Ziara ya KM wa CCM W. Mukama Kanda ya Ziwa: Matukio na Yatokanayo

Member anayejua anisaidie kufumbua hili hivi Mkama ni Mwanza - Ukerewe au Mara??
 
Veronica Modest na Raphael Okello, Bunda.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Bw. Wilson Mukama amewatoa wananchi hofu akitamba kuwa CCM ni kama taasisi hivyo si rahisi kufa kama wapinzani wanavyodai.

Alisema kuyumba kwa chama hicho kinatokana na changamoto nyingi zinazojitokeza katika vyama mbalimbali vya kisiasa duniani katika karne ya 21 na kwamba hiyo haijathibitisha kuwa CCM inakufa.

Akihutubia mamia ya wananchi na wanachama wa chama hicho katika Wilaya ya Bunda jana, alisema kutokana na changamoto hizo CCM imechukua hatua madhubuti ya kujipanga.

"Ni kweli tuko katika kipindi kigumu cha karne ya 21 ambacho chama chetu kinakabiliwa na changamoto nyingi, hivyo tumeamua kujiangalia upya kukabili changamoto hizo," alisema Bw. Mukama.

"Lakini CCM ni taasisi kubwa, taasisi ambayo imeshajiimarisha ikiwa na watumishi wengi wenye ujuzi katika siasa, kwa hiyo taasisi kama shule,hospitali na zinginezo haziwezi kufa kiurahisi kwa sababu kama kuna
watendaji wasiofaa huondolewa kazini na kuwaajiri wengine, hiyo ndio CCM,"
alisema.

Alibeza alichodai kauli ya wapinzani kuwa Rais Jakaya Kikwete hawezi kuongoza nchi hadi mwaka 2015 kwa madai kuwa nchi imemshinda na kusababisha maisha magumu kwa kupanda kwa gharama ya maisha.

Alieleza kuwa Rais Kikwete alichaguliwa kwa kura nyingi ya wananchi katika uchaguzi wa kidemokrasia, hivyo si rais kuondolewa katika nafasi hiyo kiurahisi mpaka muda wake utakapofika.

Pia alibeza kauli kuwa kujivua gamba kwa CCM haitasaidia chama hicho kujiimarisha kwa kuwa sumu ya nyoka ni ile ile hata akijivua gamba, akisema sumu ya CCM ni mbinu zake za kuendelea kushika dola.

Alifafanua kuwa baadhi ya watu wanatumia vibaya dhana ya CCM ya kupambana na wafanyabiashara mafisadi ndani ya chama hicho na kueleweka kuwa wafanyabiashara wote hawatakiwi kuwa wanachama au viongozi ndani ya chama hicho.

"Si kwamba CCM haiwataki wafanyabiashara wote kwa sababu ukifanya hivyo umekiua chama, tunachomaanisha ni wale wanaotumia fedha zao kuhujumu nchi," alisema Bw. Mukama.

Kuhusu vyama vya siasa kuongozwa na wafanyabiashara, alikiponda Chama chaDemokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kuwa waasisi wake ni wafanyabiashara wakubwa ambao Hayati Mwalimu Nyerere alikataa sera zao wakati wa uhai wake.
 
CDM kumbe chama cha wafanyabiashara wakubwa akina Ndesapesa; sie wakulima tufie CCM kimetutoa mbali! Hao CDM wakapige kampeni Samora Street na Uhindini kwa wafanyabiashara wenzao. NAMSHUKURU MUKAMA KWA KUTUFUMBUA MACHO!
 
kakufungua eeee, basi mwambie akuoshe na tongotongo kabisa manake zinaonekana bado zipo tele!!!
 
KAMA TAASISI HAITAKUFA, kama KANU!
Lakini kama chama tawala ITAKUFA..KAMA KANU!
Aksante Mukama kwa kugundua!
 
Mukama wakati akiwa mkurugenzi wa jiji ndio alimpa Kingunge tenda ya kukusanya ushuru kwenye stendi kuu ya mabasi ubungo huku akijuwa wazi kampuni ya kingunge ilikuwa haijasajiliwa bado, siwezi kumsikiliza tapeli huyu hata kidogo.
 
Veronica Modest na Raphael Okello, Bunda.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Bw. Wilson Mukama amewatoa wananchi hofu akitamba kuwa CCM ni kama taasisi hivyo si rahisi kufa kama wapinzani wanavyodai.

Alisema kuyumba kwa chama hicho kinatokana na changamoto nyingi zinazojitokeza katika vyama mbalimbali vya kisiasa duniani katika karne ya 21 na kwamba hiyo haijathibitisha kuwa CCM inakufa.

[/B]

I am sure privately, Mukama cannot quite believe the fall of CCM' fortune. Only last year viongozi wakuu wa ccm walikuwa wanasema vyama vya upinzani ni vya msimu. Less than 8 months later Mukama anatoa statement ya kama CCM itakufa au la!!! Niseme kama kweli Mukama na timu yake wanataka jina la ccm liwepo kwenye list ya mzeeTendwa (siongelei kubaki madarakani hapa) basi inabidi (a) waachane na propaganda, (b) waombe msamaha kwa umma for turning this country upside-down. Lakini nina wasiwasi hawa wakubwa wataendeleza u-special wao kama ambavyo Makinda ametuonesha kwa kujiweka mbali na 'wahalifu' yaani watanzania.
 
Ndugu wananchi, samaki akioza hata ukimkaanga au ukambanika au ukamchemsha, huwezi kuondoa wala kumaliza uozo wake!!!
 
Itaishi kama historia. Mkama anataka kutuaminisha kuwa ccm ni everlasting which is a typical intelectual heresy. Akamwambia jk maana atafurahi kuambiwa hivyo.
 
inaelezwa kuwa rais Keneth Kaunda naye pia alikuwa na washauri aina ya Mkama ambao walikuwa hawamuelezi ukweli kuwa chama tawala hali yake ni mbaya na kina hatari ya kushindwa katika uchaguzi na kupotea katika ulingo wa siasa, Kaunda alielezwa kuwa chama kinapendwa na hakiwezi kufa kama kikwete anavyodanganywa na kina Nape na Mkama, sasa tulisikia mbunge wa ccm bukoba kapigwa mawe mkutanoni, tumesikia tena kilichotokea tarime, endeleeni na porojo kitawakuta kilichowakuta UNIP na KANU, kiukweli hampendwi kabisa na wananchi.
 
Gadaffi naye si anasema bado raisi wa libya sishangai kama kikwete bado anasema ni raisi wa Tanzania.
 
Ujamaa umempofusha Katibu mkuu wa CCM Wilson Mukama ametangaza kuwafukuza Wafanyabiashara wote ndani ya chama hicho wakati alipoanza ziara ya siku nane katika mkoa wa mara ,Miongoni mwa wafanyabiashara waliotajwa na mukama akiwa kijijini kiabakari ni kama wafuatao
1.Rostam Aziz
2.Abdulharaman Kinana
3.Nimroad Mkono
4.Mwita Gachuma
5.Anthony Dialo
6.Salim Abri
7.Aziz Suleiman Premji
8.Deo Sanga
9.Bernard Membe
10.Mohsin Abdalah Sheni
11.Kisyeri Chambiri
12.Mohamed ABOOD
13.Nawab Mullah
 
Mukama atakamuliwa tu hana lolote la kutuambia kimsingi tumeichoka CCM hata kwa fimbo hatuitaki, kuwavua magamba wenzie kashindwa kuwafukuza ataweza? Asituletee porojo hapa
 
Back
Top Bottom