JPM - Ukichagua upinzani sileti maendeleo | Heche - Kazi ya mbunge si kuleta maendeleo | Hapi - Kazi ya mbunge ni kuleta maendeleo. Nini nani ni nini?

JPM - Ukichagua upinzani sileti maendeleo | Heche - Kazi ya mbunge si kuleta maendeleo | Hapi - Kazi ya mbunge ni kuleta maendeleo. Nini nani ni nini?

Mwizukulu wa Buganda

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2024
Posts
810
Reaction score
2,039
Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania na majukumu ya Bunge, mbunge hana mamlaka ya kukusanya kodi, kuidhinisha matumizi ya fedha moja kwa moja, kuajiri watendaji au kutekeleza miradi. Majukumu yake makuu ni:
  • Kuwakilisha wananchi;
  • Kutunga sheria;
  • Kuisimamia na kuishauri Serikali;
  • Kushiriki kujadili na kuidhinisha bajeti na mipango ya maendeleo.
Ibara ya 63 ya Katiba inaeleza kuwa Bunge linaisimamia na kuishauri Serikali na kujadili pamoja na kuidhinisha mipango ya maendeleo na bajeti.

Je, kauli za viongozi hawa ziko sahihi?

1. Kauli ya Hayati Magufuli:


"Mkichagua upinzani sitoleta maendeleo"
Kikatiba, utekelezaji wa maendeleo ni jukumu la Serikali kupitia bajeti, wizara, taasisi za umma na mamlaka za serikali za mitaa. Hivyo maendeleo hayapaswi kutegemea chama cha mbunge aliyeshinda eneo husika. Kimsingi wananchi wote wanastahili huduma za serikali bila kujali chama walichokichagua.

2. Kauli ya John Heche:

"Kazi ya mbunge si kuleta maendeleo, hakusanyi kodi"

Kauli hii ina ukweli lakini tutambue kuwa Mbunge si mtendaji wa Serikali wala mkusanyaji wa kodi. Barabara, hospitali, maji na shule hujengwa na Serikali kupitia fedha za walipa kodi. Mbunge hana bajeti ya kutekeleza miradi hiyo moja kwa moja.

3. Kauli ya Ali Hapi:
Kazi ya mbunge ni kuleta maendeleo kwa kutumia nafasi zake bungeni kuwasilisha mahitaji ya wananchi

Zaidi soma Ally Hapi: Heche hajui wajibu wa mbunge, CHADEMA ni waongo, hawajui wajibu wao, hawajui sheria, hawajui taratibu za nchi

Hii pia ina ukweli. Ingawa mbunge hajengi mradi mwenyewe, ana wajibu wa kupigania mahitaji ya jimbo lake kwa kuhoji serikali, kushawishi mgao wa fedha, kujadili bajeti na kufuatilia utekelezaji wa miradi. Lakini ataweza vipi kuleta maendeleo ikiwa Serikali itaamua kutopeleka maendeleo eneo lake. Hii changamoto hasa imekuwa ikiwakuta wanabunge wanaotoka vyama pinzani ikiwa ni namna ya kuwakomoa ili wasiaminiwe na wananchi uchaguzi ujao.

Hivyo, kiuliza nani "analeta maendeleo", jibu sahihi zaidi ni Serikali kwani ndiyo mtekelezaji mkuu wa maendeleo. Mbunge ni mwakilishi na msimamizi anayepaswa kuyapigania na kuyafuatilia. Chama tawala huathiri maendeleo kupitia sera zake kwa kuwa ndicho kinachounda serikali.
 
Maendeleo yako hayaletwi na mwanasiasa yeyote labda huyo mwanasiasa awe mjomba au mtoto wa shemeji yako.
 
Siasa ni mojawapo ya ajira yenye ugumu mkubwa ndani yake vile mwanasiasa inakulazimu kusema uongo ili mambo yako yapate kusonga mbele
 
Kwani katiba mbovu inasemaje mikazi yao hawa?
 
Ukiwa na ulewa wa kina Bashite ndio huwezi elewa Heche anamaanisha nini!!., Kazi ya Bunge ni kutunga sheria na kuisimamia serikali!. Mbunge kazi yake kwa waliomchagua nikuchochea maendeleo kwa kuwasemea Bungeni!.
 
Kina Ally Hapi na CCM ndivyo walivyo, kueneza na kutumikia ujinga...

Concept yao kuwa "mbunge ni mleta maendeleo kwa maana ya kujenga barabara, shule, zahanati nk", ni fallacy & total utopia na ni ya kupumbazia watu wasiojua...

Better sasa kuwa, watu wanaanza kuamka na kuelewa...

Na kulifanya hili liwe hivyo, wakaanzisha "mfuko wa mbunge wa jimbo" na huwekewa pesa ambazo kiuhalisia sio chochote, si lolote na mara nyingi huwa ni za kuhongea tu...

Kwenye jimbo lolote lililo ktk halmashauri yoyote, pesa zote za maendeleo huwa chini ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri husika...

Ni ajabu kuwa, mbunge naye asiye hata na ofisi wala wafanyakazi eti naye ana kapu lake la pesa...

Ukiuliza huwa ni za nini na huyo mbunge huzifanyia nini, jibu lake ni blas blaa tu, hakuna lolote ni wizi mtupu...!;
 
Maendeleo yanaweza kuletwa na serikali hata kama hakuna wabunge. Muhimu serikali iwe ni ya watu wanaojielewa.
 
Back
Top Bottom