Zawadi Ngoda soma hapa kwanza tafadhali

Zawadi Ngoda soma hapa kwanza tafadhali

Jamani wako wapi hawa!!!??? Nina shauku ya kusikia maoni yao juu hili!! Au bado wanajadili? ILA MSIJE NA MATUSI, TUNAHITAJI HOJA ZENYE MASHIKO!! Tafadhari!!!
 
By ABDULWAKIL SAIBOKO, 18th October 2011 Daily News

THE World Bank has called for introduction of cash transfer to people as poverty is on rise among individuals in Tanzania despite general economic growth.

The WB's report issued on Tuesday with a title; 'Tanzania: Poverty, growth and public transfers' noted that
(1) poverty in the country was widely spread.

"The report
(2) proposes that for the country to have a sustainable economic development, two options should be enforced, one of which is cash transfer and another is public works", said the WB Lead Social Protection Specialist, Ms Anush Bezhanyan.

Ms Bezhanyan observed that
(3) cash transfer involves giving cash to individuals who are unable to work in which the government is supposed to dictate modalities of expenditure and make a follow-up to get feedbacks.

"The government can, for example, direct the beneficiaries of the cash transfer to use the monies in taking their children to school, and then a follow-up must be made to see whether the target has been achieved," she said.

On public works, Ms Bezhanyan said the government was required to
(4) allocate some public works in people's localities from where the poor would earn something in terms of cash.

Citing examples, she said Ethiopia was one of the African countries which could provide best practice on how the two modes could effectively transform lives of individuals, hence, lead to overall economical growth.

WB's Consultant, Mr Jim Smith said
(5) 83 per cent of the poor are in rural areas but there are many poor people in non-poor areas. "Targeting specific areas basing on geographical locations is not proper, the report shows that poverty in the country was evenly spread," he said.

The report also shows that
(6) over 6.4 million people live below the food poverty line, some (7) 10 million people are facing severe seasonal food insecurity and about (8) 12.7million people are below the basic needs line.

According to the report, the existing projects on poverty reduction have a limited coverage which is less than one per cent of the poor and
(9) there are inclusion and exclusion errors due to generalization approach.

It suggests that "the government should move towards a single national programme large enough to cover the country and big enough to make a difference".

The Tanzania Social Action Fund (TASAF) System Manager, Mr Ladislaus Mwamanga, said the fund has already started working on some of the WB report's recommendations.

"We have already started cash transfer as a pilot project in three districts whereby some
10 (Tsh 16,000/-) US dollars (What ?) are disbursed to every household per month," he said.

He said that the pilot project which began in 2008 covers Bagamoyo, Kibaha and Chamwino districts in Cost and Dodoma regions respectively.

"Already 200 households have benefited and the project has already received some 1.9 million USD from Japan Social Development Fund and 4.5 million USD from WB to support the project's implementation", he said.

MAMBO MAZITO YALIOIBULIWA NA WATAALAM WA BENKI YA DUNIA KUHUSU WA-TANZANIA TULIVYOCHAKAZWA NA UMASIKINI CHINI YA UONGOZI WA CCM NA UENDEKEZAJI YA UFISADI NA SOKO HOLELA NCHINI


tab-A1-01_zm.jpg


(1) poverty in the country was widely spread.

Benki ya Dunia imebaini kwamba umasiki sasa umesambaa kile pembe ya taifa letu kuliko wakati wowote katika historia ya Tanzania hivyo kuhimiza hatua kadhaa za dharura kuokoa meli ya 'MV Walazwahoi' nchini tuzame jumla.

Kwa maoni ya wataalam hawa wa Benki ya Dunia na uchambuzi makini wa mienendo ya uchumi wa nchi yetu, wao wanaona kwamba kama umasikini ungekua ni maji baharini basi tayari yameanza kupanda juu kidogo ya mustachi kuelekea kabisa puani.

(2) proposes that for the country to have a sustainable economic development

Pendekezo lao la jumla ni kwamba nchini Tanzania ni wakati mwafaka tukaanza kuzingatia misingi imara ya kujenga Uchumi wa nchi yetu wenye uwezo wa KUJINAWIRISHA YENYEWE bila kulazimika kubughudhi hasa mataifa ya Magharibi kila siku kuruka na mi-dege kwenda kutembeza bakuli.

Ndugu zangu unposemwa vibaya hivi, kwa mtu mstaarabu ni sharti ukakae chini na kujichunguza mwenye kwa kujiuliza maswali kibao juu ya hali hiyo huku ukitangulia na swali zito zaidi la 'KULIKONI'? Na mimi hapa najiuliza swali kwamba kulikoni Benki ya Dunia watuambie hivi?

