Zitakuja nyakati tutatamani Magufuli arudi hata siku moja madarakani

  • Thread starter Mikocheni Junction
  • Start date
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Ukipita mitandaoni utaona baadhi ya vijana wanavyolalamika bila Sababu

Wanamlaumu Rais magufuli kwamba maisha magumu
Ati zile maisha magumu zimeripotiwa na Rais wetu mpendwa

Tuliobahatika kuishi awamu zote tano Tunajua Mambo yalivyo na yalivyokuwa

Sisi wengine tumejifunza somo la uvumilivu tulivumilia hali ngumu kipindi cha Nyerere kutokana na Nchi yetu chini ya Nyerere kuwapinga mabeberu kwa vitendo

Mabeberu walifanya kila hila kimkwamisha Nyerere ila Kwasababu tulijua Nyerere anachopigania tulimvumilia hatukutaka tuwe wasaliti Ndani ya nchi yetu na Alifanya kazi kubwa

Baada ya hapo walipita ma Rais watatu kabla ya magufuli na walifanya kadri ya wawezavyo kuijenga Tanzania ila alipokuja magufuli tulipiga magoti kumshukuru Mungu tulijua magufuli ni nani na anataka nini
Nilikuwapo pale uhuru wakati magufuli akiapishwa sio siri nilitokwa na machozi nilimwona pia kadinali pengo akiifuta mawani yake bila shaka alitokwa na machozi

Siku ile mvua ilinyesha sana sikumbuki maneno mengi ya magufuli ila nakumbuka mstari mmoja tu alisema NiTAANZA KAZI LEO LEO Hii sentensi iliniamsha Ari ya uzalendo ule niliouamini kutoka kwa Baba wa Taifa mwl.Nyerere

Moja ya ziara za kwanza kabisa ya magufuli ilikuwa ni pale BOT baada ya ziara alisema banki kuu ni kama haina fedha maana yake zilitembea na wahuni kutokana na upole wa kikwete

Tuliomwamini magufuli tuliendelea kumwombea tulijua nguvu ya mafisadi katika Nchi Hizi maskini ni kubwa sana tulijua mafisadi watutumia kila mbinu kumkwamisha ni kweli wengine walihamisha pesa zao wengine walifunga biashara wengine walifanya kila aina ya ufedhuli kuhakikisha magufuli anakwama

Lakini miaka minne baadae Mzee yupo imara zaidi maadui zake wapo hoi wengine waliamua kuonyesha hasira zao hadharani kwa kumhujumu

Mimi binafsi nafurahi mwenyezi Mungu kunijalia uhai kushudia maajabu ya awamu ya tano awamu iliyojaa uzalendo,kupenda wananchi wake na kupigania maslahi ya Nchi
Ni bahati mbaya sana kuna baadhi ya wanasiasa na watu wasio wazalendo wanakubali kutumika na mabeberu ila hawatafanikiwa

Mimi nitawasilimua wajukuu wangu uzalendo wa Huyu msukuma toka kanda ya ziwa aliyeamua kuitengeneza ile Tanzania ya Nyerere aliyoitarajia

Ahsante magufuli ipo siku wanaokubeza watatamani urudi Ikulu hata saa moja tu urekebishe Mambo
Kwani ni ngumu kupata Rais mwaminifu na mchapa kazi kama wewe
 
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Unazungumzia siku gani mkuu

Kama nikumkumbuka Magufuli tutamkumbuka sana kwa sababu uchapa kazi wake
Haipo hiyo siku na haitakuja kutokea
 
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Kwasababu upeo wako ni mdogo huwezi kuona jinsi magufuli anavyochapa kazi
Hakuna siku katika maisha yangu sitawahi tamani huyu kiumbe arudi madarakani. Haipo...
 
P

Poa 2

Senior Member
Joined
Jul 7, 2019
Messages
134
Points
250
P

Poa 2

Senior Member
Joined Jul 7, 2019
134 250
Ona watanzania mlivyo wa hovyo
Mtu wa vyeti feki ndio unamtetea kweli?

Je sisi Watoto wa maskini tutaajiriwa wapi km vyeti feki wataajiriwa

Kwahilo namuunga mkono Rais acha vyeti feki watumbuliwe tu
Kwa hiyo sasahiv watoto wa maskini mmeajiriwa?
 
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Huo ni uzushi ni Lini magufuli alizuia Watu Mbona mama samia alikwenda kimjulia hali
Vipi alivokuwa anazuia wanaccm kwenda kumuona TL nairobi? Huo uchunguzi aliosema ufanyike umeishia wapi?
 
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Kipindi cha nyuma wakurugenzi walikuwa wanatumia muda mwingi nje ya nchi kwa kutumia pesa za mkopo kutokana na upole wa kikwete
Deni limedabo lakini kazi inaonekana. Si sawa na waliokopa halafu wakafanya mikopo hiyo mali zao na wake zao.
 
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Ahsante mkuu naendelea kujifunza kupitia nondo zako
Nikuambie kitu kwa kifupi tu, wajerumani siku za nyuma wakati wa utawala wa Chancelor Gerhard Schroeder walijaribu kubinafsisha miradi mingi sana ambayo ilikuwa inasimamiwa na serikali yao.

