'Zimwi la kugombea Urais CHADEMA'!

Yaani swala hili halijakukera wewe tu Ila Watanzania wote hata wale wasio wanachama wa Chadema. Napenda nichukue fursa hii kukupongeza sana kamanda Zitto kwa kuvunja ukimya na kuamua kuweka kila kitu wazi juu ya fununu zilizokuwepo juu ya kugombea nafasi ya kuwa kiongozi mkuu wa Taifa letu Tanzania, yaani nafasi ya Urais. Hongera sana brother kwa hatua uliyoifikia maana wasiokitakia mema chama chetu walitegemea ndo itakuwa mwanzo wa mpasuko wa chama na kufarakana kwa viongozi wakuu wa chama. Narudia Tena Hongera sana kwa kufanya maamuzi magumu na yenye tija kwa chama na Taifa kwa ujumla wake.
 
Gazeti halijakosea walivofanya... Wametoa Image ya Ufinyu wa Ufikiri wa Gazeti lao....
Ni kama kutoa tahadhari kwa wajuvi "This News Paper is nothing but sheeet!"
Hawana maana kabisa! Hawafikiri wala hawastahili kufikiriwa! Na wajiita wanahabari mahiri.... Sad.
 
nadhani hili si gazeti la umma,ni gazeti la watu wachache sana hapa Tz
nadhani kwa kuwa Regia ni CDM ndio hawakuweka maanani ktk msiba wake,andekuwa wa chama chao Majira ungesikia

si vizuri mfanyacho muwe mnajificha basi msiwe wazi sana,hata aibu haipo duu
 
Zito uko sawa,mara nyingi huwa nakukubali.Watu kukuongelea kuwa unapenda kugombea urais kupitia CDM ni dalili kuwa wanahisi una uwezo na wala sidhani kama ni kosa mtu kuwa na malengo kama hayo suala ni taratibu zizingatiwe na mtu akitaka kuteuliwa na chama chake asionekane kuwa anataka kukigawa chama,atakayechaguliwa na wengi wote tumwunge mkono,hiyo ndiyo demokrasia.
 
KUMEKUWEPO taarifa zinazosambazwa kwa umma kupitia njia mbalimbali za upashanaji habari, zikiwa na nia ya kuonesha kuwa kuna mbio za kuwania urais ndani ya chama na kuwa kuna baadhi ya watu wanapewa nafasi kubwa kugombea nafasi hiyo, kiasi kwamba sasa ndani ya CHADEMA “hapatoshi” kwa ajili ya kuwania urais. Chama kinapenda kutoa taarifa sahihi kwa wanachama, wapenzi, washabiki wake na Watanzania wote kwa ujumla, juu ya suala hili ambalo linaonekana kuwa na nia ya kutaka kukifananisha CHADEMA na vyama vingine au kuwafananisha viongozi wa chama hiki na viongozi wa vyama vingine ambao wamekuwa wakilifanya suala la kugombea nafasi ya urais kuwa linaongozwa na kuamriwa kwa utashi binafsi wa mtu, ukiongozwa na uchu na tamaa ya nafasi ya vyeo. Kwa sasa ndani ya CHADEMA kitu hicho cha ‘kupamba moto’ kwa ajili ya kuwania urais hakipo na wala hakiwezi kuwepo. Hasa kwa sasa ambapo chama kimejikita kuzidi kujijenga kwa kutimiza wajibu wake, kama serikali mbadala inayosubiri kupata ridhaa ya wananchi kuongoza nchi. Kwa muda huu, kwa CHADEMA suala muhimu ni namna ya kutafuta mizizi au vyanzo vya matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii pana ya Watanzania na kisha kutafuta majawabu au masuluhisho ya kudumu, kwa kushirikiana na Watanzania wote wenye nia njema na nchi yao, kwa ajili ya maendeleo ya watu. Hii ndiyo ajenda muhimu, chama kinasimamia na hakiwezi kutolewa kwenye mstari kwa watu kukimbilia urais. Kwa CHADEMA, siku zote suala la urais linategemea na kufuata mahitaji mapana ya Watanzania, kamwe haliwezi kuamriwa kwa kufuata matakwa, utashi au uchu wa watu/mtu binafsi. Na katika kufikia hatma ya mahitaji/ maslahi mapana ya wananchi, chama hiki siku zote huamua kwa kufuata na kuzingatia katiba, kanuni na taratibu zake, si vinginevyo. Ni uwezo na umakini wa kuzingatia mahitaji ya chama na maslahi mapana ya umma katika kuamua masuala mazito kwa mstakabali wa taifa, huku kikifuata katiba yake, kanuni na taratibu, ndiyo umekipambanua CHADEMA kuendelea kuwa chama makini, kinachoaminiwa kwa dhati na Watanzania, na kiupekee kuwa kinastahili kupewa ridhaa ya kuongoza nchi hii. Mahitaji ya chama na ya Watanzania ndiyo yaliyotumika kupata wagombea urais wa CHADEMA katika chaguzi kuu mbili, mwaka 2005 na 2010. kwa kuzingatia mtazamo huo, mara zote hizo mbili, wagombea waliombwa, wala hawakuongozwa na uchu au tamaa ya madaraka. Hali itakuwa hivyo hivyo wakati ukiwadia wa kumpata mgombea urais wa mwaka 2015, kamwe utashi, uchu au maslahi binafsi ya mtu hayawezi kupata/kupewa nafasi ndani ya CHADEMA. Kwa CHADEMA, urais si cheo, ni dhamana ya utumishi kwa umma, suala ambalo linazingatia masuala muhimu, ambayo ni mahitaji ya wananchi (nchi) na kisha sifa za mtu husika kuwa kiongozi wa nafasi hiyo. Basi. Kwa sasa CHADEMA na viongozi wake makini hawawezi kuanza mbio za kusaka urais, badala yake, muda wa sasa unatumika kujikita katika kushughulikia na kutafuta ufumbuzi wa vyanzo vya matatizo ya jamii yanayozidi kuongezeka, huku serikali ikiishia kushughulika na dalili/matokeo, hivyo kukosa majawabu ya kudumu na kuishia kutoa lawama kwa wakosoaji wake. Hivyo kinachopewa umuhimu ni utumishi kwa umma, kwa ajili ya maendeleo ya watu na si mbio za kusaka vyeo. Ni vyema hii dhana ya mtu kufuatwa na kuombwa, mara anapoonekana kuwa anafaa kuongoza, kulingana na mahitaji ya watu na sifa za nafasi hiyo, kama ambavyo imekuwa ikifanyika ndani ya CHADEMA, ikaenziwa na kufanywa kuwa ni namna bora ya kupata viongozi. Daima, CHADEMA na viongozi wake makini, kitaendelea kuweka mbele kwanza kabla ya kitu kingine chochote, mapambano dhidi ya vyanzo vya matatizo kama vile umaskini (ugumu wa maisha), rushwa na ufisadi mwingine lukuki unaozidi kutafuna na kuangamiza taifa na watu wake, hali inayowafanya Watanzania kuwa katika mtanziko na mkwamo mkubwa kimaendeleo, miaka 50 baada ya uhuru, huku wakiwa ndani ya taifa lenye baraka tele za utajiri wa rasilimali na kila aina ya nyenzo muhimu inayohitajika kwa maendeleo ya watu. Hii ndiyo ajenda ya muhimu kwa sasa. Imetolewa leo, Januari 8, 2012, Dar es Salaam Kurugenzi ya Habari na UeneziMakao Makuu ya CHADEMA Taifa
 