Pengine ni kwamba mambo yenyewe yaliotufikisha hapo ni pamoja na haya haya mambo ya UFISADI ambayo ndio mpaka hivi sasa yametufanya tusitake kusikia hata baadhi ya majina ya wenzetu wakiwemo Edward Lowassa na Richmond, Chenge na Vijisenti, Mhajemi Rostam Aziz na Dowans na JK naye kauli ya kwamba hajui kwa nini tu masikini - mambo ambayo ni kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya kuendeshwa kwa Uchumi unaofuata mfumo wa Soko Holela?


(3) cash transfer involves giving cash to individuals who are unable to work

Vile vile kumedhihirika kwa Benki ya Dunia kwamba kuna UKAPA mkubwa wa Umasikini wa kipato kiasi kwamba wamegundua wazi kwa Wa-Tanzania kibao tusiokua ama na ajira au uwezo wa kufanya kazi (sisi vijana wa vijiweni kila kona ya nchi, akina mama wanaokatiliwa na mfumo dume kutopata ajira, wato na wazee - mfano wastafu wa Afrika Mashariki - ambao kwa misingi tu wa umri wao hawawezi tena kufanya kazi) n hivyo kusababishiwa umasikini wa kipato kutokana na maelezo ya hapo juu, tufike mahala tupangiwe utaratibu mwanana wa KUFIKISHA FEDHA TASLIM huku tulipo.

Mpaka hapa, laiti Mzee John Mimose Cheyo wa UDP asingalikua kwamba ndiye mlinda mlango wa mapato na matumizi ya serikali kupitia kamati yake ya miaka nenda rudi na hata kudaiwa kusaidia kuidhinisha ufisadi wa Richmond, Dowans, EPA na nyinginezo nyingi tu kutokea kwa masikitiko makubwa taifa zima, hadi hapa pengine ningempa heko kwamba mwisho wa siku Benki ya Dunia imeamua kuazima SERA YAKE YA KUTAKA KUTUJAZA MA-PESA MINGI mifukoni ili tupate kuendelea.

Lakini ni bahati mbaya mno kwa Benki Kuu hivi sasa wameazimia kushinikiza serikali ya CCM kutekeleza AZIMIO LA BENKI YA DUNIA KUTAFUTA KILA NJIA KUHAKIKISHA KWA WALAZWAHOI TUNAJAZWA MA-PESA hasa huku sehemu z vijijini; hatua ambayo kwangu mimi naona kama vile sera hii nzuri ya Mzee Ma-Pesa imelazimika kuazimwa na Benki ya Dunia LAKINI kwa kusudio la KUTIBU VIDONDA ALIVYOVISABABISHIA WA-TANZANIA yeye mwenyewe ama kwa kunyamazia au kwa kuazimia kuungana na ngurue pori (CCM) kula mabua kwa pamoja milithi ya Chama Cha Wananchi CUF ndoa ya kuchumia tumbo huko Visiwani.


(4) allocate some public works in people's localities from where the poor would earn something in terms of cash.

Ndio, miongoni mwa nji mbalimbali zilizopendekezwa na Benki ya Dunia (BD) ni pamoja na kupendekeza kwamba kukitokea kwamba barabara inajengwa kwenda Mtwara basi kila kiungo cha barabara hiyo wapewe wale Masikini wa Mwisho wa kipato katika jamii yetu.

Lengo kuu hapa ni kule kutafuta kuwafanya na wao Maskini wa kipato wanaopatikana katika eneo fulani ya barabara hiyo inakopita ndio washughulike kufanya zile kazi za mikono chini ya maelekezo na usimamizi ya wataalam ili kutokee mambo mawili makubwa; (1) taifa lipate barabara yenye kiwango cha lami kufungua zaidi uchumi wa nchi, pia nao (2) wanavijiji (si wana-CCM) wale ambao ni masikini wa kutupwa wa kipato nao wawe hawajapata tu barabara bali pia fedha za kupeleka watoto shule, kula yao, mavazi na makazi bora.


Hakika sura halisi ya hivi sasa nchini unasliti kabisa msingi huu ambao sasa imelazimika wenzetu wa ngozi nyeupe ndio waje wakatueleze ndio tupate kufanya. Nakumbu kipindi fulani Mzee Cheyo alipokua akizungumza hili, wakati ambapo bdo nilikua mwanafunzi wa sekondari tu pale Mwanza, kwa kuwa tulikua hatuelewi kwamba siku moja wazo lake lingeibukia Ulaya sisi letu lilikua ni kucheka hatuna mbavu kwa yale tulioona ni mzaha mkubwa mtu yeyote kuja KUTUJAZA MA-PESA mifuko yote kujaa.

