Wale mnaomiliki TV za flat screen piteni hapa muokoe tv zenu

buzitata

JF-Expert Member
Apr 11, 2017
1,997
7,068
Habarini

Nitatumia lugha nyepesi Ili Kila mwenye uhitaji aweze kufaidika

Kumekuwepo na matatizo mengi yanayoripotiwa na wamiliki wa hizi TV za kisasa hasa kwenye upande wa kioo ama kutowaka kabisa.

Naomba niende kwenye chanzo kikuu.

Chanzo kikuu kinachoharibu hizi TV ni uwepo wa umeme usio na mpangilio, usishangae kuhusu mpangilio.

Tv ni kifaa kinachochakata taarifa iliyopokea na kwenda kuwa katika mfumo wa picha ama sauti Kwa kutumia umeme(Kwa lugha nyepesi tunaweza kuita demodulation)

Kwaiyo tunaona kwamba Ili tv Yako iweze kubadilisha hizo taarifa inazopokea ni lazima itahitaji umeme.

Vitu viwili ni maarufu kama volt na current (ampare) lakin Kwa ndani Zaid Kuna frequence pamoja na ohms na mwisho inaingia power factor kama mzigo. Hapa naomba tuondoke na hivyo viwili (volt na ampare)

Volt Kwa lugha nyepesi tunaweza kusema ni Ile nguvu inayosukuma umeme(unaweza kuwa 220, 230,240v na kuendelea). Current ama ampare ndio hasa inayochoma tv Yako ikisaidiwa sambamba na volt, hiyo ni kutokana na power inayohitajika.


Kifaa Cha umeme kinahitaji kuifikia power Fulani Ili kiweze kufanya kazi

Volt×ampare=power
V×A×cosQx√phase=power

Chukua hiyo ya mwanzo Ili tuende sambamba(v×A=power)
Kwa mfano
220v×10A=2200watt

Sasa ikitokea hiyo volt imepungua italazimika current iongezeke Ili kuifikia hyo power ya 2200w ama current ikipungua itahitajika volt iongezeke Ili kuifikia hyo watt ya 2200w
Kama una swali utauliza kwenye comment

Huu umeme wetu tunaoutumia huku majumbani kwetu haupo stable Kwa kuweza kumaintain uwiano wa volt pamoja na ampare

Kwaiyo unakuta Kuna kipindi unapanda juu sana na Kuna kipindi unashuka chini. Umeme ukiwa unashuka hapo mara nyingi kunakua hakuna madhara sana ila madhara ya nakuja pale ambapo umeme unalazimisha Kuja juu Ili kuweka uwiano wa volt pamoja na current

Pale ambapo umeme unakuja juu mara nyingi vifaa ama components ambazo zinafanya kazi kwenye tv Yako vinashindwa kustahimili ule umeme na kupelekea vifaa hivyo kufa(kuungua)

Ukiona nyumbani kwako unatumia umeme na taa kama zinafifia flani ivi mara zinawaka sana basi jua hapo umeme haupo sawa sawa hivyo inakupasa kuzima ama kuacha kutumia vifaa vyako vya umeme ambavyo ni rahisi kuungua kama TV na friji pamoja na baadhi ya radio.

Njia Bora kabisa ya kuweza kutatua tatizo Hilo la umeme kutokuwa katika uwiano mzuri ni vema ukanunua stabilizer ambayo inafanya kazi ya kusawazisha umeme na kutoa kile kiwango ambacho TV Yako inaweza kustahimili na kuendelea kufanya kazi, japo sio Kwa asilimia 100 ila at least inaweza kuokoa Kwa asilimia 75.


Kwann umeme haupo stable?
Kuna sababu nyingi sana ambazo zinafanya umeme usiwe imara na hasa mara nyingi ni sababu zinazochangiwa na vifaa vinavyotumika kuzalisha umeme(TANESCO)

Kama una swali unaweza kuuliza kwenye comment na wanajukwaa wengine wanaweza kusaidia kutoa michango yao

NUNUA STABILIZER ILI KULINDA TV YAKO
 
Nyongeza hushauliwi sana kutumia TV yako ikiwa katika Peak brightness/contrast, Joto linakua kubwa sana matokeo yake in long way cells za kioo zinaanza kufifia hatimaye kufa..

Ushaona kwenye tv kuna vichenga chenga vidogo dogo?? Eheee hapo ujue ni dead/damaged cells..
 
Na unaponunua stablizer, stablizer nzuri ni hizi zenye technology ya Servo, stablize za servo zina kitu kama mota ndani ,umeme ukipungua utasikia mota inazunguka kustablize umeme, teknolojia ya zamani zinatumia transforma, ukitaka kununua utakuta imeandikwa Servo au Svc
Kwa kampuni bora ni Andeli ikifuatiwa na tronics, japo tronics zake nyingi bado ni za transfoma
 
Mie nilijia tumetoka kwenye stabilizer tumeingia kwenye TV guard,mtoa mada tena anashauri turudi kwenye stabilizer?
Sawa mkuu ila hapo nimeelezea umeme wa nchi yetu, differential ya up and down ni kubwa tv guard ni nzuri kama gap likiwa dogo ila kama gap ni kubwa sana ni vema ukatumia stabilizer
 
Hii issue ya umeme kupanda na kushuka ni kweli, siku hizi umeme unazima zima Sana.

Nina stabiliser na tv yangu imekata ghafla tu hakuna picha ni audio tu sijajishuhulisha nayo lkn najiuliza ni umeme? Au ni yenyewe tu!
Vifaa vya umeme ni pasua kichwa sometimes

Sent from my M2101K6G using JamiiForums mobile app
Hizi TV za kariakoo siku hizi nahisi zina majina ya samsung na lg lakini ni sunshine.
Mimi nna tv flat nlizinunua post kwenye duka flan wanauza vifaa vya samsung tu mwaka 2014. Hakuna cha stabilizer wala nini na zote mpaka leo zinapga kazi. Tena mona inawaka saa 12 na kuzimwa saa 5 usku unless umeme umekatika.
Sasa kuna LG ya kariakoo baada ya mika miwili ikabuma tu bila sababu
 
Hizi TV za kariakoo siku hizi nahisi zina majina ya samsung na lg lakini ni sunshine.
Mimi nna tv flat nlizinunua post kwenye duka flan wanauza vifaa vya samsung tu mwaka 2014. Hakuna cha stabilizer wala nini na zote mpaka leo zinapga kazi. Tena mona inawaka saa 12 na kuzimwa saa 5 usku unless umeme umekatika.
Sasa kuna LG ya kariakoo baada ya mika miwili ikabuma tu bila sababu
Tv yangu ya lg niliyopewa zawadi kibaruani mwaka 2011 bado ipo mzigoni hadi leo, heshima kwa lg
 
Back
Top Bottom