Zilipendwa

Zilipendwa

mzanzibara-

Senior Member
Joined
Feb 3, 2014
Posts
179
Reaction score
60
Wale vijana wa zamani, naomba mnisaidie wimbo 1 ulipigwa na vijana jazz kama sikosei au juwata,

yani kulikuwa na dada 1 alikuwa anaringia sana wanaume na kujifanya hataki kuolewa na wanyonge, yeye anataka wenye magari kama mtumba, ila hatimae alikuja akaolewa na mshona viatu, unaitwaje huu wimbo na uliimbwa na bend ganii
nitashukuru kwa msaada wenu
 
unaitwa top queen of moroco road,i guess
 
hapa ulimwenguni kila binadamu kaumbwa na sifa zake eeee yaaa
lakini sifa za regina unaweza kukufuru muuungu ukasema kapendelewa kapendelewaaa
uzuri wa regina sio wa karne hiii,uzuri wa regina ni wa karne ijayo
tabia njema na busara zake mamamama zimefanya wazazi waheshimu maamuzi yake
msichana huyu ni mkazi wa jiji la dar es salaama ukitaka kumuona nenda moroco road
top queen of moroco road,top queen of moroco road

corus
tabu yenyewe ikabaki kwetu wavulana wenyewe kwa wenyewe tukabaki tunagombana tunashindanaa
wengine walifika nyumbaani kwa queen na mikwara mizitooo,wengine walifika nyumbani kwa kwa queen na mashati ya kuazima,na magari ya fahari na mapesa mengi haikuwezekana
mimi na mwenzangu tulikwenda kwa miguu yetu,tukamuone queen ,hakika ameleta utata hapa mtaani,wazazi wake wakamwacha achaguemchumba ampendaeee ohhhhh
amini usiamini kijana mmoja hoehae,darasa la pili mwenye hali duni,msukuma mkokoteni wa ilala
amini usiamini kijana mmoja mfuga bata daasa la pili mwenye hali duni msukuma mkokoteni wa ilala

malizia nimesahau nilikuwa mdogo
 
huyo ni hayati jery nashon au dudumizi ambaye badi bakule anacopy sauti yake
 
Sara wacha majivuno......Hee sara wacha majivuno husiwe kama Mwanaisha kanikataa kwa kuwa mimi ni mshona viatu eee
Kampata aaa mshikaji mwingine ehee heee heee mwenye gari kubwa sana mtumba kavunja uchumba Mwanaisha kwa kuwa mimi ni mshona viatu heee

chorus
Tamaa yako Mwanaisha ,itakuponza kwa kumfuata yule bwana mwenye mtumba

Mwanaisha mama ogapa sana mamaa kazi ni kazi mwanaisha bora mkono uende kinywani eeeeh......

URAFIKI JAZZ BAND
 
Yamekukuta nini...........?
wale vijana wa zamani, naomba mnisaidie wimbo 1 ulipigwa na vijana jazz kama sikosei au juwata,

yani kulikuwa na dada 1 alikuwa anaringia sana wanaume na kujifanya hataki kuolewa na wanyonge, yeye anataka wenye magari kama mtumba, ila hatimae alikuja akaolewa na mshona viatu, unaitwaje huu wimbo na uliimbwa na bend ganii
nitashukuru kwa msaada wenu
 
Sara wacha majivuno......Hee sara wacha majivuno husiwe kama Mwanaisha kanikataa kwa kuwa mimi ni mshona viatu eee
Kampata aaa mshikaji mwingine ehee heee heee mwenye gari kubwa sana mtumba kavunja uchumba Mwanaisha kwa kuwa mimi ni mshona viatu heee

chorus
Tamaa yako Mwanaisha ,itakuponza kwa kumfuata yule bwana mwenye mtumba

Mwanaisha mama ogapa sana mamaa kazi ni kazi mwanaisha bora mkono uende kinywani eeeeh......

URAFIKI JAZZ BAND

Duh. Na huu nitaupataje ?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom