Zembwela na Mizengwe

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Wana jukwaa, hivi yule msanii nguri wa kundi la vichekesho la Mizengwe lenye kuonekana ITV yupo wapi maana haonekani siku hizi!! Na ana dili gani?? Anaejua atujulishe wajameni
 
yuko east afrika redio, anatangaza kipindi cha ASUBUHI MIDA YA SAA MBILI HADI SAA NNE HIVI
 
yuko east afrika redio, anatangaza kipindi cha ASUBUHI MIDA YA SAA MBILI HADI SAA NNE HIVI
Ni kweli yupo EA Radio, aliacha kule vichekesho vya Mizengwe. Ni katika kufanya kitu m-badala na kujiwekea malengo katika maisha. unafanya uigizaji lakini inafika mahali unaweka malengo kwamba muda flani ukifika ntaacha na kufanya kitu kingine. Ni kitu kizuri
 
yuko east afrika redio, anatangaza kipindi cha ASUBUHI MIDA YA SAA MBILI HADI SAA NNE HIVI
Ni saa tatu mpaka saa Saba monday to friday yupo na dogo mmoja Michael Baruti (and as far as I can tell they are doing a best job) wanapitia magazeti pia kuna watu wanapiga simu kuelezea dukuduku zao kwenye mitaa yao (wanaita lakuvunda halina ubani)... I think hiki ndio best kipindi cha EA radio
 
Na ktk hiko kipindi anakuwaga serious au kama kawaida yake?
Kuna yule mwigizaji mwenzake anaitwa Mkwere, niliwahi ona anahojiwa akielezea mafanikio yake kuwa amejenga nyumba ya kisasa kutokana na mizengwe.
 
Yupo serious.... lakini huwa wanazinguana na mwenzake Michael Baruti....... Nakumbuka majuzi kuna mtu alifungwa miaka 300 kwa kugushi sahihi za watendaji na kula pesa za kujengea shule.... sasa wakawa wanacompare na kesi ya Chenge ya kuua ambayo maximum sentence yake ni either kifungo cha miaka 3 au faini ya tshs. 50,000/=

Pia wameshikia bango issue ya Dowans.... Zembwela anasema kwamba hatalipa... wakati mwenzake huwa anamwabia atalipa tu labda ahame nchi.....
 
Wana jukwaa, hivi yule msanii nguri wa kundi la vichekesho la Mizengwe lenye kuonekana ITV yupo wapi maana haonekani siku hizi!! Na ana dili gani?? Anaejua atujulishe wajameni

Sina uhakika kama amesomea masuala ya uandishi wa habari ila anafanya vizuri sana katika kipindi anachokiendesha.
 
Wana jukwaa, hivi yule msanii nguri wa kundi la vichekesho la Mizengwe lenye kuonekana ITV yupo wapi maana haonekani siku hizi!! Na ana dili gani?? Anaejua atujulishe wajameni

jamani ni mtu ambaye ana mchango mkubwa kwa watanzania kupitia sanaa yake watu wameelimika na kuburudika.
 
Niko nje ya nchi lakini miezi mitatu miwili nikiwa bongo alikuwa anazungumzia muziki wa miaka ya 70. Alikuwa sahihi sana, maelezo yanakupa picha halisi, na mtiririko mzuri ulionikamata mimi kama msikilizaji. Nampata Dole, tano, he is good GOD BLESS HIM.
 
Ndugu, JF is a news and knowledge bank. Kama mtu anauliza jambo mjibu kama huwezi kujibu kaa kimya. Msije kuwa kama wale watoa maoni wa kwenye ITV ambao wanatoa jibu SIJUI. Kama hujui kaa kimya siyo unachonga, toa jibu au kaa kimya!
 
Nimemsikia pia EATV, yupo safi kama vile fani kaanza siku nyingi...kama aliamua mwenyewe, basi kacheza karata dume, kama kuna mtu alimshauri, basi ni mtaalam wa kuibua vipaji..
 
Back
Top Bottom