Baada ya mda sio mrefu miradi mingi ilirudi tena mikononi mwa serikali. Unajua kwa nini? Kwasababu sekta binafsi ilitaka kuendesha hiyo miradi kwa mtindo wa " profit maximization" kitu ambacho hakikuwa rahisi kwa wawekezaji.

Ili kufanya hivyo walilazimika kuchukua baadhi ya hatua kama ku-reduce idadi ya wafanyakazi na kupunguza efficience au ufanisi wa Services ili ku-garantii ubora wa services. Matokeo yake serikali ilipata mzigo mkubwa wa kuwahudumia watu wake katika mahitaji muhimu kama energy, maji na huduma nyingine za kimaisha ikiwemo chakula na makazi.

Deutsche Bahn kwa mfano ni kampuni ambayo inatoa huduma za transport ya abria na mzigo kwa njia ya reli. Hili shirika liko to 100% chini ya serikali yao.

Hili sjirika sio tu linatoa service bali linajihusha na mambo mengi ya kiteknolojia. Majaribio mengi yanfanyika chini ya Deutsche Bahn iwe kwa faida au bila faida. Sasa niambie sekta gani binafsi iko tayari kufanya majaribio ya teknologia bila faida Tanzania?

Usi dream ndugu yangu. Ukiona vya elea ujue vimeumbwa.

Naomba mwuulize Mohamed Dewj kama yuko tayari kuwekeza kwa hao vijana walio tengeneza gari kwa kutumia baterii, usikie atakuambia nini.

Mnajua nyie wengi wenu mna maisha ya kasuku. Mkisikia jambo mtu amelitoa basi mna dakia bila kujiuliza ni kweli au sio? Inawezekana au haiwezekani?

Sekta bina is always destructive katika maisha ya community. Sitapenda kutoa maelezo mengi ukashindwa kusoma. Maana maelezo yangu nafikiri yanawachosha.

Naomba fanya uchunguzi wa kina wewe mwenyewe, ukiwa uko tayari na kama una maswali unaweza ukaniuliza tena.

Ulimwengu unahitaji sekta binafsi katika mfumo wa "Worker Cooperative" na sio capitalism kama hivi sasa. Sisi binadam tuna ung'ang'ania huo mfumo kwa sababu ya mazara, lakini ukweli wa mambo unatakiwa kubadilishwa haraka sana. Huko tunako kwenda utabadilishwa tu tutake tusitake.

Hizo mia tano tano za Magufuli zisikupe shida. Hata uwanaja wa ndege wa Chato usikubabaishe. Chato haishi Magufuli chato wako wa Tanzania. Ni vizuri wakiwa na kwanza wa ndege kwani hata wewe ilitaka unaweza kwenda uchi huko hakuna atakaye kufukuzwa.

Mmmmh! Wafanya biashara hawako Tanzania na Uganda tuna pia biashara haija anza na sisi. Hiyo ya ID Amini Dada kuwafukuza wahindi zilikuwa sababu zake binafsi. Nyerere haja fanya hivyo.

Naomba kama una nafasi basi wasikilize hawa waamerika wawili utajifunza mengi kuhusu sekta binafsi!
 
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Naendelea kujifunza Mkuu wewe ni Mfumo wa ubinafshaji mkuu hapo juu ni Mfumo wa warltu/serkali
Nashukuru na wewe umegundua kuwa unatuchosha na utopia zako. Uchumi wa umma umefeli na uliondoka baada ya communist block kuanguka mwaka 1989 enzi za Gorbachev kwa falsafa ya Perestroika na Glasnost.

Hata kwenye syllabus vijana hawasomi tena Marxist-Leninist theories kama mfumo wa uchumi siasa, bali wanataja kidogo kama historia.

Wakeup bro Maneno Meier diaspora inakuharibu
 
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Heshima inarudi mkuu Tanzania ilishakuwa baadhi ya watu

Ila magufuli anapambana Ili kila Mtanzania ajivunie nchi yake
Nakuelewa sana bro ni kweli hi nchi ilifika sehemu akawa anahitajika raisi km Magu watu walikuwa wanapiga tu kisa baba yangu raisi
Tuliobakia tukawa tunaonekana mafara sasa hivi tunaheshimiana
 
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Huo Ndio Mfano unao relate si ndio!!
mtu anaye tamani maraika afunge mitandao ndiye unayetaka awekeze kwenye technology ya 5G ! hiyo nisawa na kumwambia kibaka avae nguo nyeupe usiku akiwa anaingia kwenye nyumba za watu kuchomoa tv.
 
