Ziara za Kinana zazua Ufisadi Mkubwa

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,490
2,000
WIMBI la matumizi mabaya ya fedha za umma limezidi kukiandama Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo hivi sasa kinatuhumiwa kutumia fedha za umma katika ziara na ukaguzi wa miradi.

Tanzania Daima imedokezwa kuwa kila ziara ya CCM inakofanyika, mkurugenzi wa halmashauri husika hutoa magari au fedha za kuwakirimu wahusika.

Imedokezwa kuwa miongoni mwa ziara ambazo zinatumia fedha za halmashauri ni inayofanywa hivi sasa mikoani na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Inaelezwa kuwa ziara hizo hazipaswi kugharimiwa na fedha za serikali kupitia halmashauri mbalimbali kwakuwa zinatokana na wananchi wenye itikadi tofauti pamoja na wasio na itikadi.

Michango hiyo ndiyo inadaiwa kuwapa nguvu vigogo wa CCM na kuacha kupitisha bakuli kuomba misaada kwa makada wake kama ilivyozoeleka siku za nyuma.

Tanzania Daima limedokezwa kuwa vyama vya upinzani na CCM vimekuwa na utaratibu wa kuomba misaada kwa makada wao au wahisani, wafadhili wa ndani na nje ya nchi.

Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni utaratibu huo unaonekana kutumiwa zaidi na wapinzani kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuwaamrisha au kuwashawishi wakurugenzi wa halmashauri kugharimia ziara zao.

Tanzania Daima liliwasiliana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ambaye alisema kuwa taarifa hizo zinalenga kukichafulia jina chama tawala.

“Madai hayo ni ya kiupuuzi na kwamba misafara yetu inawaumiza viongozi wa CHADEMA, sisi tunapoamua jambo tunakuwa na mipango sambamba na kujitosheleza,” alisema.

Hata hivyo, Tanzania Daima limepata taarifa kuwa baadhi ya halmashauri ambazo Kinana na timu yake wameshapita ziligharamia malazi, chakula na usafiri wa ndani ikiwemo magari ya serikali kutumika.

Halmashauri ambazo taarifa zake zimekusanywa na gazeti hili ni pamoja na Nzega, Igunga na Uyui zilizopo mkoani Tabora na Iramba iliyopo mkoani Singida huku wakurugenzi wake wakikiri kutumia magari ya serikali na baadhi ya watumishi kuhudhuria katika ziara hiyo.

Katika Wilaya ya Igunga, msafara wa Kinana ulikaa kwa muda wa siku tatu ambapo halmashauri kupitia viongozi wa CCM wa wilaya hiyo waligharimia usafiri wa ndani, chakula na malazi pamoja na kukodisha pikipiki 50.

Pikipiki hizo zilitumika kumpokea Kinana na magari 10 yaliyotumika kuwabeba wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo waliotakiwa kuhudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Igunga.

Mbali na gharama hizo, pia ziara hiyo inaelezwa kusimamisha kazi mbalimbali za kiutendaji katika maeneo wanayopita kutokana na watendaji wa serikali kutakiwa kuwa sehemu ya ziara hiyo.

Chanzo kutoka ndani ya Halmashauri ya Igunga, kilieleza kuwa mbali na gharama ya malazi, vyakula, usafiri na malazi, pia hakukuwa na malipo iliyolipwa na chama hicho kwa kutumia ukumbi wa halmashauri kufanya mikutano yake ya ndani.

Chanzo hicho kilieleza kuwa msafara wa Kinana ulikuwa na magari zaidi ya 28 na kila gari likiwekewa lita 80 za mafuta kutembelea maeneo mbalimbali.

Kigogo mmoja wa CCM, alidokeza kuwa walitakiwa kuandaa chakula cha watu 200 huku sahani moja ya chakula ikiuzwa kwa shilingi 5,500.

Alisema walikodisha pikipiki 42 kwa sharti la kila mwenye pikipiki aliyehudhuria mapokezi ya Kinana, atalipwa sh 7,000 na kuwekewa lita mbili ya mafuta.

Alibainisha pia walitakiwa wahakikishe msafara wa Katibu Mkuu unapatiwa malazi.

