Zimua (msamiati mpya)

Watu wanazimua miaka yote hamna jipya hapo. Ukipiga mitungi kesho yake unazimua kupunguza mning'inio!
 
Msamiati huu nimeupata leo ukiwa na maana refresh. Nimeipenda sana hii, naomba tujulishane misamiati mingine ya Kiswahili
Asante kwa neno hilo "zimua".
Lakini wewe umeuita huo ni msamiati mpya wa kiswahili na kwamba unaomba upewe "misamiati mingine" ya kiswahili. Ndugu, neno "msamiati" halina maana ya neno gumu. msamiati ni jumla ya maneno yote yanayounda lugha moja. Kwa hiyo tunao msamiati wa kiwahili, kiingereza n.k. Hayo uliyoyataka ni maneno mapya (au tuseme mageni) katika msamiati wa kiswahili. Kwa hiyo kule shuleni mwalimu alipokuwa anatufundisha "msamiati" maana yake ni kuwa alikuwa anaboresha uelewa wetu wa msamiati wa kiswahili. sio alikuwa anatufundisha "misamiati" mipya. Ukishasema "misamiati" tayari unazungumzia lugha zaidi ya moja.
Nawasilisha.
 
asante sana senior bachelor , ambaye naamini una hawara wengi waliokupa huo u-senior.. ni kweli kabisa msamiati ni jumla ya maneno yote (yaliyokwisha sanifishwa na kukubalika na jamii) yanayounda lugha fulani, hivyo naamini hata neno ZIMUA ni msamiati wa lugha ya kiswahili unaounda lugha hii, kwa mtazamo na kwa uelewa wangu nilionao, nadhani mwanzisha mada alimaanisha ni msamiati ambao kwake yeye ameona ni mpya katika misamiati aliyoifahamu kuwa inaunda lugha ya kiswahili, hivyo ni sahihi kuuita kuwa ni msamiati ambao ni neno la kiswahili.
nawasilisha.... asante kwa maada.
 
Msamiati huu nimeupata leo ukiwa na maana refresh. Nimeipenda sana hii, naomba tujulishane misamiati mingine ya Kiswahili

Sidhani kama uko sahihi kwani mimi hili neno nalifahamu tangu siku nyingi na tulikuwa tunalitumia wakati wa practical za pharmacy kwenye maelekezo ya dawa.ZIMUA ni sawa na DILUTE.
 
asante sana senior bachelor , ambaye naamini una hawara wengi waliokupa huo u-senior.. ni kweli kabisa msamiati ni jumla ya maneno yote (yaliyokwisha sanifishwa na kukubalika na jamii) yanayounda lugha fulani, hivyo naamini hata neno ZIMUA ni msamiati wa lugha ya kiswahili unaounda lugha hii, kwa mtazamo na kwa uelewa wangu nilionao, nadhani mwanzisha mada alimaanisha ni msamiati ambao kwake yeye ameona ni mpya katika misamiati aliyoifahamu kuwa inaunda lugha ya kiswahili, hivyo ni sahihi kuuita kuwa ni msamiati ambao ni neno la kiswahili.
nawasilisha.... asante kwa maada.
Asante kwa jibu lako.Kwanza nikusahihishe. Si kweli kwamba kuwa mseja mwandamizi "senior bachelor" eti maana yake ni kuwa na mahawara wengi. Hii inamaanisha kuwa na umri aghalabu mkubwa bila kuoa. Watu wenye mahawara wengi tunaweza kuwaita mafuska. Hii ni kwa kuwa dhana ya hawara inatumika kumuelezea mtu aliyeoa/olewa au ambaye bado kuoa/kuolewa mwenye uhusiano wa kingono na mtu aisye mkewe/mumewe. kwa kuwa mseja mwandamizi au la sio sababu ya kukufanya uwe na uhusiano na wake za watu.Pili nasisitiza kuwa neno "msamiati" linabeba dhana ya "jumla ya maneno yote yanayounda lugha moja". Kamwe neno moja, mathalan "zimua" haaliwezi kuwa msamiati. Hilo ni neno tu katika msamiati wa kiswahili.Nawasilissha.
 
Back
Top Bottom