Zipi ni dalili za mwanaume kukuchoka?

Zipi ni dalili za mwanaume kukuchoka?

Reina princess

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2015
Posts
1,322
Reaction score
1,503
Heshima mbele...

Hivi ni dalili gani ambazo mwanaume huzionyesha ambazo mwanamke ukishaziona tu, uanze kukusanya kila kilicho chako na kujiandaa kisaikolojia kwamba penzi linakaribia ukingoni na unaelekea kuachwa?

Kwenu wanaume... mke au mpenzi wako ukianza kumchoka huwa unajikuta unafanya au hufanyi nini?
 
Kama zile ambazo mwanamke anazifanya akikuchoka..MTU akikuchoka kama upon sensitive unajua mapemaaa
 
1. Anaanza kupunguza mawasiliano na hata ukimpigia simu hataki muongee muda mrefu na kingine hapendi mchati. Mara nyingi ww ndiyo unampigia simu. Ukikaa kimya hata wiki inapita hakutafuti. Akikutafuta ujue anataka penzi.
Na km utampa, hawezi kukutafuta na hawezi kukuuliza km umefika home salama. Kuna wakati namba yake inakuwa busy sana wakati wa usiku
2. Anakuwa na visingizio vingi hasa unapotaka muonane na km ukienda kwake bila taarifa lazima akukalipie
3. Ukimbana kwann haueleweki atakuambia shughuli nyingi zinambana kwahiyo anachoka. Ukidhidi kumbana sana kwann hili tatizo linajirudia sana, anaweza kukutukana au kukukalipia unasumbua.
wengine wataongezea

POLE SANA NAONA KIMENUKA HUKO
 
Anakuwa na tabia za akina Dada pindi pale wanapotongozwa na wanaume ambao hawajawaelewa....
Full kusumbuliwa na Drama za kutosha mpaka mwenyewe unaamua kujiondokea and vice versa is true.......
 
1. Anaanza kupunguza mawasiliano na hata ukimpigia simu hataki muongee muda mrefu na kingine hapendi mchati
2. Anakuwa na visingizio vingi hasa unapotaka muonane na km ukienda kwake bila taarifa lazima akukalipie
wengine wataongezea

POLE SANA NAONA KIMENUKA HUKO
Huku kimeshanuka[emoji3]

Vipi akikuambia ana mwanamke mwingine?
 
Back
Top Bottom