Zimbabwe: The turmoil, reconciliation, and the future!

Zimbabwe: The turmoil, reconciliation, and the future!

Dua,
Unajua nyie vijana wa siku hizi mna dream za ajabu ajabu!...Sasa hicho kizazi Kipya kinakuja na nini? kuwa asubuhi saa moja kunasaidia nini kama huna kazi?...real change na real freedom itakujaje ikiwa ardhi ipo chini ya mkoloni uliyepigana naye kwa miaka!
I mean mnalaumu tuuu kila siku wakati solution ya matatizo hamna na kila mnachozungumza ni maneno ya mzungu sio kutoka kichwani mwenu, ndio maana hamna ushahidi wowote zaidi ya ule wa mzungu.
Mugabe aondoke hilo sii tatizo wote tunaopmba hivyo, lakini nambie nani aje mwenye sifa kama ulizozitaja -huyo kizazi kipya nani?, Sio kusema tuu hali huna kiongozi mwingine mkononi. Nchi bila kiongozi ni sawa na Somalia bila Maj. Gen. Mohamed Siad Barre....au Iraq bila Saadam. Kuna viongozi madikteta lakini ndio pekee wanaoweza kupambana na watu wake..Mugabe ni mmojawapo.
 
Mkandara

Dream iko wapi hapo? Nafikiri wewe ndio unaota tena ndoto ya usiku wa manane, ardhi ipi iko chini ya mkoloni wakati wazungu walioko Zimbabwe na Wazawa wa Zimbabwe wamekubaliana ardhi ni lazima ichukuliwe na ambao hawajapata ardhi ndio wanaolalamika na Mugabe kaweka pamba masikioni na kupata washabiki wengine. Hata msemo wa saa moja asubuhi hufahamu Mugabe (killer) ana miaka 80 (saa kumi na mbili jioni - jua linazama siku yake imeisha) sijui ana siku ngapi za kuishi? Hana wazo jipya yeye ni kupiga wapinzani na kuiba pesa ya walipa kodi pamoja na kuwapa mashamba ndugu na marafiki zake. Unataka soulution gani kama sio ya kumwondoa Mugabe (dictator) ataingia kwenye history books kama Bokasa, Mobutu, Banda na rafiki zake. Sina sababu ya kukwambia nani aje kwani umesikia Zimbabwe aliyesoma ni Mugabe peke yake? Yeye alitokea wapi? Mbona unakuwa na mawazo kama hayo? Basi wewe subiri lakini swaiba yako anaondoka tena hamalizi hata muda endelea kusubiri na utaona nani ataongoza Zimbabwe yeye akiondoka.

Sawa mie kijana na wewe mzee: Nyie wazee hamna mawazo mapya tena, mawazo yenu yamefilisika kitu mnachokimbilia ni oh mnatumiwa na wazungu, kila kitu mnatumiwa na wakoloni wakati ukweli unawasuta. Nani alimwambia Mugabe aende kuchoma nyumba vijijini ili wasiwe na pa kuishi - wazungu! HONGERA NAONA HAMNA TOFAUTI NA MAWAZO YA MUGABE.
 
Dua,
Naona hapa tunazungumza lugha mbili tofauti. Nadhnai nitaachia hapa maanake nazungumzia ukubwa wa tembo na kipofu. Huo msemo wa Mugabe nimekujibu vizuri kuwa hiyo asubuhi ina faida gani kama huna kazi?...sasa wewe ndio hukuelewa mapana ya msemo wako mwenyewe.
Hizi habari za ujana, kusoma na leadership dikteta zinahusiana nini?
Bob sioni hoja kabisa zaidi ya matusi na chuki kwa Mugabe, which won't solve the main problem.
Uzee nini hasa ikiwa zina charge! mimi hapa ndio naingia 10 la mwisho kulingana na umri wa kisayansi kwa mwafrika lakini bado kabisaaaa! Kuna vijana wenzako kibao wanategemea mwongozo toka kwangu na bado mimi hapa napata mwongozo toka kwa wakubwa zangu.. mwongozo ambao una uhakika na namshukuru Mungu mambo yangu yanakwenda saaafi.
Umri mjomba sii kitu ujana wenu ndio huo tunayaona matunda yake. Namba kubwa ya waathirika wa Ukimwi ndio age yenu hiyo ya asubuhi,wenye elimu.... elimu????!!!!
Nilikuwepo... haitusaidii kitu hii habari ya Mugabe ila utakuja nambia siku ya siku.......Utabiri wangu umekamilika!
 
