Zijue aina kuu 2 za misukule

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,901
6,661
Kuna msukule wa nje na msukule wa ndani.

Msukule wa nje ni yule mtu ambae wachawi humfata usiku na kuchukua kivuli, kucha, nywele na mate alafu wanaenda kumfunga nyota na ridhiki na kufukia katika makaburi.

Huyo atakuwa msukule wa nje hatothaminika na wala hatofanikiwa kwa chochote atakachokifanya.

Msukule wa ndani ni yule ambae wachawi huja usiku na kuweka nafsi yao na kufunga nafsi ya mhusika katika mwili kisha kuondoka.

Ile nafsi itampelekampeleka mhusika na kupelekea kifo (kiinimacho) alafu nafsi itatoka na mwili kwenda mafichoni.

Utabebwa mgomba (maiti) mpaka nyumbani, kile chumba ambacho itakaa maiti ndio chumba ambacho mtu huyo atakaa nyuma ya mlango siku zote za msiba na mkienda kuzika ndo mwili utatolewa kwenda mafichoni.

Mwili huu hautoharibiwa mpaka zifike siku 30 na nafsi ya marehemu itakuwa inahaha kwa ndugu jamaa na marafiki kutafuta msaada ndo hapo unapokuwa unamuota marehemu kila siku.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom