Zijue breed za mbwa 20 hatari zaidi duniani

Zijue breed za mbwa 20 hatari zaidi duniani

Hizi types nyingine kama Rottweiler zimesababisha vifo vya watu USA ndie ije kuwa uku kwetu Bonge utapata majanga
Naona jibu langu linazungushwa sana, kwa maana hiyo ni kitu kisichowezekana kabisa kwa hizi jamii tofauti za mbwa kufugwa sehemu moja?
 
Ndio lakini wakishakuwa wakubwa ndo challenge inaanza
Napenda sana lile dubwasha la kijeremani shephadi, kwanza umbo lake tu limekaa kibabe ile mbaya, muungurumo wa sauti yake umejaa mitetemo ya kutisha inayoashiria kuwa na ukatili mkubwa ndani yake
 
Naona jibu langu linazungushwa sana, kwa maana hiyo ni kitu kisichowezekana kabisa kwa hizi jamii tofauti za mbwa kufugwa sehemu moja?
Ni ngumu kwa sababu hizi.
1. Kila breed ina tabia tofauti sana na mwenzake. Mfano: Rottweiler ana tabia tofauti na Dull Dog au German Shepherd, sasa wakiwa wadogo au Puppies unaweza kuwafuga pamoja lakini wakishakuwa wakubwa ndo tabia hujionesha labda kama unataka kuandaa uwanja na mashindano ya mapigano ya mbwa.
2. Mazingira yana athari kubwa sana kwa mbwa. Kwa marekani wanakupa mpaka ushauri Wa namna ya kuwatunza na wanakutembelea mpaka home kuangalia mazingira sasa. Chukua umewafuga wote eneo moja baadaye wataanza kutambiana nani bingwa pia kuna ishu ya competition ya himaya.
 
Huyu ndo Rottweiler:View attachment 1182434 Ana sifa ya kutokutii maagizo akishakuwa mkubwa tu.
View attachment 1182435 Wolf Hybrid ambao wanapatikana sana kwenye nchi ya Czechoslovakia.
View attachment 1182436 American Bull Dog.
View attachment 1182438 huyu ndo Gull Dong.
View attachment 1182439 huyu ndo Boer Boel.
View attachment 1182440 Dogo Argentino.
View attachment 1182441 Bull Terrier.
View attachment 1182442 Cane Corso.
View attachment 1182443 American Bandogge.
View attachment 1182444 Inu breed ya Japan anaitwa Shiba Inu

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilikua nina mbwa wawili mmoja nilimpa jina la Simba huyu alikua mweusi tii mwingine nilimuita jina la Hodi mwekunduuu.

Simba alikua ananichungia mbuzi anaenda nazo na kuzirudisha maskani wakati mwingine anakuja kapakata sungura mdomoni.

Huyu Hodi yeye alikua mlinzi wa boma tu maskani hakuna geti ila hukatizi hovyo hovyo, dume hili lilipenda majike ya rangi rangi ama meupe tu.

Usiniulize walikua breed gani manake majina yenu haya ya kizungu yanatuchanganya. Walikua wana dozi ya mbegu za mmea mkuu na maziwa kila baada ya mwezi ili kuwakuza vema. Hali hovyo hovyo alikua.

RIP simba na hodi.
 
Mie ni mpenzi mkubwa sana wa kufuga mbwa katika Maisha yangu nimekuwa na mbwa mbalimbali lakini haswa ni German Shepherd ingawa pia nilikuwa na mbwa mmoja niliuziwa na jamaa yangu sikuwa hata najua ni breed gani huyo mbwa alikuwa mkubwa sana rangi nyeupe na nyeusi na alikuwa ana uzito mkubwa mrefu na mkia una manyoya mpk tulikuwa tunayapunguza.

Kuna tatizo moja kubwa sana kwenye nchi zetu za tropiki hawa mbwa breed za nje uwa wanashindwa kuvumilia mazingira. Mfano mie nilikuwa na Germany Shepherd wakubwa wa 4 wote wamekufa mwezi wa nne 2019 kuna ugonjwa uliingia walikuwa hawal.i na wanaharisha kinyesi cheusi. Nilikuwa nawachanja chanjo zote ila walikufa wote. Niliumia sana

Sasa baada ya hao mbwa kufa kuna siku nilikuwa natoka Moro nikakuta madogo maeneo ya Ruvu wanatembea na mbwa ila ana masikio kama Germany Shepherd basi nikasimama na kuwaomba waniuzie wakakubali

