Michael Amon
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 8,775
- 3,610
Kuwa TV si kazi ngumu lakini kazi ni kuchagua TV iliyo bora kulingana na bajeti yako. Kwa kuliona hilo nimeamua kufanya utafiti na kuchagua TV zilizo bora kulingana mahitaji na kipato cha Watanzania kama nitakavyoanisha hapo chini:
Hii ni smart tv inayotumia teknolojia ya OLED ambayo inafanya TV hii iweze kuonyesha picha yenye ubora wa hali ya juu kuliko TV zote. TV nzuri sana na inaonyesha picha vizuri sana hata kwenye giza au hata kama mtazamaji akikaa kwenye kona ya TV.
Tatizo kubwa la hii TV ni bei, hivyo TV hii inaweza isiwafae watu wengi. Lakini kama uwezo wako wa kifedha unaruhusu basi nakushauri uichukue TV hii.
BEI: Bei ya TV hii inaanzia $1800 kwa 55 inch.
2. VIZIO P SERIES
Najua wengi mtakuwa hamuifahamu kampuni ya VIZIO kwa sababu wafanyabiashara wa Tanzania bado hawajagundua ubora wa hizi TV na kuamua kuanza kuziuza huku Tanzania. Ila kwa ufupi tu, VIZIO ni kampuni ya kutengeneza TV iliyopo marekani ambayo inatengeneza TV bora na kuziuza kwa bei nafuu ukilinganisha na kampuni nyingine kama Samsung, LG, Panasonic, Sony n.k. Kampuni hii imekuwa ikijishindia tuzo ya kutengeneza TV bora na za bei nafuu karibu kila tangu nilipoanza kuzifahamu. TV ya Vizio P Series ni TV nzuri sana na inaonyesha picha vizuri sana hata kwenye giza na hii ni kutokana na hii TV kutumia teknolojia ya full array local dimming backlight na Hidh Dyanamic Range na kubwa kuliko kuliko zote, ukinununu TV unapata na tablet ndogo ambayo utaitumia kama remote ya TV yako.
BEI: Bei ya TV hii inaanzia $999 kwa 50 inch.
3. Samsung KS8000
TV ya Samsung KS8000 ni TV nzuri sana na inaonyesha picha vizuri sana hasa kwenye sehemu zenye mwanga mkali, lakini TV hii si nzuri sana kwa kuangalia kwenye giza.
BEI: Bei ya TV hii inaanzia $1,297 kwa 49 inch.
4. Sony X810C
Sony X810C ni TV inayoonyesha vizuri sana ukilinganisha na bei yake. Ni TV inayoonyesha vizuri sana kwenye mwanga na kwenye giza pia.
BEI: Bei ya TV hii inaanzia $850 kwa 55 inch.
5. VIZIO D SERIES
Naam, kwa mara nyingine tena Kampuni ya Vizio imerudi kwenye list, na hii ni kutokana na ubora wa hizi TV na unafuu wake. TV hii inaonyesha picha nzuri na inauzwa kwa bei ambayo wewe mpenzi wa 4k TV unaweza kuimudu. Kwa ufupi tu naweza kusema TV hii ni the best katika ubora na bei.
BEI: Bei ya TV hii inaanzia $430 kwa 40 inch.
Baadae nikipata wasaa nitakuja kuandika TV bora za 1080p FHD.
TV Bora za 4k UHD
1. LG EF9500