Zipi ni dalili za mwanaume kukuchoka?

Zipi ni dalili za mwanaume kukuchoka?

Heshima mbele...

Hivi ni dalili gani ambazo mwanaume huzionyesha ambazo mwanamke ukishaziona tu, uanze kukusanya kila kilicho chako na kujiandaa kisaikolojia kwamba penzi linakaribia ukingoni na unaelekea kuachwa?

Kwenu wanaume... mke au mpenzi wako ukianza kumchoka huwa unajikuta unafanya au hufanyi nini?
mi humtonya tu live. kwa heshima na taadhima kabisa. humwambia sababu na mtizamo wa mahusiano yetu mbele, humpa nafasi ya kutafakari na kuona kama maamuzi haya ni sawa kwa pande zote
 
Tutachoka wangapi?
Mapenzi huwa yanakinahisha lakini hayachokeshi kinachotokea ni wanandoa au wapenzi kupata ishara za hisia za mapenzi kukinahi kwa sababu ya kitu kile kile kujirudia kila siku iwe ni mapenzi, chakula au muonekano wa mwenzi wako au hata mazungumzo baina ya wapenzi. Dalili hii ni ishara kwamba mahusiano yanahitaji mabadiliko hivyo kila mmoja anatakiwa kujikagua na kuangalia namna ya kuboresha na kubadili aina ya mapenzi anayotoa kwa mwenzi wake.

Kama kuna mwenye changamoto ya aina hii anitafute inbox nitamsaidia.
Unatoa msaada gani hasa?
 
mi humtonya tu live. kwa heshima na taadhima kabisa. humwambia sababu na mtizamo wa mahusiano yetu mbele, humpa nafasi ya kutafakari na kuona kama maamuzi haya ni sawa kwa pande zote
Bora hivo. Maana wengine tunakuwaga kama vipofu, bila kutuambia live hatuelewi somo kabisa
 
Wanaume huwa tunakuwa tumewaacha siku nyingi sana ile wewe wastuka ulishaachwa kitambo hata kama tuko wote tunalala na kuamka
 
Back
Top Bottom