Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
HATUWEZI kuzungumzia maendeleo ya sekta ya mafuta na gesi nchini Tanzania bila kwanza kuzifahamu kampuni zilizowekeza humo. Hawa ndio wadau muhimu Zaidi kwa sababu, kama tulivyoona, hata ugunduzi wa awali usingeweza kufanyika na kufanikiwa bila wao kwa sababu kama inavyoeleweka, Tanzania haikuwa na bado haijapata wataalamu na mitaji ya kutosha kuwekeza katika tafiti, uchimbaji na uchakataji wa gesi.
Tangu mwaka 1952 utafiti ulipoanza kufanyika, kumekuwepo na kampuni nyingi za kigeni ambazo zilipewa mikataba ya kufanya tafiti na sasa nyingine tayari zimekwishapewa mikataba ya uchimbaji pamoja na kutengeneza miundombinu inayotakiwa katika sekta hiyo, hasa gesi ambayo tayari inaendelea kuzalishwa.
Kwa habari zaidi, soma hapa => Zijue kampuni zilizowekeza katika mafuta na gesi Tanzania – AFREN | Fikra Pevu