Sasa Zitto ndiye anayepatia kuendeleza malumbano wakati wa msiba? Tena Facebook?

Sasa yeye na hao anaowasema wanakuwa na tofauti gani?

Kama kweli unaheshimu msiba, hulumbani wakati wa msiba period. Utasubiri msiba uishe utalumbana mpaka liamba. Ukilumbana wakati una msiba unaonekana wewe Zitto na hao Majira wote sawa.
 
zitto tunashukuru kwa kauli hiyo. Kubwa lililobaki ni namna gani mtajipanga kugombea nafasi ndani ya chama. Hili nalo linahitaji busara sana
 
Sasa Zitto ndiye anayepatia kuendeleza malumbano wakati wa msiba? Tena Facebook?

Sasa yeye na hao anaowasema wanakuwa na tofauti gani?

Kama kweli unaheshimu msiba, hulumbani wakati wa msiba period. Utasubiri msiba uishe utalumbana mpaka liamba. Ukilumbana wakati una msiba unaonekana wewe Zitto na hao Majira wote sawa.
hajaendeleza malumbano, he just stated the obvious! It is amazing that we Tanzanians have reached here! Are those good times are gone?
 
Kweli kabisa ni suala jema kutimiza mahitaji wa wapiga kura wenu sasa kwani wakati wa mchakato wa kumsimamisha mgombea urais ukifika atatafutwa kwa njia iliyo halali tu na siyo hii wanayoittmia wanachama wa magamba kujifanya sasa ndo wanajua kutoa misaada kwa kutuhadaa ili wakishaingia ikulu watufanyie haya 2nayofanyiwa sasa.
 
Sasa Zitto ndiye anayepatia kuendeleza malumbano wakati wa msiba? Tena Facebook?

Sasa yeye na hao anaowasema wanakuwa na tofauti gani?

Kama kweli unaheshimu msiba, hulumbani wakati wa msiba period. Utasubiri msiba uishe utalumbana mpaka liamba. Ukilumbana wakati una msiba unaonekana wewe Zitto na hao Majira wote sawa.

Halumbani mkuu ametoa taarifa ya kupinga upotoshaji wa gazeti la majira.Sasa hapo kalumbana nini? RIP Regia
 
Wapuuzi sana, mimi ni kati ya watu wanao kampeni hili gazeti lisiuzike, kwa mfano ofisini kwetu haliingii kabisa kwaajili ya huu upuuzi nalichukulia kama uhuru tu.. shame on them
 
Back
Top Bottom