Zembwela acha upotoshaji...!

Zembwela acha upotoshaji...!

...so kazi ya mbunge/diwani ni kuwabana,na kama amefanya hivyo na bado hamna kilichofanyika nani alaumiwe ? Hapo ndo tunapishana mtazamo na zembwela yeye anatupa lawama kwa mbunge/diwani wakati si kazi yake. Tukienda mbali zaidi hiki ndo chanzo cha rushwa,mfuko wa jimbo na serikali kutojali kauli za wabunge maana inajua haitawajibishwa kwa makosa yake bali mbunge ndo atawajibishwa kwa kosa ambalo kimsingi ni la serikali...
Unaweza kuangalia tatizo hili kupitia kwenye mfumo wa uundwaji wa Halmashauri zetu na uwajibikaji wake.

Shughuli za Halmashauri zinafanywa kupitia vikao vyake. Kwa mfano mkutano mkuu wa Halmashauri, katibu wake huwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri. Vikao vya kawaida vya Halmashauri hizo katibu wake huwa ni Mkuu wa Idara. Mkurugenzi wa Halmashauri ni cheo cha kuteuliwa na Rais... Aidha kwa wakuu wa idara nao wanateuliwa toka serikalini. Hapa ndio walakin unapoanzia.

Hivyo basi labda tuanzie hapa na kuona je kuna wakurugenzi wenye kudharau maelekezo ya madiwani wao kwa sababu tu ni wateuliwa wa Rais, na kwa namna moja ama nyingine hawawajibiki moja kwa moja kwa Madiwani?

Je kimefanyika nini ili kuona kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri anachaguliwa na Madiwani, ili aweze kuwajibika moja kwa moja kwa Madiwani hao na sio venginevyo?
 
Nimefuatilia kwa muda mtazamo wa huyu mwanahabari zembwela na nimegundua kunamambo hafikirii sawa. Kwa mtazamo wake ni kwamba mbunge na diwani ndo mwenye dhamana ya maendeleo ya jimbo. Sitaki kuhoji kiwango chake cha elimu,lakini kwa mtu mwenye ufahamu unajua nani anawajibika kuleta maendeleo na nani anapaswa kupeleka vipaumbele vya wananchi husika. Bwana mdogo zembwela nadhani unapaswa kuwaunganisha vijana kuishinikiza serikali kutimiza yale mliyowatuma wabunge wenu wakayapeleke serikalini kwa kutengewa bajeti na utekelezaji. Lakini ukiendelea kuwaaminisha watu uzembe wa serikali ni wa mbunge unakosea. Sote tunawajua wabunge wawajibikaji na wazembe na lazima tuwawajibishe,lakini hujuma za serikali kwa baadhi ya wabunge kuwafanya hawawajibiki ndo kumezaa mfuko wa jimbo. Sasa wabunge wakiwa watendaji nani ataisimamia serikali ? Mwisho nilistuka na kuogopa zembwela alipowahamasisha wananchi kumng'oa diwani bila uchaguzi eti hawawezi kusubiri uchaguzi wakati anachelewesha maendeleo. Nahisi sheria ya uchaguzi haijui. Amekomaa na azimio la arusha bila kujua kuna azimio la zanzibar wameleta ccm.

kumuita zembwela mwanahabari ni kushushia hadhi tasnia ya habari.
 
kumuita zembwela mwanahabari ni kushushia hadhi tasnia ya habari.

...dah..! mkuu umenistua kidogo,kwani dogo ni full kanjanja..! Siamini kama ipp wako loose namna hii...
 
Unaweza kuangalia tatizo hili kupitia kwenye mfumo wa uundwaji wa Halmashauri zetu na uwajibikaji wake.

Shughuli za Halmashauri zinafanywa kupitia vikao vyake. Kwa mfano mkutano mkuu wa Halmashauri, katibu wake huwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri. Vikao vya kawaida vya Halmashauri hizo katibu wake huwa ni Mkuu wa Idara. Mkurugenzi wa Halmashauri ni cheo cha kuteuliwa na Rais... Aidha kwa wakuu wa idara nao wanateuliwa toka serikalini. Hapa ndio walakin unapoanzia.

Hivyo basi labda tuanzie hapa na kuona je kuna wakurugenzi wenye kudharau maelekezo ya madiwani wao kwa sababu tu ni wateuliwa wa Rais, na kwa namna moja ama nyingine hawawajibiki moja kwa moja kwa Madiwani?

Je kimefanyika nini ili kuona kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri anachaguliwa na Madiwani, ili aweze kuwajibika moja kwa moja kwa Madiwani hao na sio venginevyo?

...hakika mkuu hoja yako ni nzito sana,kukosa nguvu ya kuwawajibisha watendaji wa serikali ni pigo kubwa sana kwa wabunge/madiwani...
 
How does CHADEMA comes in? Hey boy think far and clear all ur dew in ur brain b4 the thumb types.
 
...maazimio yote ni kwaajili ya tanzania,majina yalikuja kwa kuzingatia mkutano wa hilo azimio ulifanyika wapi....

lakini unajua ya kwamba tokea mwanzo zanzibar ilikuwa bado nichi ndani ya nchi? Tokea zanzibar walipofanya mapinduzi walianza kuwa na rais wao na jeshi,bunge n.k

embu nitabanaishe kidogo, azimio la arusha lilifanya kitu gani zanzibar au azimio la zanzibar lilifanya jambo gani huku tanganyika
 
Acha kupanic huo Mfano nimeutoa kuoonesha kuwa Zembwela yuko sawa na Kazi ya mbunge ni kuhishinikiza serikali kuahakikisha maendeleo yana patikana na hakishindwa yeye ndiye wa kwanza kupewa lawama!

