Zifahamu kampuni bora za simu Duniani kwa 2020

Zifahamu kampuni bora za simu Duniani kwa 2020

Huawei..'waanzilishi wa technology ya 5G'
Lenovo..'kampuni ya china'...
Anyway..sawa
 
Simu bora duniani means zilizoko soko la dunia na TECNO MOBILE imeweka kipaumbele africa na wakizungumzia ubora wanaangaliwa vitu vingi ikiwa ni pamoja na uwezo wa simu kutenganishwa kama ushawahi kuona s20 ikiwa imefunguliwa yn kila kifaa kinaweza kutenganishwa ,tofauti na hzo sm za tecno na infnx unaweza kutenganisha spika,mic,vibration, betr,screen na motherboard, ila izo simu nyingine zinazoitwa bora mpka ile motherboard inafaa kutenganisha ....

Ila tecno wame base sana africa ukichek matoleo ya povour wamebase kwenye betri, matoleo ya spark na camon wamebase camera na hizo wanazosemaga unasubiri keyboad ije mara nyingi na wale ambao hawana uelewa mkubwa kivile kwenye masuala haya ya tech unakuta mtu ana simu ya ram ya 512 au 1GB na sometimes 2GB ila app alizoziacha background (hajazifunga) ni nyingi na zina consume ram kubwa., af tena unakuta simu inazaidi ya 1yr-2yrs tokea ainunue....
 
Nina Sony kali najivunia yaan mtaa mzima ninayo peke yangu, haijawahi kuniletea shida ni mwaka wa 4 huu sasa ninayo japo siendi na wakati lakin Sony is the best. Battery life is good, Camera quality, sound quality.. Haina scratches ipo soft kama nilivyoinunua. Sony is the best

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1: SAMSUNG • Ni kampuni ya vifaa umeme iliyopo Korea Kusini. Wana shika nafasi ya 1 kutokana na ubora wa simu zao kama; Galaxy S20, Galaxy S11, Note 10 n.k.

2: HUAWEI • Hii ni kampuni kutoka China waanzilishi wa teknolojia ya 5G. Wana matoleo MaTaTa ya simu kama; Huawei P30 Pro, Mate X, Mate 20 Pro n.k. Pato lao ni $ 121.71 kwa mwaka

3: APPLE iPHONE • Hii ni kampuni kutoka Marekani ambayo ina mfumo wake wa kipekee wa kuendesha simu zao iOS. Wana simu kama; iPhone 11 Pro, iPhone X, iPhone XR n.k. Pato lao ni $33.3 kwa robo ya mwaka.

4: XIAOMI (MI) • Hii ni kampuni nyingine kutoka China. MI inasimama badala ya Mobile Internet, wamewekeza kwenye simu, Tv, Viatu n.k. Wana simu kama; Xiaomi Mi9, Xiaomi 8 Pro, Mi Mix 3 n.k. Pato ni $ 494 kwa theluthi ya mwaka.

5: OPPO • Hii ni kampuni nyingine kutoka China ilianzishwa mwaka 2016. Ipo pamoja na Vivo, One plus na Realme. Wana simu kama; Oppo A31, F15, A5, A9 n.k.

6: VIVO • Hii ni kampuni nyingine kutoka China ilianzishwa mwaka 2011. 2015 ikaingia kwenye 10 bora kwa Mara ya kwanza. Wana simu kama; Vivo ZIX, V17 Pro, S1 Pro, V 51 n.k. Umesambaza zaidi ya simu million 103.

7: MOTOROLA • Ilianzishwa mwaka 1928 pale Marekani. Mwaka 2007- 2009 iliyumba kiuchumi, 2011 ikaja kivingine. Wana simu kama; RAZR, Mate X, Motorola 24 n.k.

8: LENOVO • Kampuni nyingine ya China inatengeneza simu, komputa na vifaa vingine vya umeme. Pia kwenye simu hawapo nyuma japo walinakili aidia ya iPhone. Wametengeneza kama; Lenovvo Z2 plus, P2, K6 power n.k.

9: LG • Kampuni nyingine ya pili kutoka Korea kusini, LG inasimama kama Life Good's. Wana simu kama LG W10 Alpha, K415 n.k

10: NOKIA • Kampuni ya Nokia inatufungia kumi bora yetu. Ni kampuni kutoka Finland wana simu kama Nokia 2.3, Nokia 110, Nokia 2.2 n.k.

Sent using Jamii Forums mobile app

mimi ni mfuatiliaji sana wa simu. Lakini simu inayoitwa samsung galaxy s11 sijawahi kuisikia.

I stand to be corrected.
 
Back
Top Bottom