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Huo ni mtazamo wako kwa sababu unamchukia Magufuli
Ukiambiwa Kwanini unamchukia sababu huna
Ondoa zile negative opinions kuhusu magufuli utaona jinsi mzee anavyochapa kazi
Sidhani kama kuna MTU anatamani IDD Amin arudi huko Uganda
 
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Mkuu magufuli hana chuki binafsi na mfanyabiashara yoyote

Hao wafanyabiashara uliowataja wengi wao walikua wanakwepa sana kulipa kodi

Walikiwa wanacheza michezo ya kihuni alipoingia magufuli alichofanya ni kusimamia sheria tu ni serakasi zikaanza
Mawazo yako na speed sana. Unafiikiria vitu vikubwa sana kutatua mambo mepesi. Sina nia ya kuku embarass lakini nataka niseme issues nyingi zinakosewa na viongozi wetu. Hebu fikiria ni kazi ngapi zimepotea kwa chuki binafsi ya Jiwe dhidi ya Yusuf Manji. Manji through makampuni yake alikuwa anaajiri watu kwa maelfu. Mtu mmoja mwenye madaraka ana kisasi naye amemvuruga na Manji kafunga viwanda na ahughuli zake yuko Canada. Wanao suffer ni Watanzania waliokuwa wanafanya kazi kwenye makampuni yake.
 
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Mtu akija kama kichaa utamjibu vipi? Waliokuja mstaarabu nimewajibu hivyo
Waliojifanya wanabangi kichwani nimewapa wanachostahili

By the way wakati Nyerere anaondoka nilikuwa kijana mdogo nilishuhudia kila kitu
Nimekwoti baadhi ya majibu yako....

Unaonekana kupaniki sana mzee wangu uliyezishuhudia tawala za awamu zote tano Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na sasa Magufuli......

Nadhani hukutegemea andiko lako kutopata uungwaji mkono wa kiwango hiki kutoka kwa wajumbe wengi bila shaka......

Pole sana mzee wangu......

USHAURI:

Ukileta hoja, jaribu kufokasi kwenye lengo la hoja yako. Wanaojadili kistaraabu unawajibu kistaarabu....

Unaohisi wanakukejeli na wakitaka kukutoa kwenye mstari, usiwadharau bali wote hao onyesha appreciation kwa michango yao kwa ingalao ku - like comment zao.....

Si lazima uwajibu kama unadhani hakuna cha kujibu.....

Wewe waache hivyo hivyo, achana na tabia ya kurushiana vijembe na matusi eti tu kwa sbb mtu hajajibu upendavyo wewe....

Kinachonishangaza zaidi mimi, ni umri wako kuwa mkubwa kwani umejinasibu kuwa umeziona na kuziishi awamu zote za tawala za taifa hili kuanzia Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na sasa Magufuli....

Kwa hiyo ni wazi umri wako umekwenda kidogo miaka pengine si chini ya 60.....

Kwa mukutadha huu, kama unaanzisha mjadala na kisha kuusimamia kwa kujibu hoja za wachangiaji kwa staili na kwa kutumia lugha hii, napata shaka na busara na hekima yako....!!

Kwa maoni yangu, ni makosa sana kuwaita watu wanaotofautiana na mtazamo wako juu ya uongozi wa Magufuli kama Rais kuwa ni wajinga na aina nyingine za matusi....

Kama huwezi kuwa mvumilivu na mwenye subira, nakushauri usiwe na account zozote ktk social media vinginevyo utam- block kila mtu.....

Bahati tu kuwa hapa JF huna uwezo huo.....

Unachoweza kukifanya kwa ushauri wangu na kama huna ngozi ngumu ya kuvumilia kukosolewa, usianzishe mada (mjadala) wowote humu, vinginevyo utamtukana kila mtu.....

Sasa hiyo ni mbaya sana maana utadhihirisha na kujifunua wazi kuwa wewe ni mtu wa namna gani.....

Mpaka hapa mimi nimeshakuelewa na kukufahamu tayari. Kuwa wewe ni Mzee mwenye shida kidogo upstairs na unahitaji kusaidiwa....!!

Mimi ni kijana mdogo tu. Nikiwa na akili za utu uzima nikisoma sekondari nimeanza kuuona utawala wa Mkapa na kidogo nikiwa mtoto utawala wa Mwinyi. Lakini naweza kukushauri na uahauri wangu ndiyo huu...uzingatie.....

Asante, nakutakia kila la kheri
 
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
2,252
Points
2,000
Mikocheni Junction

Mikocheni Junction

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
2,252 2,000
Wewe ndio akili zako zimeishia kutamka lumumba tu
Nyie vijana hamna wazazi?

Naamini huyu Mikocheni Junction ni kati ya wale wanaoitwa Buku 7 wa Lumumba. Wapo tayari kubisha na kutetea hata vitu vya kijinga ambavyo Serikali inafanya. Wanadhalilisha elimu zao kama wamesoma na heahima zao kwenye jamii. Kama hajakuelewa kwenye hiyo ushauri uliompa basi amekwisha.
 
NASRI1

NASRI1

Member
Joined
Aug 2, 2019
Messages
58
Points
125
NASRI1

NASRI1

Member
Joined Aug 2, 2019
58 125
Nilitaka kutia neno hapa lakini nahisi si neno zuri, ni bora nikaacha tu, maana naheshimu Uhuru wa Mawazo.
 

Forum statistics

Threads 1,336,673
Members 512,696
Posts 32,547,374
Top