Zijue breed za mbwa 20 hatari zaidi duniani

Zijue breed za mbwa 20 hatari zaidi duniani

Habarini za Alhamis natumaini mpo salama sana. Naomba kuleta Uzi huu maalumu kuhusu tunaopenda kufuga mbwa. Duniani kuna aina nyingi sana za breed ya mbwa achilia mbali German Sheepshead na Bull Dog au Chihuahua. Kuna breed hatari sana zaidi ambazo zinaweza kuleta shida kwa mfugaji wake.

Hapa ninaweka breed 20 ambazo lazima ukae chonjo ukiwa nazo.

10. Inu.
Huyu ni mbwa ama breed ya mbwa yenye uzito kuanzia kilogramu 58 mpaka kilogramu 90. Na ana urefu unaoanzia inch 24 mpaka 32.

Kiuhalisia huyu ni mbwa Wa mapambano na baadhi ya nchi wamekata kufuga mbwa Hawa kabsa.

Mfano mzuri sana ni Inu aina ya Shiba anayepatikana katika nchi ya Japani, ambaye huyu hutumika kwenye kuwinda. Pamoja na aina nyingine Tosa Inu.

9. American Bandogge.
Huyu ni cross breed ya American Pit bull Terrier pamoja na Neapolitan Mastiff. Sasa huyu Pit bull Terrier ni mkorofi balaa unakwenda kuchanganya na kiburi cha Neapolitan Mastiff. Hapo unakwenda kutengeneza mbwa mmoja mkatili sana.

Ni mbwa aliyejaa misuli sana, ijapokuwa alipofanyiwa breed hakukuwa na malengo ya kuwa mbwa Wa kupigana lakini matokeo yake yakawa ndo hivyo.

8. Cane Corso.
Mbwa kwenye uzito kuanzia kilogramu 44 mpaka 68. Kuanzia sura mbaya mpaka tabia yake hakika ni mbwa mwenye ukali Wa kipekee.

Akiwa ni breed ya Mbwa aina ya Canis Pugnax ambao Hawa ni mbwa waliotumika na Warumi kwenye Vita. Hivyo damu inatembea ndani ya Cane Corso.

7. Bull Terrier.
Mbwa hawa wana kichwa kikubwa lakini wanaongoza kwa kuwa na misuli mikubwa na imara sana. Ana uwezo Wa kuwinda kwa ukali na ukatili sana hasa hasa kwa wanyama wadogo.

6. Dogo Argentino.
Huyu ni mbwa mrefu,mkubwa na aliyejaa misuli sana, chimbuko lake ni Argentina kwa lengo la kusaidia kuwinda.

Na inasemekana alifanyiwa breed ili kuweza kupambana na wanyama kama Puma pamoja na Dubu mwitu.

5. Boer Boel.
Mbwa mkubwa sana na ni breed ya Mastiff kutoka kwenye South Africa. Alifanyiwa breed kwa lengo la kulinda mashamba au nyumbani.

Mwanzoni walitumika kama mstari Wa mbele kupambana na mbwa mwitu. Pia hata kwenye mawindo ya mwituni mfano nyati au swala walikuwa na uwezo Wa kufuatilia mnyama na kumchukua mpaka kwa mwenye naye. Ni mbwa wenye uaminifu sana nyumbani pia kulinda familia zao.

4. Gull Dong.
Anajulikana sana kama (Pakistan Bull Dog) akiwa ni cross breed ya Gull Tarrier pamoja na Bully Kutta. Ana nguvu sana na alifanyiwa breed kama mbwa mpiganaji. Ni ngumu sana kumtunza na ana hasira za karibu.

3. American Bull Dog.
Huyu ni mbwa mwenye misuli mingi kuzidi mbwa wote. Ukisikia inafika sehemu mtu anampiga shaba mbwa wake basi jua kuwa American Bull Dog ni moja wapo.

Kwani wana tabia ya kuwa wagumu kusikia na kufuata maagizo. Alifanyiwa breed kwa lengo la kupambana na dubu mwitu, pamoja na kulinda mifugo ikiwemo na mali.

