'Zimwi la kugombea Urais CHADEMA'!

Zitto Kabwe


Ona Watanzania na baadhi ya vyombo vya habari. CHADEMA imepata msiba mkubwa, imefiwa na Mwanachama, Mbunge, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Kivuli wa Kazi na Ajira. Lakini Gazeti la Majira linabeba habari ya kwanza 'Zimwi la kugombea Urais CHADEMA'! Hata staha ya msiba watu wanakosa. Nimeshangazwa sana na gazeti la Majira kuumbua zimwi lisilokuwepo. Sigombei Urais 2015. Nitamwunga mkono mgombea wa CHADEMA



https://www.facebook.com/zittokabwe

Hayo ni maneno ya hekima, Zito. Sisi wapenda mabadiliko wote ni lazima tuseme hivyo. TUPO TAYARI KUMWUNGA MKONO MGOMBEA YEYOTE AMBAYE CHAMA KITAKUWA KIMEMPITISHA KWA TARATIBU ZINAZOKIONGAZA CHAMA. Tufahamu na tuamini kuwa ni Mtanzania mmoja tu, ambaye ataungwa mkono na sisi wote, ndiye atakayeweza kusimama na kuwawakilisha Watanzania wote wapenda mabadiliko katika nafasi ya mgombea Urais. Kuna mbinu nyingi zinafanywa za kuonesha umma kuwa Mh. Kabwe Zito hayupo pamoja na viongozi wenzake katika mambo mengi. Ni vizuri na ni muhimu Zito kila mara kutolea ufafanuzi kauli zote zenye hila ya kufitinisha na kugombanisha uongozi na wanachama wa CHADEMA. Zito, kauli yako nimeipenda.

SISI TUNAOMBOLEZA WENZETU WANAHANGAIKA NA KULETA FITINA. Kwa kuwa nia ya Majira tumeijua, adhabu kubwa tunayoweza kuwapa ni kupunguza mauzo yao kwa kususia kusoma upuuzi.
 
Back
Top Bottom