Nilipofika nae Dar huyo mbwa alikuwa na mambo ya ajabu sana yaani alikuwa hatoki bandani anaogopa mpk tunaomfuga. Kuna siku nikambeba naikaenda kumtupa kama km 5 from home. Tumekaa baada ya wiki tukamkuta getini kakonda kama kijiti. Tukampokea tukamwita daktarin akamtibu.
To cut story short huyo mbwa baada ya kurudi nadhani akili ikamkaa sawa yaani alikuwa mkali sijapata kufuga mbwa akafikia level hiyo ya ukali. Ameshaua paka wawili na ana sauti akibweka mpk nadhani vibaka wameshaiwekea X nyumba yangu na anakuwa haraka na ana umbo la ajabu na pia hajawahi kuumwa nimempa jina la MAWAZO kutokana na tabia zake alipokuwa mdogo
Isije ikawa wale mbwa breed ya nguchiro
 
Napenda sana lile dubwasha la kijeremani shephadi, kwanza umbo lake tu limekaa kibabe ile mbaya, muungurumo wa sauti yake umejaa mitetemo ya kutisha inayoashiria kuwa na ukatili mkubwa ndani yake
Mkuu una uhakika unawajua hawa mbwa? Naona unavowaelezea ni total different.
 
Mtoa mada umenisikitisha sana baada ya kuona hujamweka mbwa bora wa ulinzi na msharp kuliko wote BELGIAN MALINOIS a.k.a BELGIAN SHEPHERD
 
Nilikua na GS kama huyu,nilimnunua akiwa mdogo kabisa nkaamuuza akiwa na miaka miwili na kuhamia kwa Belgian Malinois(Belgian shepherd)
Faida au uzuri wa GS niliouona:
1.Ni mbwa alert sana kwa kitu chochote akiwapo lindoni au mazingira yanayomzunguka.
2.Ni mbwa anaenusa sana.
3.Kichwa chepesi.
4.Rangi nzuri,mvuto.
Mapungufu yake:
1.wavivu wa mazoezi,mpaka umforce
2.anazoea kila mtu hovyohovyo tu,mpaka umfundishe.
3.dhaifu kwenye mambo ya misosi wanapenda kulakula zaidi.

Nilipokua nae nkitoka nae kukimbia na kwenye mazoez,watu wakimwona wanamsifia mno uzuri wake,mwonekano wake...hadi wakina mama utawaskia "mbwa wako mzuri jamani"...ntamshawishi na mr anunue kama huyu"
Washkaji ilikua mwanangu fanya mpango wa mbegu au niuzie nk.
Kwenye tizi,km chache tu ulimi tai[emoji3]!!!
Ni mbwa ambae nilipokea ofa kedekede.

Tangu nihamie kwa BS mambo tofauti sana,mtaani utasikia "dah jibwa linaogopesha" na hakuna ofa niliyopokea [emoji3][emoji3].
Belgian malnois ni mzuri zaidi kwakua hahitaji sana mafunzo,akimwona mtu yoyote mgeni kwa mazingira ya lindo lake anamharrass iwe mchana au usiku,iwe mwenyeji nipo nae au sipo nae...mpaka nimkataze.
Kwenye mazoezi ndo usipime utachoka wewe,ni wepesi mno sababu ya maumbo yao...kuruka ndo usiulize kama ukuta nk tena hata bila ya mafunzo meengi.
Kunusa au kutrack kitu ndo mwenyewe...nadhani mnaona hata polisi wenyew wanawatumia zaidi kwenye viwanja vya ndege.

Ni hayo tu.
 
Mtoa mada umenisikitisha sana baada ya kuona hujamweka mbwa bora wa ulinzi na msharp kuliko wote BELGIAN MALINOIS a.k.a BELGIAN SHEPHERD
Nisamehe sana mkuu nilikuwa na listi kubwa sana wa Hawa Jamaa ila ni kweli BS ni Noma lakini niliwahi kupata taarifa kuwa kwa baadhi ya kaya za uswahili huyu anakuwa Assassin maana Mwizi akiingia night bac unaweza kukuta maiti kabsa.
Big up sana Mkuu
 
Sijajua but ngoja niwaulize wad
hivi kwann huwa wanawakata mikia fc?

Niliwawahi kumuuliza Mfanyabiashara na Mfugaji Nguli wa Mbwa
(Sio Mbwa Koko)
Jibu alilotoa yeye ni kuwa akitolewa Mkia ndio anavutia zaidi kuliko akiwa nao na kawaida ka-Mkia kenyewe kwa aina ya wale ambao mara nyingi hutolewa ni kembamba flani tu.
Ukichunguza si Mbwa aina yoyote anakatwa.

Binafsi nimemuelewa vinginevyo labda aje mdau mwenye sababu zaidi ya niliyopewa Mimi maana Dunia Pana Hii.
 
Uzi mzuri lkn kwa ukosefu wa mapichapicha unakosa mashiko kiboyaboya kabisa.
 
Back
Top Bottom