2. Wolf Hybrid.
Kama jina linavyosema hapo, huyu ni mbwa mwenye breed ya mbwa pamoja na Mbwa mwitu. Huyu alifanyiwa breed na kupelekea kuwa na tabia zinazoshabiana na Mbwa mwitu.

Hana tabia inayoeleweka kwani anaweza kuwa kama mbwa lakini baadaye anakuwa kama mbwa mwitu tena.

1. Rottweiler.
Huyu naomba nimuweke namba moja maana ni mbwa mwenye kiburi balaa kwank ni breed ya American Bull Dog pamoja na Mbwa mwitu. Na anaanza kubadilika tabia akiwa na miaka 3 tu.

Bonus:
1. German Shepherd.
Huyu nimemweka bonus. Ni mbwa mwenye akili sana, anajiamini sana, sio muoga na anapendwa kutumiwa na Polisi kwenye kutuliza ghasifa. Lakini cha ajabau ni kuwa jike hawezi kuvumilia ukicheza na Watoto wake kwani anaweza kukushambulia mpaka kifo.

2. Pitbull.
Hili ni jina linalotumika kuelezea breeds za mbwa kama vile: American Pit bull Terrier, the Staffordshire bull Terrier, the American Staffordshire Terrier and the American Bull Dog.

Huyu ni mbwa mahususi kuwinda na kuzuia dubu pamoja na Ngombe mwitu. Pia Pitbull walitumika kupiganisha mbwa na ni kati ya mbwa wenye hatari kubwa duniani.

3. Causanian Ovcharka.
Anajulikana kama Caucasian Shepherd na lengo kubwa ilikuwa ni kutengeneza breed ya mbwa atakayelinda mifugo. Lakini mbwa huyu ni mkali na hatari hasa kwa watu asiowatambua kabsa.

Ninajaribu kufanya attachment ya picha nikiweza nitaweka....
Asanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
DOG BREEDS.jpg
DOG BREEDS.jpg
DOG2.jpg
DOG2.jpg
 
Msamehe tu mtoa mada, ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Certificate of Vetinary Services

Nilikwisha kusema kuwa kulikuwa na Tatizo wakati wa kupakia picha!! Ila Naomba niombe radhi tena... Samahani [emoji120]
 
Thnx
Huyu ndo Rottweiler:View attachment 1182434 Ana sifa ya kutokutii maagizo akishakuwa mkubwa tu.
View attachment 1182435 Wolf Hybrid ambao wanapatikana sana kwenye nchi ya Czechoslovakia.
View attachment 1182436 American Bull Dog.
View attachment 1182438 huyu ndo Gull Dong.
View attachment 1182439 huyu ndo Boer Boel.
View attachment 1182440 Dogo Argentino.
View attachment 1182441 Bull Terrier.
View attachment 1182442 Cane Corso.
View attachment 1182443 American Bandogge.
View attachment 1182444 Inu breed ya Japan anaitwa Shiba Inu

Sent using Jamii Forums mobile app
Thnx
 
Huyu ndo Rottweiler:View attachment 1182434 Ana sifa ya kutokutii maagizo akishakuwa mkubwa tu.
View attachment 1182435 Wolf Hybrid ambao wanapatikana sana kwenye nchi ya Czechoslovakia.
View attachment 1182436 American Bull Dog.
View attachment 1182438 huyu ndo Gull Dong.
View attachment 1182439 huyu ndo Boer Boel.
View attachment 1182440 Dogo Argentino.
View attachment 1182441 Bull Terrier.
View attachment 1182442 Cane Corso.
View attachment 1182443 American Bandogge.
View attachment 1182444 Inu breed ya Japan anaitwa Shiba Inu

Sent using Jamii Forums mobile app

Pitia hapa kuna picha zote mkuu @Jorojik
 
Pitia hapa kuna picha zote mkuu @Jorojik
Hivi mfano hawa mbwa wote kumuuwa Simba (Full grown) inabidi wawe wangapi ??

Je hizi aina zote ni brake fast ya haraka kwa chatu au si rahisi kuuliwa??

Mimi nina kilo 52 naweza Survive kwa hawa mbwa endapo nitapambana nao for any confidence labda paap kanivamia??
 
Back
Top Bottom