“Sisi chama tulibeba jukumu lile kwa kuwa ni ugeni wa chama, lakini hakuna hata senti moja tuliyotumia kutoka mfuko wa chama zaidi ya fedha hizo kutoka ndani ya halmashauri yetu,” alieleza mtoa habari wetu kutoka Igunga.

Katika Wilaya ya Nzega, Uyui na Iramba, msafara wa Kinana ulipatiwa mafuta ya magari na chakula kwa fedha zilizotoka katika halmashauri na kukabidhiwa viongozi wa CCM wa wilaya, huku suala la malazi likiachwa kuwa jukumu la waliokuwa katika msafara.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, wakurugenzi wa wilaya zilizofanyiwa uchunguzi walikanusha kugharamia ziara hizo, lakini wakikiri kutoa magari yaliyozunguka katika miradi iliyokuwa ikikaguliwa na Kinana.

Mkurugenzi wa Wilaya ya Igunga, Rusika Turuka, alipoulizwa juu ya halmashauri yake kugharamia ziara ya Kinana, alitaka apewe muda kwa maelezo kuwa yupo katika mkutano na hata alipopigiwa tena simu hakupokea.

Mkurugenzi wa Wilaya ya Nzega, Abraham Mndeme, alikiri ofisi yake kutoa magari yaliyowabeba watumishi wa serikali na madiwani wa CCM kuongozana na Kinana katika ziara hiyo wilayani mwake.

Mndeme, alisema ugeni uliofika katika wilaya yake ni wa kitaifa, na kwamba miradi iliyohitaji kukaguliwa ni ile iliyosimamiwa na halmashauri ya wilaya.

“Walioambatana na msafara wa Kinana ni madiwani na sisi tulitoa magari ya kuwasafirisha kwenda kwenye miradi na kwa watendaji mimi nilitumia gari moja na mhandisi wa manispaa,” alisema Mndeme.

Mkurugenzi wa Wilaya ya Uyui, Hadija Mkauani, alipoulizwa juu ya kugharamia ziara ya Kinana, alimuomba mwandishi akutane nae ofisini na alipoambiwa simu inapigwa kutoka Dar es Salaam alikata simu.

“Baba naomba tuonane ofisini tuweze kuongea vizuri hayo mambo au umtume mwakilishi wako hapa mkoani si mnaye huku, tutaongea vizuri tu,” alisema Mkauani.

Kaimu Mkurugenzi wa Iramba, Mariam Mpita, alisema gharama za ziara hiyo zilibebwa na CCM huku yeye, watendaji wa halmashauri hiyo waliambatana na Kinana kukagua miradi ya maendeleo.

Nape afafanua

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, badala ya kujibu hoja ya ziara zao kutumia fedha za umma aliilaumu CHADEMA.

Alisema ziara zao zinawaumiza CHADEMA waliokuwa wakifanya ziara za aina hiyo ili kujiimarisha, lakini sasa wanaona zinafanywa na CCM wanahofia kuanguka mwaka 2015.

“Hata mtoto wa darasa la kwanza akisikia hayo madai atajua ni upuuzi, lakini ulizeni halmashauri iliyochangia hata shilingi moja. Najua ziara hizi zinawaumiza sana CHADEMA,” alisema.

Alipoulizwa kama ziara yao ina lengo la kuwaumiza CHADEMA au kuangalia changamoto zinazowakabili wananchi, na CCM itakavyoishauri serikali kutatua yatakayobainika, Nape alisema swali aliloulizwa ni fikra za kijinga za CHADEMA.

Nape alisema CHADEMA hawana ujanja wa kukwepa kifo chao, huku akisema uzushi na uongo hautawasaidia kupona.

Wakati Nape akikana halmashauri hizo kugharamia ziara za chama hicho, wiki iliyopita katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Jiji la Arusha, Mkurugenzi wa jiji hilo, Juma Idd, alikiri kufanya hivyo.

Idd, alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu maswali ya madiwani wa jiji hilo waliohoji sababu za ziara za madiwani au viongozi wa CCM kutumia magari ya halmashauri.

Idd, alisema walitoa magari hayo ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya serikali iliyotaka viongozi wa CCM kupita kukagua utekelezaji wa ilani yao.

Alisema kuwa jiji walitoa wataalamu na gari kwa ajili ya kwenda kutoa ufafanuzi juu ya miradi hiyo.

Source:Tanzania Daima.
 
Ben Saanane

Verified Member
Jan 18, 2007
14,595
2,000
Chama cha Mapinduzi kimeingia katika kashfa kubwa ya Ufisadi kufuatia ziara za Katibu Mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana.

Taarifa za Uhakika kutoka katika wilaya ambazo Kinana amefanya ziara ikiwemo Igunga,Nzega na Uyui zinasema Halmashauri zimegharamia Chakula,Malazi na mapokezi ya misafara ya Katibu Mkuu huyo ikiwemi kukodi pikipiki za kumpokea na magari ya kusomba watu kuwapeleka sehemu za mikutano.

Ufisadi huo wa kuchota fedha za umma kugharamia ziara za Kinana umepachikwa jina la Kugharamia ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Akihojiwa kuhusu ufisadi huo Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye aling'aka na kusema Chadema wanaionea wivu CCM kuhusu ziara zake.

Source:Tanzania Daima.

Huu ni ufisadi period.Ni sheria gani au ni bajeti gani ya Halmashauri inayoruhusu matumizi ya fedha za Halmashauri katika shughuli za kisiasa kwa vya na viongozi wake?

Hapa ni lazima watu wawajibike ili kukomesha kabisa upuuzi huu

CCM wanapokea ruzuku Milioni 800 kila Mwezi.Huu ni mkakati wa ku-save fedha zao kwa ajili ya uchaguzi baada ya kuona wamebanwa kila mahali na upinzani kuzuia yale ya EPA 2005 . Sasa wamebuni mbinu mpya ya aibu na fedheha katika demokrasia yetu na pia kufuru kwa Umma wa watanzania.Haikubaliki hata kidogo na inahitaji hatua za kibunge na nje ya bunge .Haiwezekani hata kidogo
 
Precise Pangolin

JF-Expert Member
Jan 4, 2012
12,671

Mimi nilikuwa nashangaa jangili mzima azunguke bila faida yeyote? Hilo anaweza akafanya Dr Slaa tuu
 
Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,222
2,000
hiki chama ni mchwa, ni waizi hujapata kuona nilishangaa akina nape wamefutuka kama mama mwenye mimba ya miezi 7, tumbo namatako hinha..
 
Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,490
2,000
Huu ni ufisadi period.Ni sheria gani au ni bajeti gani ya Halmashauri inayoruhusu matumizi ya fedha za Halmashauri katika shughuli za kisiasa kwa vya na viongozi wake?

Hapa ni lazima watu wawajibike ili kukomesha kabisa upuuzi huu

CCM wanapokea ruzuku Milioni 800 kila Mwezi.Huu ni mkakati wa ku-save fedha zao kwa ajili ya uchaguzi baada ya kuona wamebanwa kila mahali na upinzani kuzuia yale ya EPA 2005 . Sasa wamebuni mbinu mpya ya aibu na fedheha katika demokrasia yetu na pia kufuru kwa Umma wa watanzania.Haikubaliki hata kidogo na inahitaji hatua za kibunge na nje ya bunge .Haiwezekani hata kidogo

Ufisadi huu hauna tofauti na ule wa EPA
 
Ben Saanane

Verified Member
Jan 18, 2007
14,595
2,000
Mimi nilikuwa nashangaa jangili mzima azunguke bila faida yeyote? Hilo anaweza akafanya Dr Slaa tuu

Anavaa ndala kwenye mikutano kuhadaa wananchi huku akiwaibia fedha hata za madawa kwa wagonjwa katika hospitali za wilaya ? Huko kote walikopita kwa ufisadi huu tutapita kama hatua za kisiasa lakini hatua za kibunge na kisheria ni lazima zichukuliwe dhidi ya wote waliofanya ubadhirifu huu na matumizi mabaya ya madaraka
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,981
2,000
Hizo fedha zilitengwa kwenye bajeti ipi? maccm wezi kila mahali, kinana mwenyewe hajaelezea ujangili alioufanya wa kuua tembo wetu sasa kaibukia kwenye fedha za halmashauri shenzi kabisa!!
 
Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,490
2,000
Anavaa ndala kwenye mikutano kuhadaa wananchi huku akiwaibia fedha hata za madawa kwa wagonjwa katika hospitali za wilaya ? Huko kote walikopita kwa ufisadi huu tutapita kama hatua za kisiasa lakini hatua za kibunge na kisheria ni lazima zichukuliwe dhidi ya wote waliofanya ubadhirifu huu na matumizi mabaya ya madaraka

Halafu eti anadanganya Taifa kwamba Lissu kazuia wananchi wasichange ndiyo maana maendeleo hakuna.