Mnyika Swala la maji limemshinda na bahati mbaya hawezi kurudi bungeni Tena!

unaweza kusema sababu gani hawezi kurudi? Je! Ni kwa mtu mwenye uelewa mf. Swala la maji analishughulikia au la? Ni mara ngapi tumesikia blabla za mawaziri wa miundo mbinu na vilaza wa dawasco wakitoa ahadi hewa? Je kama angekuwa halifanyii kazi hao vilaza wangekuwa wanajikosha kwa blabla zao? Anyway he play on his part.
 
Tatizo Bawacha mnachojua ni matusi tuu! Jimbo linapokosa maendeleo wa kwanza kuulizwa ni Mbunge!

tuweke vyama pembeni, maendeleo ya wananchi yanaanzia kwa madiwani na baada ya hapo yanaenda kwa mbunge. Madiwani wako kila sehemu katika wilaya. Kupitia mabaraza yao wanawakilisha mahitaji yao ya kata husika ambapo na mbunge anakuwa ni mmoja kati ya wajumbe ya hiyo kamati. Mbunge anapoenda bungeni inamaana anawakilisha mahitaji yote ya wananchi kupitia vikao walivyokaa na kuchambua vipaumbele. Wakati wa bunge la bajeti ni kipindi ambacho mbunge anapambania mahitaji ya wananchi wake ili katika bajeti awe amepatiwa fedha. Si fedha zote za maendeleo zinapitishwa na bunge ila kuna baadhi ambazo kupitia halmashauri husika zinaweza kuwa na njia za mapato ambapo madiwani na wabunge wanayajua. Hapo pia ni jukumu la diwani na mbunge kuangalia matumizi halisi ya mapato na kupitia hayo mapato maendeleo yanapatikana. Huwezi kuwa mnalipisha magari mwaka mzima halafu mshindwe kutengeneza stand bora.
 
...so kwa mtazamo wako mnyika ndo anapaswa kujenga miundombinu ya maji toka ruvu mpaka ubungo,em tusaidie kuondoa uvivu...

chukulia katika familia kwani ni serikali tosha. Baba ndiye rais, je yeye anaweza kujua kuwa mtoto anashida bila kupewa taarifa?au bila yeye kupigiwa swala fulani kuhusu mtoto atalifanya kwa wakati? Neno nitakufanyia/nitakuletea kesho mwanangu linamaanisha nini katika familia?
 
Jukumu la Mnyika ni kuimiza serikali kuwaletea wana ubungo maji na alikubali kubeba jukumu hilo na kama hawezi sisi tutampa mtu mwingine 2015 .

samahani, simpigii chapuo mnyika sababu hanihusu. Hivi mara yako ya mwisho kumsikia akizungumzia maji ni lini? Au kwa mwaka huu umemsikia mara ngapi akilizungumzia hilo swala?au kijijini kwenu matatizo yenu yametekelezwa?
 
...kiongozi na kama amehimiza na akathibitisha kufanya hilo,lakini serikali haijaleta hapo inakuwaje,atabeba msalaba kwa niaba ya serikali au inabidi waziri awajibike....?

asante kaka
 
Wewe ni wakuonea huruma yani mtu kasema ukweli mnatokwa na povu!

uelewa wake ndiyo umekomea hapo. Shida wanapenda sifa za kijinga na kupinga /kudharau/kukashifu bila kutumia muda ya kujiuliza nini lilikuwa lengo. Wao wanchojua ni kutafuta sifa za kijinga.
 
kumuita zembwela mwanahabari ni kushushia hadhi tasnia ya habari.

samahani hivi mwandishi wa habari ni nani? Je wajua kuwa mwanavichekezo anaweza kutumia taaluma yake ya vichekesho kuelimisha jamii na kukosoa serikali?
 
lakini unajua ya kwamba tokea mwanzo zanzibar ilikuwa bado nichi ndani ya nchi? Tokea zanzibar walipofanya mapinduzi walianza kuwa na rais wao na jeshi,bunge n.k

embu nitabanaishe kidogo, azimio la arusha lilifanya kitu gani zanzibar au azimio la zanzibar lilifanya jambo gani huku tanganyika

...kubwa kwenye azimio la arusha ni miiko ya viongozi wa umma na azimio la zenj lililegeza ile miiko na kuruhusu baadhi ya mambo yaliyokatazwa na azimio la arusha. Kumbuka maazimio haya si ya bara au visiwani ni ya viongozi wote...
 
samahani hivi mwandishi wa habari ni nani? Je wajua kuwa mwanavichekezo anaweza kutumia taaluma yake ya vichekesho kuelimisha jamii na kukosoa serikali?

...yes anaweza kufanya hayo lakini asipotoshe jamii kwa uelewa wake mdogo ktk jambo husika,na huu ndo ugomvi wangu na zembwe...
 
Mleta mada atakuwa ni moja ya madiwani walioshindwa kuwaletea maendeleo wananchi.
 
madiwani lazima waulizwe kwa mfano nipo hapa mbezi beach lakini upande wa juu maeneo kama unakuja five star hall ni diwani wa chadema hakuna maendelo kwake miundo mbinu yake ni mibovu. upande wa chini ni diwani wa ccm kuna miundo mbinu mizuri sana,madiwani wengi wa chadema na wabunge wao hawajafanya kitu kabisa tangu wawe madarakani
 
Back
Top Bottom