Mkandara, I think hapa kuna factors nyingi kwa haya matatizo. MY PROBLEM NI KUONA wewe unamuabsolve mugabe na haya matatizo ukisema shida ni west na ardhi. Mimi nadhani Muungwana Dua anachokisema hapa ni kwamba Mugabe has failed, though wazungu have contributed.... Land policy zake ni disaster. He must admit and go back to the basics. Hakuna anayesema wazungu wapewe ardhi yote. Ila sidhani kama wazungu wamekataa kupewa ardhi kwa mkataba..lease! Kama una ushahidi wa hili let me know. But for sure hili swala la ardhi, lilifanyika KISIASA NA WALA SI KWA MISINGI YA KIUZALENDO, as people would want us to believe. Mugabe MUST COME BACK TO THE BASICS. Wazimbabwe wanalijua hili ndo maana All along I have said, ardhi ni mali ya wazimbabwe, lakini Mugabe did what he did thinking hakutakuwa na consequences! Iam sure Mugabe kama aliweza kuwafukuza kutoka kwenye nyumba zao..kwa nini asingepitisha sheria za kuregulate use of land? sheria zilikuwepo wakakataa kuzifuata?, Mugabe ameruhusu..sheria na mahakama za ZIM kuwa kichekesho. One can decide to follow the law or not! Its a tragedy..tusitetee uozo hapa this man has failed his country for his personal gains! Tunavyoongea hapa ni kwamba High Court inaweza kutoa judgment na ZANU PF wakasema hii judgment hatuikubali na kwa hiyo hatuifuati.....mara ngapi order zimetolewa kuwaruhusu hawa wazungu warudishiwe hata nyumba zao lakini wapi......
 
Mikuki,

Kama nilivyosema toka awali kuwa mimi huwa sizui mambo. Ila hujaribu kufuatilia swala with open mind.. sitaki kumhukumu mtu kabla sijapima ktk mzani wa maono yangu.
Kama umefuatilia mada hii utaona ya kwamba nimeweka vitu vyote wazi ambavyo navitetea na kutoa maelezo yangu zaidi ya kunyoosha kidole, lakini kila napofanya hivyo hoja naona issue inabadilika na kuwa mimi mhusika zaidi kwa sababu namtetea Mugabe. Nadhani muhimu ni kutazama content za matetezi yangu badala ya kumtazama Mugabe ni nani!
Hii ndio mbinu westerners wanataka tuikubali hali Mugabe asingekuwa mtu mbaya kwao kama swala la ardhi lisingejitokeza. Kwetu sisi Waafrika Mugabe alikuwa mbaya hata kabla ya swala la ardhi kwa hiyo hukumu ya Mugabe tunayo sisi na kwa mashtaka yetu siyo yao kupewa kipaumbele.
Pili, umeuliza swala la Mugabe kutaka kurudisha ardhi na uhakika wa mpango huo. nakuomba soma link hii kisha soma maelezo ya wachangiaji.

Nakubaliana na wewe sana kwamba Mugabe na utawala wake lazima watafute njia ya kuondokana na njaa iliyopo lakini isiwe kwa gharama ya wananchi wake na ridhaa yao ndio muhimu zaidi kwa sababu unaweza kuwaridhisha nchi za magharibi lakini ukazua matatizo ya ndani. Pia nadhani hizo ardhi kubwa yenye rutba iko zaidi kwa hao Ndebele kama sikosei. Hapa najaribu ku avoid kile kinachotokea Iraq leo hii ama Somalia maana yangu hasa ni tuwe na upeo zaidi ya Mugabe mwenyewe ktk maamuzi na utetezi wetu.

Link hii hapa:-
http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/4937310.stm
 
Mikuki,
Mpaka sasa hivi serikali za UK na US hazijawafidia wazungu walionyanganywa ardhi yao. hao walipaswa kulipwa kutokana na makubaliano ya Lancaster.

Kila mara BBC wanalalamika kwamba Mugabe kachukua ardhi bila kuwafidia wazungu. Hivi kuna mtu mwenye akili timamu anaweza kudai Mugabe atumie kodi ya wazalendo wa Zimbabwe kulipia ardhi iliyoporwa toka kwa mababu zao? Mugabe angesikiliza ushauri huo angekuwa hai leo?

