kama yuko tayari kuwekeza kwa hao vijana walio tengeneza gari kwa kutumia baterii, usikie atakuambia nini.

Mnajua nyie wengi wenu mna maisha ya kasuku. Mkisikia jambo mtu amelitoa basi mna dakia bila kujiuliza ni kweli au sio? Inawezekana au haiwezekani?

Sekta bina is always destructive katika maisha ya community. Sitapenda kutoa maelezo mengi ukashindwa kusoma. Maana maelezo yangu nafikiri yanawachosha.

Naomba fanya uchunguzi wa kina wewe mwenyewe, ukiwa uko tayari na kama una maswali unaweza ukaniuliza tena.

Ulimwengu unahitaji sekta binafsi katika mfumo wa "Worker Cooperative" na sio capitalism kama hivi sasa. Sisi binadam tuna ung'ang'ania huo mfumo kwa sababu ya mazara, lakini ukweli wa mambo unatakiwa kubadilishwa haraka sana. Huko tunako kwenda utabadilishwa tu tutake tusitake.

Hizo mia tano tano za Magufuli zisikupe shida. Hata uwanaja wa ndege wa Chato usikubabaishe. Chato haishi Magufuli chato wako wa Tanzania. Ni vizuri wakiwa na kwanza wa ndege kwani hata wewe ilitaka unaweza kwenda uchi huko hakuna atakaye kufukuzwa.

Mmmmh! Wafanya biashara hawako Tanzania na Uganda tuna pia biashara haija anza na sisi. Hiyo ya ID Amini Dada kuwafukuza wahindi zilikuwa sababu zake binafsi. Nyerere haja fanya hivyo.

Naomba kama una nafasi basi wasikilize hawa waamerika wawili utajifunza mengi kuhusu sekta binafsi!



Nyerere alishawahi Fanya hivo kutaifisha biashara zifanywe na serikali umewahi sikia azimio La arusha,unayajua mashirika ya umma yako wapi sasa watu walisoma wakala hio nadharia ya serikali kufanya biashara inafaa Kwa jamii nyingine na si waafrica, mfumo wetu wa maisha atulazimishi kujituma hatuna nidhamu ya usimamizi wa mambo.Mashirika ya umma yalikufa Kwa kukosa usimamizi, ushindani, yakaendeshwa Kwa ruzuku badala ya faida yakawa mzigo ikabidi yabinafishwe.Kurudi kwenye makosa ya Nyerere ni matumizi mabaya ya kodi zetu itaishia kutoa ruzuku Kuendesha miradi inayofurahisha macho ya watawala huku ikiumiza wananchi.
 
Chato haijaendelezwa km mnavyodanywa kwenye media
Chato pa kawaida sana
Airport inayojengwa chato unafikiri ni milioni mbili?
Chato haina umuhimu kuendelezwa huku kuna sehemu nyingi Tanzania zenye population kubwa na rasilimali za kutosha, we niambie Chato ina nini cha muhimu sana kuwekewa airport kubwa? Labda kuna kitu sikioni. Tumegundua madini kule au?
 
Deni limedabo lakini kazi inaonekana. Si sawa na waliokopa halafu wakafanya mikopo hiyo mali zao na wake zao.
Hio miradi Kwa uchumi uliofungwa pesa kurudi ni ngumu,labda aruhusu pesa zizunguke sio kuzifungia
 
Huo ni mtazamo wako tu
Lkn makonda Kwenye swala la madawa ya kulevya amejitahidi kuyadhibiti
Mmekaa kusingizia mtandao wa madawa ya kulevya, hehehe, em niambie mtandao upi huo ambao Makonda aliukomesha? ulishawahi sikia hata mtu moja mkubwa kakamatwa toka hilo sakata lianze? Msiwe mnakuja na vitu ambavyo havina proof, makonda hajafanya chochote kudeal na wauza madawa, ni the same na kipindi cha nyuma tu, sanasana amekaa kutukana tu watu wazima kawageuza watoto wake.

Sisemi magufuli ni mjinga kukaa kimya, lazima ana sababu zake ndiyo, ila na wewe huwezi kaa ukadhani yeye ni smart kwa kukaa kimya, huwezi jua makonda ana nini cha kumfanya akae kimya, yaweza kua ni negative sio positive, au hata ikawa ni ego tu kua hapangiwi kitu na mtu, si mara ya kwanza anakurupuka kufanya jambo kwa sababu ya ego tu kujifanya kua yeye ndiye anajua kuliko mwingine nchi nzima.

Tatizo we ni sifia kila kitu, mmemgeuza jamaa kama mungu flani vile kua hana mapungufu. Kaa ukumbuke na yeye ni binadamu vilevile, ana feelings ka wengine, tena yeye ana hasira za kijinga sana kuliko mtu wa kawaida, ukitaka proof ingia online angalia hotuba zake karibia zote.
 
Acha wivu wa kitoto mkuu tutambue uchapa kazi wa mh.Rais
Kweli tunatofautiana maono, yaani na huyu Magufuri unamfananisha na Nyerere na kumuita saint?? Hata shetani ameshituka alipoona maandishi yako, anyway kumbe wewe ni diaspora
 
Ukiambiwa weka ushahidi utaleta au unabweka nyuma ya keyboard tu
Makonda alikuja kusambaratishwa waletaji madawa washindani na kutengeneza mfumo wa kuingiza madawa ya kulevya ya wapambe wake tu.
 
Hata ndege ilikuwa kipaumbele cha ilani ya Uchaguzi mkuu
Sawa nakubaliana na wewe , maana hata walioendelea walipitia wakati mgumu sana kimaisha na kiuchumi kama nchi lkn je kipimo cha maendeleo ni nini kwani?

Maana hatuwezi sema tunaendelea au tutaendelea huku watu wanalia ukata kila kona. Angetuandaa saikolojikali kuwa jamani kwa situesheni hii hatutaweza kukamilisha yafuatayo na baada ya kufanya hili tutafanya hili ambalo lina tija kwa taifa na vizazi vijavyo

Sio tujikaze huku hatujui nini kinachoendelea mara zinanunuliwa ndege ambapo si uwekezaji wenye tija kwa taifa mara mia angejenga SGR nchi yote mastiglaz goji ambapo tunajua nishati ni muhimu na usafirishaji wa ndani ni muhimu pia
 
Nyerere anaondoka madarakani Mimi kijana mdogo najitambua mkuu
Usibishe bila Sababu

Kama uchapa kazi wa magufuli unakuumiza roho hama nchi
Nenda zako huko, Nyerere akiwa Rais ulikuwa na umri gani? Na Mwinyi alipokuwa Rais ulikuwa unasoma wapi? Na Mr Clean alipokuwa Rais ulikuwa unafanyakazi wapi? Acha kutetea upumbavu kwa kuandika uongo wako. Brarifuuuuuu!!
 
88 Reactions
Reply
Back
Top Bottom