'Zimwi la kugombea Urais CHADEMA'!

habari za ugomvi wa kugombea urais ccm hata zisipoandikwa zipo mpaka vilabu vya pombe za kienyeji,wana kilo za kutosha za sumu ya kuuana.
chadema kama kungekuwa na mgogoro ungesubiri gazeti moja liandike siku moja na baada ya wiki mbili lingine lije na habari ileile copy and paste kweli?watanzania tumekuwa wavivu wa kufikiri kiasi hiki?

barubaru,ritz,ff,malaria sugu,rejao na wenzenu mimi nilikuwa nafikiri mnalia winga hela za mafisadi kumbe hata uwezo wa kuchanganua ni mkenge upi muingie hamna?poleni yenu na jaa zenu zitawaua.

kwanza tupo kwenye msiba.tucheni endeleeni kula dhulma zenu.
 
Tangu Mwananchi watoe habari za namna hiyo nilijua kuwa kuna Waandishi wanatumiwa na wagombea urais wa CCM kuleta minyukano CDM ili kupunguza nguvu ya CDM. Naamini habari hizo zitaandikwa tena kutoka gazeti moja hadi nyingine.
Kumbe..... mi nilidhani ni coincidence tu
 
Gazeti tuliloliamini sasa limekuwa pandikizi na lenye kufuata maslai ya watu wenye dola.
Majira badilikeni, mmekuwa ovyo sasa.

Mkuu gazeti hili lilinunuliwa tangu kwenye uchaguzi wa Igunga.wenye akili zetu tulianza kulitilia shaka tangu wakati huo.
 
Mkuu gazeti hili lilinunuliwa tangu kwenye uchaguzi wa Igunga.wenye akili zetu tulianza kulitilia shaka tangu wakati huo.
Natunza orodha ya wahujumu mabadiliko na majira mpo hivi ippmedia kodi mnalipaje vile .... Hukumu inakuja
 
Majira tunawaheshimu ila mnakosa staha kwa watanzania kwahili heshima inashuka. Tuko msibani mnatumika kwa staili mbaya. RIP Regia Mtema.
 
Ni kawaida yenu wanachadema kutokwa na mapovu mdomoni hata kwa ishu ndogo tu. Mbona gazeti lenu la tanzania daima hamlitupii macho?
 
MAJIRA ni wehu kabisa!
ZITTO amenena;je ni ya kweli hayo zitto?
Songa mbele CHADEMA!
R.I.P REGIA!!!
 
Kama tunakumbuka vizuri gazeti hili liligeuka toilet paper tangu mmiliki wake wa awali Mh. Richard Nyaulawa (Mb - Mbeya Vijijini - CCM) afariki. Ni kipindi hicho Shitambala alipogombea kupitia Chadema lakini kwa njaa zake akauza haki yake ya ushindi kwa CCM na hivi leo (Shitambala) karudi CCM jumla. Mwenye ufahamu na afahamu.
 
Kauli yako nimeipenda sana Zitto maana tatizo si kila mtu rais , tunachotaka ni viongozi makini kama nyie muingie serikalini haijalishi kuwa nani ni nani, ili mradi serikali iwe chini ya CHADEMA, narudia tena kuwa ZITO NIMEIPENDA KAULI YAKO.
 
Hongera Zitto! kweli sasa umekomaa nadhani unatakiwa kugombea 2020, nilikuwa napinga kabisa wewe kugombea 2015 kwasababu naamini Dr Slaa bado anafaa zaidi na kama akishinda basi tukutegemee 2025.
 
Ni kawaida yenu wanachadema kutokwa na mapovu mdomoni hata kwa ishu ndogo tu. Mbona gazeti lenu la tanzania daima hamlitupii macho?

Funga domo lako wewe.Ni ishu ndogo huu msiba mkubwa wa kitaifa? Tafadhali kaa mbali.Kama huna cha kusema usidhalilishe wafiwa wala marehemu.
 
Mkuu Molemo hili nalo gazeti la kusoma? Mara ya mwisho nililinua miaka 4 iliyopita nilipoambiwa jina langu lipo humo ili kujiunga na Chuo kikuu

Mkuu hakika hawa watu wamenikera sana.Inaonekana wamefurahia sana huu msiba na sasa wakaona tuwasambaratishie hapahapa kilioni.Ee Mola waangalie watu wako
 
Mkuu Molemo,nakuunga mkono kwa asilimia mia.Nimepata mshtuko mkubwa baada ya kusoma upuuzi wa gazeti la majira.Walishindwa tu kuungana na Chadema katika kipindi hiki kigumu? Nakubaliana na Molemo wanaChadema wote kususia gazeti hili la Majira.

Asante mkuu kuniunga mkono mpaka sasa nimepata PM 129 za wanaJF wakiunga mkono kususia hili gazeti kwa unyama waliofanya.
 
Mh Zitto katika update yake ya facebook amefafanua jinsi alivyosikitishwa na habari za baadhi ya magazeti hususan majira. Pia amefafanua na kumaliza ile minong'ono kuwa anajiandaa kugombea uraisi. Katika dokezo hilo Zitto ameandika.
"Ona Watanzania na baadhi ya vyombo vya habari. CHADEMA imepata msiba mkubwa, imefiwa na Mwanachama, Mbunge, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Kivuli wa Kazi na Ajira. Lakini Gazeti la Majira linabeba habari ya kwanza 'Zimwi la kugombea Urais CHADEMA'! Hata staha ya msiba watu wanakosa. Nimeshangazwa sana na gazeti la Majira kuumbua zimwi lisilokuwepo. Sigombei Urais 2015. Nitamwunga mkono mgombea wa CHADEMA"

zittokabwe.jpg


Chanzo: Ughaibuni.com
 
Back
Top Bottom