Nilileta makala hapa inayoonyesha kwamba hata wazungu wakulima wakubwa wana matatizo sasa hivi kutokana na ukame. Land policy ime-fail kwasababu ya vikwazo vya uchumi, na ukame wa muda mrefu. Pamoja na kupewa ardhi, hao wakulima wadogo-wadogo walihitaji msaada wa pembejeo na mafunzo ili waweze kuzalisha.

Land redistribution is not something that was "invented" by Robert Mugabe. USA ilishasimamia zoezi kama hilo ktk nchi za Asia. Isnt it ironic that USA is condemning Mugabe for redistributing the land, something that the USA did in Asia?
 
Selling fish to Mugabe is risky business
Zim Online

Tuesday 15 May 2007

By Nigel Hangarume

HARARE - Zimbabwean soldiers at the weekend severely beat up fish vendors in
the working class suburb of Kuwadzana in Harare for displaying baskets of
fish to President Robert Mugabe's passing motorcade.

The soldiers, who were armed with rifles and truncheons, accused the hapless
vendors of insulting Mugabe after they displayed their "smelling fish" to
the President.

It was not clear if the vendors had moved towards the passing motorcade in a
bid to beg Mugabe, who was traveling from his rural home in Zvimba, to buy
some of their fish.

Under Zimbabwe's tough security laws, it is an offence to make offensive
gestures or swear at Mugabe's motorcade.

The law says that a person "shall not make any gesture or statement within
the view or hearing of the state motorcade with the intention of insulting
any person traveling with an escort or any member of the escort".

The vendors told ZimOnline on Monday that all hell broke loose when some
soldiers returned to the scene, about 20 minutes after Mugabe passed through
the suburb.

"First they asked why we were showing off our fish to Mugabe and then they
started beating us randomly," said Norbert Marenga, one of the vendors.

"One of the soldiers said the President was angry because we were turning
the roadside into another Mbare Musika. The soldiers said we were
embarrassing the government by openly showing off our poverty to the
President."

Army spokesperson Colonel Simon Tsatsi could not be reached for comment on
the matter last night.

The Zimbabwean government two years ago violently removed all vendors from
roadsides in a military-style clean-up crackdown dubbed Operation
Murambatsvina.

But the vendors have slowly returned to city pavements and on the road sides
as a seven-year old economic crisis most people blame on Mugabe's
mismanagement deepens. - ZimOnline.
 
Mikuki,

Ningekuomba ulifuatilie swala hilo zaidi ya makala hiyo. Ebu tazama huyo aliyesema kwamba askari mmoja alisema kuwa Mugabe alichukia kuonyeshwa samaki waliooza!..
Sasa tujiuliza huyo askari alikuwa na ukaribu gani na Mugabe hata kusikia Mugabe akisema hayo?..
Yawezekana kweli kasikia na kumwambia huyo jamaa na nini madhumuni hasa ya hawa watu kuchukua samaki waliooza ktk msafara wa rais?...Historia inatuonyesha kuwa mara nyingi samaki waliioza huwa ni ishara ya serikali mbovu yaani mnawatupia msafara samaki waliooza ama mayai viza....Je, hili ndilo lilikuwa lengo la hawa wauza samaki ktk mtaa ambao hauuzwi samaki?
Kitendo kama hicho huwa kina gharama zake!. Gharama ambazo akina Mandela wamekwenda nazo bega kwa bega hadi wamefanikiwa. Hawakuhitaji hisani ya mtu ama kulia kwa sababu walichokusudia kukifanya walikusudia kweli na kutegemea adhabu. Walikuwa tayari kuzitoa nafsi zao dhidi ya uongozi mbaya.
Kisha kitendo cha Machinga wa Harare ilikuwa vurumai tofauti na kwetu Dar. Machinga wetu hawakujitokeza kupinga serikali kwa kutumia nguvu tofauti na wenzetu wa Zimbabwe. Machinga wetu walikuwa wepesi kukubali na wanyonge chini ya sheria ya serikali hata kama ilikuwa mbaya. Na kusema kweli Dar leo hii inatazamika kuliko ilivyokuwa awali!...Hiovyo basi sioni ubovu wa operation zinazoondoa uchafu, wizi na madhara mengineyo yanayotokana na Machinga mjini.
Kwa hiyo ukitazama sana utaona tofauti ni kati ya wananchi wa Zimbabwe na Tanzania ama nchi nyinginezo ktk kutafuta haki..sisi wepesi sana kumwachia Mungu.
Yanayotokea leo hii TZ yasingepata nafasi Zimbabwe wananchi wake hawakubali mzaha hata kidogo. Kwa hiyo nguvu anayotumia Mugabe ni kubwa zaidi kuliko Mkapa ama JK kwa sababu Upinzani ni mdogo kwetu hapa...
Yote bado tunarudi kule kule kuwa Mugabe ni kiongozi mbaya sana lakini swala la ardhi bado ni kubwa kuliko tunavyolifikiria. Viongozi wa Zimbabwe wamejitajirisha wenyewe kama walivyo viongozi wa TZ , Kenya, Uganda You name it isipokuwa tu kuna nchi wananchi wake hawataki upuuzi na mapambano yanakuwa makubwa zaidi na ndipo unaweza kupima mapana ya udharimu wa kiongozi.

Kifupi Afrika hatuna viongozi ila watawala na wote ni wabaya sana isipokuwa tu wanapishana kutokana na nguvu ya Upinzani..Afrika hakuna demokrasia sii Zimbabwe wala wapi!
 
Mikuki

What a story, naona wauza samaki walitaka angalau anunue wapate vijisenti kidogo kumbe noma.
 
Ndugu wana JF,

Kuna kitu huwa nakiita ukada ama uzalendo pofu ambao mara nyingi wanajamii fulani huwa wanakuwa nao katika kuchambua matatizo na mafanikio katika jamii zao.

Hali hii huwa naiona ikitokea kila mara katika mjadala wa Kamarade Mugabe na Zimbabwe kama ilivyo katika Mjadala wa Sudan na darfur. Hili sio jambi jipya maana hata wakati Iddi Amini anafanya yake wapo waliokuwa wakimteteaa kwa kutumia vigezo kama vyako. Actually hadi sasa wapo wengi tu wanaoamini kuwa Amini alikuwa hana makosa kama inavyosemwa ispokuwa ni longolongo la wazungu tu. Hata mimi kuna wakati huwa mawazo kama hayo yananijia.

Suala la Kamarade Mugabe ni chachu kwa waafrika kuwa macho wazee wetu na hata vijana wenzetu ambao wanakuwa na sura ya uanamapinduzi wakati kwa upande mwengine ni mufilisi kisiasa, kiimani na hata kidira. Kamarade Mzee Mugabe ni mmoja wapo. Si unajua hata nyumbani tunao wengi tu......magwiji na wale wanao ibuka kama uyoga??

Wakati tukitambua kuwa hawa manyang'au wa magharibi wana mikono yao tena mikubwa tu ni muhimu vilevile tuwe na ujasiri wa kunyooshea vidole hata wale tunaowaona kuwa ni mashujaa wetu.

Hivi sasa hali ni mbaya mno huko Zimbabwe na kama haijatokea nguvu ya kisiasa miongoni mwa wanaharakati ndani na nje ya ZANU PF ni wazi wanajeshi ambao bahati mbaya wamejaa aina ya Mugabe watanyakuwa uongozi wa nchi na hiyo sio habari njema kwa Wanazimbabwe.

Ni bahati mbaya zaidi kuwa hadi sasa upinzani uliokuwepo ni hovyohovyo ukiongozwa na "demagogue" mwingine ambaye anamfanya Kamarade Mugabe kuwa malaika.

Naomba ndugu zangu tuamke kutoka katika usingizi usingizi huu wa uzalendo pofu unaotufanya wengi wetu tushindwe ama kujirudi au kusimama kidete kupambana na uhuni wa waheshimiwa wetu ambao wengi tunawaona kama mahusjaa wetu.

Tanzanianjema
 
Tanzanianjema,

Ndugu yangu unapotoa hoja na kuiacha ktk mafumbo inakuwa vigumu kwetu kuelewa unachozungumza.
Nafikiri mada hii inahusu Uhusiano wetu na Zimbabwe...
Hili ni somo kubwa sana zaidi ya fikra za baadhi ambao wanataka tuamini kitu kimoja tu.
Nitakwambia kwamba, mimi naunga mkono kabisa uhusiano wetu na Zimbabwe kwa sababu hawa jamaa ni ndugu zetu na tulikuwa nao katika mapambano ya Uhuru wao na kutokomeza apartheid. Yes, leo hii wamekumbwa na jinamizi jingine toka ktk zimwi likujualo!
Sasa hapa tunatengana zaidi ni kuhusu Mugabe himself kama kiongozi. Na nakuomba uelewe ya kwamba msimamo wangu kuhusu Mugabe kama rais wa nchi ile hautofautiani na mtu mwingine yeyote isipokuwa siamini kabisa kwamba kumwondoa Mugabe ndio suluhisho la matatizo yao.
nakuomba ukumbuke tu hata Marekani walipotaka kumwondoa Saadam madarakani kuna viongozi wa nchi na hata UN walikataa. Hii haikuwa na maana walikuwa na uzalendo pofu, laa walitazama na kutanguliza maslahi ya nchi ile kabla ya Saadam. Kisha hata Nyerere alipokuwa akijaribu kuwapatanisha Habyalimana na Kagame, pamoja na kwamba Habyalima alikuwa hapendwi, Nyerere alikuwa akiyafanya hayo kwa maslahi ya Wanyarwanda.
Kutosikia ama kutazama mbali kwa Marekani na kule kwa Kagame ndiko kulikosababisha matatizo yote haya ambayo ni makubwa kuliko thamani ya kuwaondoa vibaraka ktk Uongozi.
Nachodai mimi ni kwamba Zimbabwe wamehukumiwa kwa sababu ya mtu mmoja - Mugabe! hali Wamarekani na Uingereza wanaweza kabisa kumwondoa ktk uongozi lakini wanafahamu kwamba kumwondoa Mugabe dikteta kutazua genocide ndani ya Zimbabwe.
Sasa basi akiondoka Mugabe kesho nani atashika madaraka? napenda sana aondoke lakini tukumbuke tu swala la Adrhi limepitishwa bungeni na ZAPU-PF wataendeleza zoezi hilo ambalo haliwezi kuondoa njaa kwao.
Pili, swala la ardhi halina ufumbuzi kwa wazungu zaidi ya kurudishiwa ardhi yao, jambo ambalo wananchi wa Zimbabwe (weusi) hawaliafiki isipokuwa vibaraka wa MDC. Na kama kuna watu wanaotumia njaa kwa kampeni ya kisiasa ni hawa jamaa kwa sababu hawawezi kusimama na kuuambia Umma kwamba lengo lao ni kurudisha ardhi kwa wazungu...
Kutoweza kusema hivyo kulimpa Mugabe ushindi ktk uchaguzi uliopita baada ya yeye Mugabe na chama chake kuzisema siri za hawa wapinzani! na waliitwa kweli vibaraka wa Blair!...kwa sababu walitaka kurudisha ardhi kwa makaburu... Mugabe na chama chake won the election. Kwa hiyo unaweza kuona jinsi swala la ardhi lilivyo sensitive!

Sasa tuache hili swala la uzalendo pofu, wewe nambie njia gani ambayo unaona itumike kuweza kuondoa matatizo ya Zimbabwe baada ya maelezo yangu yote!..
Huo uchafu wa Mugabe ama huko Darfur ni vitu vya kujadiliana. Ufumbuzi wa haya maswala sii mdogo hata kidogo tena yanatofautiana sana zaidi ya kuwa Afrika tuna TAWALIWA na wananchi wetu wenyewe. Je, solution ni kutokuwa na rais kabisa? maanake kila rais Afrika hana ridhaa ya wananchi ktk utekelezaji ila ridhaa ya wananchi wakati wa upigaji kura zao.
 
jamboonormal_ukraine2.jpg


SERIKALI YETU YA JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA INAVYOWATREAT HAWA HAKUNA TOFAUTI NA SERKALI YA ZIMBABWE
 
_41341557_cupboard-afp203.jpg


Zimbabwe slum evictions 'a crime'

The forcible eviction of 700,000 people from slums in Zimbabwe in 2005 was "a crime against humanity", according to independent legal opinion. The human rights groups that sought the legal advice, say the issue could now be referred to the International Criminal Court in The Hague. Zimbabwe's government called Operation Murambatsvina an urban clean-up campaign to remove illegal structures. But the United Nations condemned the demolitions of shops and homes.

The Geneva-based Centre on Housing Rights and Evictions and another group, Zimbabwe Lawyers for Human Rights, sought independent legal opinion. This concluded that the evictions in Zimbabwe were a widespread and systematic attack against a civilian population, as part of state policy.

"What happened in Zimbabwe was akin in magnitude to the Asian tsunami," Zimbabwean human rights lawyer Alec Muchadehma told reporters in The Hague. The finding is that Operation Murambatsvina was a crime against humanity, and the UN Security Council therefore has authority to refer the matter to the International Criminal Court.