Mungu atawalipa kwa ufisadi na uovu huu.
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,869
2,000
Huu ni ufisadi period.Ni sheria gani au ni bajeti gani ya Halmashauri inayoruhusu matumizi ya fedha za Halmashauri katika shughuli za kisiasa kwa vya na viongozi wake?

Hapa ni lazima watu wawajibike ili kukomesha kabisa upuuzi huu

CCM wanapokea ruzuku Milioni 800 kila Mwezi.Huu ni mkakati wa ku-save fedha zao kwa ajili ya uchaguzi baada ya kuona wamebanwa kila mahali na upinzani kuzuia yale ya EPA 2005 . Sasa wamebuni mbinu mpya ya aibu na fedheha katika demokrasia yetu na pia kufuru kwa Umma wa watanzania.Haikubaliki hata kidogo na inahitaji hatua za kibunge na nje ya bunge .Haiwezekani hata kidogo
Huo ni umbumbumbu wenu tu na kujitia vipofu. Kinana anaenda kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye miradi inayotekelezwa na Halmashauri. Hafanyi kazi za kichama na ndo maana kwenye ziara zake viongozi wote wa kiserikali wanakuwepo. Nyie CHADEMA inawauma nini? Mbona hamuulizi matumizi mabaya ya fedha za ruzuku wanazotafuna viongozi wa chama chenu?
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,869
2,000
Halafu eti anadanganya Taifa kwamba Lissu kazuia wananchi wasichange ndiyo maana maendeleo hakuna.

Mungu atawalipa kwa ufisadi na uovu huu.
Si kadanganya bali wananchi wenyewe ndo wamesema kuwa Lissu anazuia michango. Hakika hawa akina Lissu wameingizwa chaka na akina Mbowe. Ukienda kilimanjaro, wananchi wanachangia kweli shughuli za maendeleo
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,869
2,000
Hizo fedha zilitengwa kwenye bajeti ipi? maccm wezi kila mahali, kinana mwenyewe hajaelezea ujangili alioufanya wa kuua tembo wetu sasa kaibukia kwenye fedha za halmashauri shenzi kabisa!!
Nyie serikali ya CCM inawahusu nini? Acheni hizo bana. Subirini mwaka 5025 CHADEMA watakapotwaa madaraka ndo muje kuhoji
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,869
2,000
Cha kushangaza, taarifa yenyewe imeandikwa na Gazeti la Udaku lakini watu wameshupalia kweli
 
Precise Pangolin

JF-Expert Member
Jan 4, 2012
12,671
2,000
Huo ni umbumbumbu wenu tu na kujitia vipofu. Kinana anaenda kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye miradi inayotekelezwa na Halmashauri. Hafanyi kazi za kichama na ndo maana kwenye ziara zake viongozi wote wa kiserikali wanakuwepo. Nyie CHADEMA inawauma nini? Mbona hamuulizi matumizi mabaya ya fedha za ruzuku wanazotafuna viongozi wa chama chenu?
Jibu hoja wewe ELIZA-BON hela wanayotumia kutoka kwa hao wakurungezi zilitengwa kwenye bajeti au ndio kahamishia ujangili wake huko?
 
lane

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
894
225
Kule kwenye kapu kuu yaani BoT wamekwapua Bil 200, na dalili za kurejesha hazipo. Huku nako kwenye halmashauri zetu fedha kiduchu kwa ajili ya miradi ya maendeleo inatumika kugharamia shughuli za kisiasa za CCM. Shame CCM, uovu mkubwa huu. Ujangili na wizi

Halafu hapo hapo watanzania hawa hawa ndio wafuasi wakuu wa CCM, tena wanaipa kura ila wanakuwa wa kwanza kulalamika maisha magumu na hudum mbovu za kijamii

Ewe mtanzania mwenzangu - adui mkubwa wa mendeleo ni wewe mwenyewe. Kura yako, sapoti yako oende kwa watetezi na wakombozi wa kweli ktkt nchi yetu. Sote tuisapoti CHADEMA

Inauma sana haya mambo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom