Ndo cha ajabu hicho!! Yaani wanajilengesha wapewe zawadi halafu wanalaumu wanaume!! Lakini hili mzee ni tatizo kubwa maofisini mwetu humu..Hivi unaweza kutoa rushwa ya ngono kwa matakwa yako mwenyewe halafu mwisho wa siku ukasema wa kulaumiwa ni mwanaume?
Hebu wasaidie mabinti wenzako waweze kujitambua na kujiamini kuwa wanaweza kua-achieve jambo lolote lile bila kutoa au kuombwa rushwa ya ngono
hapana mkuu naona huyu mdau badala ya kuchangia mada anadeal na mimi. mimi sio kilaza atii
Hus nimekusoma mwaya.
Ukwelini kwamba maadili hayakosekani kwa wanaopokea bali kwa wanaotoa pia.Wote wapo kwenye kundi moja, maana ikitokea mmoja akiamua katu katu hatoi/hapokei mwenzaki hawezi kumlazimisha.Kuna namna nyingi tu za kuepukana na rushwa ya ngono (kwa wale wanaodai walilazimika kutoa) sema tu watu wanapenda urahisi.Hawataki kuhangaikia wala kupigania kile wanachotaka.
Sema case namba moja naweza kumtetea maana kwa kua binti mdogo amabae amekosa support ya mwalimu wake wa darasa ,pengine hata wazazi/walezi anaweza hata akabakwa ikiwa hatoamua mwenyewe kukubali. Inatisha kweli kwamba mtu unaemtegemea kukulinda hatoi msaada unaohitajika na kuishia kumwambia bibti avumilie.Mi mijitu kama hiyo ningeipeleka jela yote. . .
Mi naishi dunia ambayo sitoi wala sipokei zawadi zisizoeleweka, mambo ya kukabwa kabari kisa chips mayai siwezi mie.wee Lizy
unaishi dunia ipi hiyo
ambayo mwanamme akikupa lazima ulipe?
Njoo uone huku kwetu kwa Tumbo
tunapokea na ukileta zako unaitiwa mwizi
inategemea na mazingira ya kupokea
i can. ngoja nikuulize kitu ukiwa na gari mtu mwingine akakupa zawadi ya gari hutopokea?
My daddy taught me well, kujitegemea ndio mpango mzima.
EMT tuko pamoja, ila swala la kulaumu wapokeaji pekee mimi nakubaliana nalo pale inapotokea anaelazimika kutoa hiyo rushwa anapokua hajitambui kutokana na umri. Zaidi ya hapo, wanaendekeza wenyewe.Kama ambavyo mwalimu halazimiki kupokea ,ndivyo ambavyo mwanafunzi nae halazimiki kutoa .Utayari wao ndio unaopaswa kulaumiwa.Lizzy inawezekana umeshaulizwa hili au kuna mtu keshachangia huko nyuma. Umeshajaribu kuliangalia hili tatizo kwa jicho lingine? Sina maana kuwa unachosema sio kweli. Lakini kuna baadhi ya wanafunzi wachache ambao kutokana na hali wanayojikuta nayo wanakuwa hawana jinsi bali kugawa ngono kwa walimu wao. Wako baadhi ya wasichana wanawekwa na walimu wao katika mazingira ambayo itabidi wagawe ngono tuu. Remember the relationship kati ya mwalimu na mwanafunzi has never and will not be equal.
Sometimes, the student just doesn't have a choice ukizingatia mwalimu ndie anayeshika mpini. Ndio maana hata sheria inatambua kuwa uhusiano kati mwalimu na mwanafunzi is based on trust and confidence. But there some teachers out there who abuse this trust. Pia wapo wanafunzi ambao wanajua kuwa baadhi ya walimu wana-abuse this trust, so wanatumia this as an opportunity kujilengesha. Hao wanaogawiwa ngono ni wa kulaumiwa pia, otherwise wanafunzi wasingeweza kugawa.
Tatizo lingine ambalo nimeliona ni kwamba walimu wengi wa siku hizi did not intend to become teachers. Kwa wengine imetokea tuu kwamba hawakuwa na pass marks za kutosha kuwawezesha kusoma kozi walizozipenda, so the last option was kuwa mwalimu. Wanasema ualimu ni wito. Na mwalimu mwenye wito nai anayejua na kufanya kazi yake ipasavyo, sidhani kama atafanya ngono na mwanafunzi wake hata kama huyo mwanafunzi anajilengesha.
Sorry sikujibu maswali yako.
Cant even thnk 'bt it. Kwangu itakua km kula haram, kuchuma haram.
Muhm kujiamini tu. Ndo mana hatuendelei, utakuta mtu hata haqualify lkn anapeta kuliko mwenye uwezo. Mungu awalaani wote wanaotoa na kula rushwa especially hii ya ngono kwani wanizibia rizk wenziwao. Ameen
Mbaya sana aiseee. . .nashukuru umekubali kuwa mtoa rushwa na mpokeaji wote wana makosa na wote wanafaa kulaumiwa. lizzy huwezi amini huyo mwalimu yeye ana deal na watoto wa o level tu, watoto wa advance anawaheshimu. nawaonea huruma madogo maana huyo ticha naskia bado yupo na anaendeleza mchezo wake.
mimi kila mwaka nachukua zawadi ya mfanyakazi bora niko vizuri am professional ujue kuna mahali hapahongeki besides sijasoma elimu zenu uchwara za bongo. niko na confidence na kazi yangu ipo kwenye damu yangu siitaji kuhonga k nipate kazi cause nauzika kila mahali dunia nzima usipime
ngumu kuzuia kuombwa ila kuzuia kutoa inawezekana kwa asilimia zote. inabidi nifungue darasa rasmi la peer education.lol
Mbaya sana aiseee. . .
Sasa aliowatumia wote wanashindwa nini kumfundisha na yeye somo?Watafute namna ya kumkomesha.
hivi mwanamke wa miaka 45, ana kadegree umfunze nini?
Bora mtoto au kijana aliyepinda hufunzwa lakini mtu mzima achana naye amalizie maisha yake yalobaki
cha kujiuliza, wote tumeng'aka sasa wanaofanya ni akina nani?
Ningependa kusikia ushahidi toka kwa victim angau mmoja
tunawahukumu bila kuwapa nafasi ya kusikia upande wao
shule gani hiyo?nashukuru umekubali kuwa mtoa rushwa na mpokeaji wote wana makosa na wote wanafaa kulaumiwa. lizzy huwezi amini huyo mwalimu yeye ana deal na watoto wa o level tu, watoto wa advance anawaheshimu. nawaonea huruma madogo maana huyo ticha naskia bado yupo na anaendeleza mchezo wake.
Sasa wewe Hus unategemea kama alitoa sec. , akatoa chuo, akatoa kazini ataacha kabla hajafikia malengo?hivi hadi wazee wanatoa rushwa za ngono!? Na uzee huo elimu ya ufahamu bado hana tu! Mi naona wanawake tuliochangia hapa hata kumi hatujafika, labda wahanga watakuja kutoa ushuhuda.
Hii inanikumbusha wadada wapenda dezo waliokuwa wakienda JKT enzi hizo. Bahati nzuri JKT imefutwa vinginevyo kwa ukimwi huu wa sasa wengi wangeangamia kwenye makucha ya maafande wenye uchu wa ngono.