"We believe it is now time for the Security Council to take up this issue and we are calling on all 15 members ... to put it on the agenda and officially debate it," said Malcolm Langford, of the Geneva-based Centre on Housing Rights and Evictions. The programme to build new homes to replace those demolished has faltered, says Amnesty International in its 2007 annual report. "By May (2006) one year after the programmes launch, only 3,325 houses have been built, compared to 92,460 housing structures destroyed in Operation Murambatsvina," it said.
In recent years, millions of Zimbabweans have left the country as it grapples with runaway inflation, high unemployment and food shortages.
http://news.bbc.co.uk/go/pr/fr/-/2/hi/africa/6683619.stm

Sasa hili swala ni kazi ya UN kulishughulikia Mama Migiro kesi hiyo........................Hawa hawakuwa machinga ni nyumba ambazo watu walikuwa wanaishi.
 
Profesa Tibaijuka ni kati ya viongozi wachache wa kiafrika walaiokandia sana serikali ya Mugabehas apale alipopitisa operations Murambatsvina ya kubomoa vibanda vya machina waliokuwa wanvamia jiji la hararae kutokana na "njaa kali". Siku zote hizo, mahasidi hawa wawili hawajawai kuonana usoa kwa uso. Hivi majuiz walikutana ana kwa ana. Hebu jionee picha hapa

Ninaona kama Mugabe alikuwa "akijipendekeza" kuweka maongezi na Tibaijuka huku huyu mama akim-ignore.
 
mugabetibaijukabig.jpg


Arriving in Kenya for a summit of the COMESA trade block this week, Mugabe came face to face with Tibaijuka -- who is also COMESA's secretary general -- for the first time since her report which his government condemned as unfair and unbalanced.

Judging from the body language in our photo essay, you didn't need to be on that red carpet to know what exactly went on.




Mzee mzima amekosa busara iliyobaki ni kujikomba komba

Kichuguu

Take 5
 
ukraine2.jpg


NDUGU ZETU HAWA...WANAWEZA KUWA MADAKTARI,MAINJINIA,NA WATAALAM WA KILA NYANJA...LAKINI HIYO KWETU SIYO MUHIMU....MUHIMU. TUNAWEZA KUFANYA MASHEREHE YA IFAHARI LAKINI KUWALIPIA AU KUWATAMBUA HAWA SIYO MUHIMU KABISAAA

JE BADO UNA IMANI NA SERIKALI YAKO TUKUFU?

JE KULIKUWA NA HAJA GANI AKINA ADAM SAPI KUPIGANIA UHURU WETU?

MZEE KINJIKETILE AKIFUFUKA LEO ATASEMAJE?

WATAWALA WETU WANGEWEZA KUMTAZAMA MWALIMU NYERERE MACHONI?
 
Kichuguu,
Mzee wangu samahani lakini hawa watu wameingia mkutanoni pamoja! on red carpet together unajua tena north America huwa na ishara gani!
Hiyo sura ya Tibaijuka imesha choka, akicheka kama analia kama Mugabe mwenyewe!
Kwa hiyo kama kulikuwepo na lolote wasingeingia pamoja!...Tazama hata sura za walinzi! Mkutano umehudhuliwa na viongozi wangapi asiwe nao ila Mugabe!... jamani huu ndio msimamo wa nchi yako na kama unaupinga ni bora kuweka maelezo na sio picha za bwana na bi harusi ktk ndoa!.
 
Na UN ndo haiwezi kumwambia kitu Mugabe! UN is always seen as a tool of the west to advance their agenda. Unajua UN bado inaheshimiwa huku kwetu kwa akina developing world! Ambako wanatusaidia matatizo ya chakula, polio, wakimbizi nk!!!! Its sad ila ndo ukweli. We kwa nini unafikiri Anan alikuwa characteristically quite kucriticize waafrika wenzake? anawajua sana...na asingerisk position yake huku "home" kwa kutetea msimamo wa akina Blair & co . Unajua hakuna kazi ngumu kama hizi. Inabidi uwe mnafiki! Kusurvive. Annan did it. Though at a price.
 
yaani Zimbabwe imekuwa kama imalaaniwa . Mzee wa Zimbabwe Mugabe anawaza kama CCM kwamba Tanzania ni mali yao tu .
 
Back
Top Bottom