ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

kuna wimbo nautafuta sikumbuki kama waliimba vijana Jazz au bendi gani, kibwagizo chake kilikuwa hivi "enyi wote wake zangu mapenzi yangu kwenu ni sawa mpendane ndio heshima ya ndoa ee"
 
Samahani mkuu kuna wimbo diamond sound, siufahamu jina ila kuna koras wanaimba

Morogoro morogo tulale wapi eeh kama unao naomba nisaidie, ninacho kipande nilirekodi redio nimejaribu kuattach imeshindikana

Mkuu ulishaupata huu wimbo? Nautafuta sana, kama umeupata naomba copy tafadhali.
 
Wakuu kwema humu? Huu uzi ndo nimeuona na ndo kwanza niko ukurasa wa tatu nataka kuoitia kurasa zote! Nimeona vema niwasalimu tu. Mimi mpenzi mkubwa wa muziki wetu wa zamani. Shukrani kwa wote mnaochangia na natoa rai tuuendeleze huu uzi. Kwa mwanzilishi wa uzi, my hat off for you! Unaujua muziki wetu vilivyo.
 
habar wakuu kuna nyimbo ya zamani zilipendwa inaimbwa '
"nakutafuta DAr es salam nzima nikuone mpenzii wanguuu sheri wangu mama nakuomba unisikiliizee, kosa gani nililolifanya kwako mpaka unikimbie mpenzi wangu"...
anayeikumbuka pls naomba anisaidie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tupo pamoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wimbo uitwao Huba hakika naupenda sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu kwema?
Ebana kuna wimbo wa Sikinde kiitikio chake wanasema “kwa kauli yangu ya ukiwa siwalaumu enyi wakwe”
Mwenye kuujua jina lake au mwenye nao please yamenikuta mkongwe mwenzenu nauomba tafadhali
 
Naomba msaada wimbo WA ,mwinjuma mumin wimbo sjui unaitwaje ila unaimba ivi (anameremeta (anameremeta )oo bibi harus anameremeta (anameremeta ) mambo yake si mchezooo ,anatisha kama ukoma ,
Watu wanasema mwinjuma tumemkubali kwa kazi yake anavyoifanya mwisho WA yote tunamzimiaaaa..
Aliye nae msaada please naomba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi Salim Chimbende akiendelea kuhakikisha muziki wa dansi uendelee kuwepo na pia kuwa balozi wa heshima /rapporteur wa muziki wa dansi Tanzania na kimataifa.
Wimbo: Maneno Maneno (watasema)

Source: Salim Chimbende
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…