Zembwela acha upotoshaji...!

Zembwela acha upotoshaji...!

samahini, hivi azimio la arusha lilikuwa kwa ajili ya tanganika au tanzania? Na azimio la zanzibar ni kwa ajili ya zanzibar au? Maana zanzibar ni nchi inayojiendesha kwa katiba yake na serikali yake

...maazimio yote ni kwaajili ya tanzania,majina yalikuja kwa kuzingatia mkutano wa hilo azimio ulifanyika wapi....
 
"MKINICHAGUA MIMI" Nitahakikisha zahanati inajengwa na tunapata dawa.
Wazazi hamtatozwa michango ya madawati.
Soko la kahawa litapatikana nje ya nchi.
Tatizo la maji litakwisha. Nisisahau umeme.
Kwa kauli hii nani anastahili kuleta maendeleo kwa wananchi. Mr Politician anaona ahadi alizotoa hazijatekelezeka anataka kutuaminisha kuwa sio yeye aliyetoa ahadi.
WAJINGA NDIO WALIWAO

...mkuu si kila wakati wajinga ndo waliwao,wakati mpaka sasa watanzania tunanyonywa tu wote kwa pamoja wajinga na werevu na tumeshindwa kulikomboa taifa,wakati mwingine huwa nadhani waerevu ndo waliwao maana ukiwashawishi 1+1=11 wakaamini basi utawatawala hata miaka 50 ilimradi uwambie kesho utawafundisha ulivyopata jibu la 11,watasubiri kwa matumiani makubwa...
 
Ni mjinga mmoja anaboa hata hicho kipindi chake huwa sikisikilizi tena maana ni ujinga anaongeaga

A man with much knowledge is a knowledgeable man, not an educated one. The educated Cultivate confidence so as not to seem flustered when attention is placed upon you
 
Nimefuatilia kwa muda mtazamo wa huyu mwanahabari zembwela na nimegundua kunamambo hafikirii sawa. Kwa mtazamo wake ni kwamba mbunge na diwani ndo mwenye dhamana ya maendeleo ya jimbo. Sitaki kuhoji kiwango chake cha elimu,lakini kwa mtu mwenye ufahamu unajua nani anawajibika kuleta maendeleo na nani anapaswa kupeleka vipaumbele vya wananchi husika.
Yupo sahihi sana hapo, Kupitia kwa Wabunge na Madiwani inakuwa ni rahisi kwa serikali kujua matatizo na viupa umbele vya jimbo husika.

Kinachotakiwa kufanywa na Wabunge na Madiwani ni kujua kero zote za jimbo lake/wadi, baada ya hapo ni kujua kipi kitatuliwe mwanzo na kipi kifuatie! Then anakipeleka serikalini kwa utekelezaji tu!

Kutegemea serikali kuleta maendeleo, ni msingi mbovu wa mipango ya kutatua kero katika jimbo/wadi. Kwa mfano serikali inaweza kusema jimbo lile pajengwe barabara kiwango cha kokoto wakati kero kubwa ni zahanati.
 
Mii napita tu nyie endeleeni maana usilolijua ni sawa na usiku WA Giza nene.
 
Sijaona zembwela alipokosea.Mbunge na diwani kazi yao ni kusimamia serikali.Kama wameshindwa Kusimamia serikali kwa nini wasiwajibishwe?Kuna wabunge na madiwani wanaotimiza wajibu wao huo nakini serikali ikawa kichwa ngumu kwa hao watu wanajua.Watu wajua viongozi wanaowajibika na wale wasiowajibika.
 
Ni kweli kbs Zembwela anatatizo la kutojua pillars of the gvt na mipaka yake kiutendaji. Kipindi cha Super mix kinachorushwa hewani kuanzia saa 3 hadi 7 mchana EA RADIO kilikuwa more logical akiwepo Michael Baruti kwani yeye aliweza hata kumbishia Zembwela pale alipoona kunaombwe fulani la ufahamu!
 
Tatizo la Zembwela ni shule ndogo, mara nyingi huwa anaongea mambo asiyoyajua, na anataka kuonekana anajua kila kitu(much know) hapo ndipo huboronga bila kujijua
 
Huyo Mchumia Tumbo kama wengine wengi wenye ajira zao pale Lumumba... Kama vipi mpotezee tu...
Nimefuatilia kwa muda mtazamo wa huyu mwanahabari zembwela na nimegundua kunamambo hafikirii sawa. Kwa mtazamo wake ni kwamba mbunge na diwani ndo mwenye dhamana ya maendeleo ya jimbo. Sitaki kuhoji kiwango chake cha elimu,lakini kwa mtu mwenye ufahamu unajua nani anawajibika kuleta maendeleo na nani anapaswa kupeleka vipaumbele vya wananchi husika. Bwana mdogo zembwela nadhani unapaswa kuwaunganisha vijana kuishinikiza serikali kutimiza yale mliyowatuma wabunge wenu wakayapeleke serikalini kwa kutengewa bajeti na utekelezaji. Lakini ukiendelea kuwaaminisha watu uzembe wa serikali ni wa mbunge unakosea. Sote tunawajua wabunge wawajibikaji na wazembe na lazima tuwawajibishe,lakini hujuma za serikali kwa baadhi ya wabunge kuwafanya hawawajibiki ndo kumezaa mfuko wa jimbo. Sasa wabunge wakiwa watendaji nani ataisimamia serikali ? Mwisho nilistuka na kuogopa zembwela alipowahamasisha wananchi kumng'oa diwani bila uchaguzi eti hawawezi kusubiri uchaguzi wakati anachelewesha maendeleo. Nahisi sheria ya uchaguzi haijui. Amekomaa na azimio la arusha bila kujua kuna azimio la zanzibar wameleta ccm.
 
Yupo sahihi sana hapo, Kupitia kwa Wabunge na Madiwani inakuwa ni rahisi kwa serikali kujua matatizo na viupa umbele vya jimbo husika.

Kinachotakiwa kufanywa na Wabunge na Madiwani ni kujua kero zote za jimbo lake/wadi, baada ya hapo ni kujua kipi kitatuliwe mwanzo na kipi kifuatie! Then anakipeleka serikalini kwa utekelezaji tu!

Kutegemea serikali kuleta maendeleo, ni msingi mbovu wa mipango ya kutatua kero katika jimbo/wadi. Kwa mfano serikali inaweza kusema jimbo lile pajengwe barabara kiwango cha kokoto wakati kero kubwa ni zahanati.

...my point is,mbunge na diwani ndo wanapaswa kuwajibika kama mambo waliyowatuma hayajatimizwa...?je mbunge/diwani ndo mtekelezaji wa vipaumbele vya wananchi ?...
 
Ni kweli kbs Zembwela anatatizo la kutojua pillars of the gvt na mipaka yake kiutendaji. Kipindi cha Super mix kinachorushwa hewani kuanzia saa 3 hadi 7 mchana EA RADIO kilikuwa more logical akiwepo Michael Baruti kwani yeye aliweza hata kumbishia Zembwela pale alipoona kunaombweo fulani la ufahamu!


Kweli mkuu, alipoondoka Baruti kipindi kikapwaya hadi leo....Baruti alikuwa anamchallenge maana alimjua kuwa Zembwela ana ufahamu mdogo wa mambo mengi. Baruti akaibukia BBC. Huyo aliyenae kwenye kipindi ndio kitu kabisa, anachosema Zembwe yeye ni sawa tu.
 
Ni kweli kbs Zembwela anatatizo la kutojua pillars of the gvt na mipaka yake kiutendaji. Kipindi cha Super mix kinachorushwa hewani kuanzia saa 3 hadi 7 mchana EA RADIO kilikuwa more logical akiwepo Michael Baruti kwani yeye aliweza hata kumbishia Zembwela pale alipoona kunaombweo fulani la ufahamu!


Kweli mkuu, alipoondoka Baruti kipindi kikapwaya hadi leo....Baruti alikuwa anamchallenge maana alimjua kuwa Zembwela ana ufahamu mdogo wa mambo mengi. Baruti akaibukia BBC. Huyo aliyenae kwenye kipindi ndio hajui kitu kabisa, anachosema Zembwe yeye ni sawa tu.
 
sina tatizo na uhuru wa kuongea ila kwenye redio na unasikilizwa na watu wengi ni vema ukaongea unachokijua. kuliko usichojua usipotoshe umma nao wakaamini maelezo yasiyo sahihi

Mi Sidhan Kama Ni Upotoshaji Mkuu, Labda Wewe Ndo Umemwelewa Hivyo Lakn Jamaa Ni Jembe, Au Na Wewe Ni Kiongozi Nin?
 
Tupatie kazi za Mbunge na Diwani katika suala zima la kuondoa kero na kuleta maendeleo jimboni mwake

...kwa nijuavyo mimi mbunge/diwani ni sauti wa wananchi,so yeye kama kiranja anatakiwa kujua matatizo ya wananchi husika na kuiambia serikali,kufuatilia na kuisimamia serikaki itekeleze jukumu lake la msingi kwa wananchi. Pili ni kutunga sheria za kuendesha nchi,huu ni makubaliano ya kisheria ya wananchi na serikali wa namna ya kuishi kutenda,kuwajibika n.k. ....
 
Back
Top Bottom