Zikiwa zimesalia saa 38 wahamihaji 520 kati ya 36,000 ndo wamekubali kurudi ; kutii agizo la JK

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
Bukoba. Ngara. Zikiwa zimesalia saa 48 kabla ya kumalizika kwa muda uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa wahamiaji haramu kuondoka nchini au kuhalalisha ukaazi wao na wenye silaha kuzisalimisha, makundi ya wahamiaji hao, yameanza kuondoka kwa hiari.

Wastani wa wahamiaji haramu 150 wanaendelea kujiandikisha kuvuka mpaka katika Kituo cha Rusumo, Ngara mkoani Kagera kutekeleza agizo hilo.

Ofisa Uhamiaji wa Kituo cha Rusumo, Samweli Mahirane alisema mpaka sasa Wanyarwanda 520 wameshaondoka katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Ngara na kurejea makwao huku Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fabian Massawe akisema silaha 17 za aina mbalimbali zimesalimishwa.

Mahirane alisema wahamiaji hao wanatokea katika vijiji vya Wilaya za Ngara, Karagwe, Kyerwa, Biharamulo na Geita pamoja na Runzewe na wamekuwa wakiishi katika maeneo hayo bila vibali halali.

“Kuondoka kwa hiari kwa wahamiaji haramu, kutahitimishwa Jumatatu Agosti 12 na baada ya tarehe hiyo, vyombo vya dola vitaanza kufanya kazi kama agizo la Rais Kikwete lilivyoelekeza katika Mikoa ya Kagera na Kigoma,” alisema.

Aliwahakikishia wahamiaji hao usalama katika mataifa yao kwani hivi karibuni Serikali ya Rwanda ilikubali kuwapokea hata walio na mifugo kwa masharti kuwa ndani ya kipindi kifupi wataipunguza kwa kuiuza na kuboresha maisha yao.

“Rwanda wanahitaji mifugo michache, hivyo walio na mingi wanatakiwa kuipunguza kwa kuuza na kujenga makazi bora ikiwa ni pamoja na kuhifadhi ama kulinda mazingira ya nchi hiyo,” alisema Mahirane.


 
Safi sana acha waende kwao, naogopa sana kauli ya rais kikwete inaweza kutumika vibaya kama ile ya pinda kwa polisi sasa. Raia walio na asili ya rwanda hasa wenye mwonekano wa kitusi ama wale waliozaliwa na wazazi wawili(tanzania na rwanda) watanyanyaswa na konewa sana kama hakuana angalizo litakalo tolewa. Sheria izingatiwe.
 
Kazi bado ipo, kwa akwimu ni wahamiaji 36000 waliopo ni 520 tu ndio wameii amri. Ngoja tusubiri shuruti ambayo naamini watendaji wa vyombo vya dola watajinufaisha maana watakuwa na mikwara mingi sana.
Heri yao walioamua kutangulia kwa hiari.
 
Hivi na sisi na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, ilikuwaje tukawaacha hawa watu wakaanza wa 1, wa 2, wa 3 hadi wakafika 36,000 kuingia kwetu kienyeji kama wanaingiakwenye choo cha kilabuni? Au ndo tulikubali kuhongwa vgcent na kuwafumbia macho wahamiaji haramu? Nashauri likimalizika zoezi la kuwaswaga watu hawa tuwaadhibu wote waliowafumbia macho wahamiaji haramu.
 
Mtikila alisema kumbe nimeamini wakati mwingine huwa anaongea vitu vya maana.
 
to be frank, 36,000 immigrants ni tatizo. ikifikia mwaka 2050 watakuwa si chini ya 100,000 na wanaweza kuanzisha republic yao. kama vipi, tusiwafukuze lakini wasisettle kigoma na kagera, waje huku dsm, dodoma, arusha na maeneo mengine wachangamane na watz, ile kuwa mpakani na wako wengi namna hiyo inatia hofu kwamba kuna siku wanaweza kuwa wengi wakataka kaeneo kao kama vile wanavyotaka goma ya congo, na kwasababu watakuwa ni raia wetu sisi wenyewe kipindi hicho tunaweza kujikuta tumepata matatizo yale ya congo, given the fact that maeneo hayo ni maeneo ya madini kama ilivyo goma tu. Rwanda na Tz wakae chini kudisscuss about this matter, ili wafikie muafaka mzuri. Mungu ibariki Tanzania.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom