Epuka na usikubali kushauriwa na watu hawa katika Ndoa/Mahusiano yako.

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
37,213
85,338
1. Ikiwa unapitia changamoto yeyote, usije ukaomba ushauri kwa Ex kwasababu huyu atakushauri kwa kusukumwa na wivu ama hisia.
2. Jitahidi kuto mshirikisha rafiki wako wa karibu changamoto za mahusiano yako kwasababu, huyu ni rahisi kukushauri kwa kutumia hisia kwasababu atayabeba maumivu yako.
3. Baba na mama yako sio vizuri kumshirikisha changamoto zako kwasababu ni rahisi kukushauri akuongozwa na hisia na sio kuongozwa na akili. Na pia dam ni nzito kuliko maji.
Ushauri wangu ni huu.....
Kwa yeyote anaetaka kudumu kwenye mahusiano ama ndoa, kwanza anatakiwa awe msiri wa mambo yake binafsi. Na panapo tokea changamoto yeyote, jifunze kumaliza matatizo yako wewe mwenyewe ama na mwenzako. Sio vyema kuwashirikisha watoto wako, ndugu ama wanao kuzunguka maumivu yako.
Ikiwa utashindwa kuzikabili changamoto zako then fanya maamuzi ambayo wewe binafsi unaona yanakufaa na yatauponya moyo wako.
Good morning sunshine....🙋‍♂️
 
....... awe msiri wa mambo yake binafsi.... kwa kizazi/wazee wa zamani sawa - waliweza tatua matatizo yao na walisikilizana ... iliposhindikana baba aliondoka na kumwachia mama mazingira wezeshi kulea familia

kwa leo hii hata mie mjuajii.
 
Padre, hajawahi kuoa, anakushauri mambo ya ndoa, kwa uzoefu upi wa changamoto alioupitia yeye binafsi?
Mkishindwana nyie wawili hamna atakayeweza kuwasuluhisha
6 years back niliwahi pata changamoto kwenye ndoa, na wife alienda kwa paroko akiamini pale ndipo sehem sahihi kwa fikra zake miakaile...
Basi nilipo itwa nilienda kwenye shauri, baada ya kusilikiliza shauri lile nilimuuliza kwamba "unauzoefu wa muda gani kwenye ndoa?"
Badala ya kujibu, alikasirika na kikao kile kikavunjika palepale...🤣
Kuanzia siku ile ilibadilishwa sheria pale Parokiani kwamba migogoro ya ndoa inasikilizwa na wazee tena wazee wenye ndoa...😜
 
1. Ikiwa unapitia changamoto yeyote, usije ukaomba ushauri kwa Ex kwasababu huyu atakushauri kwa kusukumwa na wivu ama hisia.
2. Jitahidi kuto mshirikisha rafiki wako wa karibu changamoto za mahusiano yako kwasababu, huyu ni rahisi kukushauri kwa kutumia hisia kwasababu atayabeba maumivu yako.
3. Baba na mama yako sio vizuri kumshirikisha changamoto zako kwasababu ni rahisi kukushauri akuongozwa na hisia na sio kuongozwa na akili. Na pia dam ni nzito kuliko maji.
Ushauri wangu ni huu.....
Kwa yeyote anaetaka kudumu kwenye mahusiano ama ndoa, kwanza anatakiwa awe msiri wa mambo yake binafsi. Na panapo tokea changamoto yeyote, jifunze kumaliza matatizo yako wewe mwenyewe ama na mwenzako. Sio vyema kuwashirikisha watoto wako, ndugu ama wanao kuzunguka maumivu yako.
Ikiwa utashindwa kuzikabili changamoto zako then fanya maamuzi ambayo wewe binafsi unaona yanakufaa na yatauponya moyo wako.
Good morning sunshine....🙋‍♂️
Ujumbe mzuri sana huu barikiwa 🙏.
 
Sio rahisi kama unavyodhani, ukikaa nayo moyoni unaweza kufa kwa mawazo
Mkuu....
Hayo nilio yaandika nimeyaishi kwa miaka mingi chief, na kuna meengi tumejifunza ndani ya ndoa.
Lakini pia ndoa ama mahusiano meengi leo yameimarika baada ya kupitia changamoto na wengi wamedumu baada ya kukaa chini na kuzungumzia matatizo na tofauti zao.
 
Back
Top Bottom