Ndio kazi ya viongozi wa Dini, kama wewe ni mkristo utakuwa unajua kazi za watu hawa, Nabii Eliya dhidi ya utawala wa yeroboam na wenzake, Nabii Daniel dhidi ya utawala wa Mfalme nebkadneza wa babeli, Nabii Yohana wa ufunuo dhidi ya utawala mkatili uliokithiri maovu na uonevu wa Dola ya Rumi n.k, Kazi ya kiongozi wa Dini ni kukemea maovu popte yanapoyokea kwa nguvu zote hata kama ni serikali ambayo watawala huwa wanaipenda.
Ndio maana tunawashangaa viongozi wengine wengi wa dini wanaonyamazia unyama huu, tunajiuliza wanafundisha neno la Mungu lipi? Kwa maslahi ya nani??
Juzi humu tumewashambulia sana viongozi wa katoliki kwa kutochukua hatu ya kukemea kama kanisa.
Gwajima ni wa kuungwa mkono na kila mpenda haki na sio kumwita mpuuzi.