Ama kweli hata naye Mtaalam haheshimiki kwao kama huyu Mzee Cheyo, British trained accountant na maono yake kwa Wa-Tanzania yalimwagwa mbali kabisa na yale ya akina Tambwe Hizza, Sheikh Yahaya, Lusinde wa Mtera na Mwigulu Nchemba kuonekana ya maana na kutiliwa maanane zaidi.

(5) 83 per cent of the poor are in rural areas but there are many poor people in non-poor areas.

Kwa hali ya ajabu sana ni kwamba BD miongoni mwetu Wa-Tanzania tulio masikini wa kutupwa wengi wetu tuko sehemu za vijijini.

Hawajaishia hapo tu, BD wanaongeza kwamba kwenye kundi hilo kubwa la watu masikini hohehahe ukiwapanga Wa-Tanzania hao masikini kwa mafungu ya watu kumi kumi basi utakuta kwamba katika kila Wa-Tanzania masikini hohehahe 8 kati yao wanaishi vijijini na kwamba wale masikini wa kutupwa 2 tu ndio wanahimili mikiki mikiki ya kuendelea kuganga njaa mijini huku wakitimuliwa vumbi bila huruma na walanchi wenye meno kwenye magari ya kifahari. Jamani sasa mtu akija kuuliza tena swali kwa nini sehemu za vijiji CCM huhonga pishi la ubwabwa tu na kupata kura karibu zote, siri yote ndio hiyo takwimu heshimiki walioumwaga hapa ndugu zetu wa Benki ya Dunia.

Hii inamaan kwamba miradi kibao hiyo ambayo iko njiani kuletwa Tanzania ikitekelezwa vizuri basi Gala la Kura kwa CCM vijijini nalo litakua limeteketea kwa kuwa ubwabwa, T-Sheti, kofia na vijisenti vitaakua si dili tena - tuko pamoja mpaaka hapo?


Mpaka hapo maelezo haya, ya taasisi hii inayoheshimika sana duniani, yanatuelekeza watu tupende kujua kwamba ni iddi gani hasa wanaozungumzi hapa wenzetu. Tazama hapo chini.

(6) over 6.4 million people live below the food poverty line

Watalaam hawa wa benki ya Dunia waanatuambia kwamba kati ya Wa-Tanzania milioni 48, milioni 6.5 wetu ni watu ambao hatuna hata uwezo wa kupata mlo mmoja kwa maana kwamba kipato chetu kwa siku ni chini ya Dola 1 ya ki-Marekani (yaani tunaishi kwa chini ya kipato cha Tsh 1,600 kwa mmoja katika familia anayejihangaisha wakati watu tunaomtegemea kipato hicho hicho si chini ya watu 10). na

(7) 10 million people are facing severe seasonal food insecurity

Mbali na wale watu milioni sita unusu masikini wale, BD inatufahamisha kwamba umasikini nchini umeongezeka kwa namna ambayo zaidi Wa-Tanzania zaidi ya milioni 10 kumi ni watu ambao ni kama Matonya ambao hata mahitaji ya msingi kama upatikanaji wa chakula kwao ni mgogoro mkubwa sana.

Kwa maana hii ni kwamba tunasema ya kwamba kati ya Wa-Tanzania wote kwa ujumla wetu milioni 48, wale wengine milioni 38 hawako salama hata kidogo kutokana na zaidi ya wenzetu milioni 10 ambao kila wakati upatikanaji wa chakula kwao ni kwa kubahatisha.

Pengine watafiti wetu wakichagua kwenda mbele zaidi huenda wakatueleza kwamba kati ya hawa Wa-Tanzania wenzetu wenye kukodolewa macho na hatari ya kutokua na uhakika na chakula katika nchi yenye rutuba na pana sana ka hili la kwetu, ni wangapi kati yao amba huenda watakua wamesukumwa katika michepuo ama ya (1) kuuza mwili ili chakula kipatikane, (2) ujambazi ili mkono uende kinywani, au na (3) mikopo isiorudishwa ilmradi 'bora lawama kuliko fedheha ya kufa' na baa la njaa.

Vile vile itakua muhimu wakatueleza kwamba ni (4) watoto wangapi wanaoachia ngazi kutafuta elimu kwa kuwa michango kibao inayohitajika ma-shuleni wazazi wanaonelea kwamba ni bora wale katika ujinga kuliko wafe wakipiga danadana ya elimu ambayo hata matunda yake mwisho wa siku ni kwa misingi ya kubagwana ... naamini watafiti wetu watatuletea majibu murua sana tu!!!


(8) 12.7million people are below the basic needs line.

Naam, Benki ya Dunia haikuishia tu kihivyo hapo juu. Wameenda mbali kidogo kutufunulia siri ambayo uongozi wa CCM siku zote ungependa kuuficha kwa kutumwagia takwimu kibao isioleta maana yoyote kwa maana ya mlo kwenye meza yetu nyumbani.

Kile wananchosema hawa waheshimiwa ni kwamba kama mtu uliona ajabu ya wale watu milioni 10 hapo juu bsi tangu leo ujue kwamba wewe unapokula mlo wa miraba mitatu na kumwaga kwenye pipa pale nyumbani, nguo ikipatawa tu na doa dogo tu unapigia deki na uhaywani mwingine kama huo basi ujue kwa kuna Wa-Tanzania zaidi ya milioni 13 ambao kama si aibu tu usoni tungepashwa kujimwaga pembeni mwa barabara kila mmoja kibakuli cha kutafutia msaada.

Misaada hii ingalikua ni kwa minajili ya kununulia mahitaji ya msingi sana kama vile nguo, na chakula kulala ni kwamba hadi hivi sasa tunalala kwenye viota vya vindege ambavyo vinatufanya tusiwe salama hata kidogo na binadamu wenzetu na hata wanyama wakali porini - tafakari mwenzangu haya si masimulizi ndio hali halisi huku ukisikia wengine kukukwapulia kodi yako.


(9) there are inclusion and exclusion errors

Kama utani vile, Benki ya Dunia kumbe nao wanayo taarifa kwamba hata kwa miradi michache tulionayo nchini naayo inaaelekezwa mahala kwa kufuata vigezo fulani visivyo rasmi na kujulikana kwa Wa-Tanzania wote.

Kwa mfano tu hapo juu ukiwauliza TASAF ni jinsi gani walifikia kugawa miradi michache hiyo ya Wa-Tanzania tunaoishi katika mikoa yote 26 na wao kupeleka mradi mmoja mkoa wa Dodoma na miwili iliobaki kwenda mkoa wa Pwani kwa maana ya Kibaha na Bagamoyo ... kero tupu!!!!!!!!

Sura kama hii inajulikana mahali pengi sana ikiwa ni pamoja na kupembuliwa wasio Wana-CCM kunyimwa baadhi ya huduma kama vile upatikanaji umeme, maji safi, mikopo benki, ajira serikalini (serikali ndiye mwajiri mkuu nchini mwetu), mikopo kwenda elimu ya juu, ufadhili kusoma Ughaibuni, kuganywa kwa miradi ya serikali na mambo kama hayo.

NB: Pindi unapomaliza kusoma tathmini hii ya Benki ya Dunia kama ambavyo nimejaribu kuisogeza jirani zaidi na uelewa wa wengi wakiwemo Bibie Ngonda, FaisaFoxy, Tropical, Omr, Malaria Sungu, Kishingo, Selemani na wengine wengi wa kundi hilo la kishabiki zaidi, kavute pumsi kubwa ndani na kisha upumue kwa nguvu huku ukimalizia hasira zako kwa kusema

TANGU SASA NATAMBUA WAZI KWA MABADILIKO YA KWELI TANZANIA YANAANZA NA MIMI NA NI JUKUMU LANGU WAKATI WOTE BILA KUSUKUMWA NA MTU, KUBEMBELEZWA WALA KURUHUSU KIWINGU CHA TOFAUTI ZA ITIKADI TU ZA KISIASA NA KI-DINI KUNITENGANISHA NA WATANZANIA WENZANGU KATIKA HARAKATI ZA KUTAFUTA HAKI NA USAWA KWA WOTE.

Mwisho.
 
Zawadi (Mwa)-Ngonda, karibu tutfakri kwa pamoja hii ripoti RAASMI ya Benki ya Dunia juu ya nchi yetu n wala si kutumia tu hisia kwenye mijada kama ulivyoonyesha tangu tukuone ulipojiunga hapa JF majuzi.
 
Naomba aje na data na atueleze mwelekeo wa serikali ya CCM na mwenyekiti wao ukoje juu ya Uzalendo na maendeleo ya Tanzania .Maana ka mwendo huu hakuna umoja na amani ambayo mnadhani imeletwa na CCM.Kisha aseme msimamo na mabilion kwa dowans .
 
Mr.Lunyungu you are not serious.
Haiwezekani unakuja na hoja nzito kama hii alafu unataka kuijadili na watu wasio serious.
Hili jambo linahitaji watu makini na wenye upeo mkubwa waje kulijadili.

Tumechoka matusi kil kukicha hakuna hoja ni Slaa , Mbowe , Chadema , Heche .Leo tupumzike wote kama watanzaia tujadili hili but nataka kwanza aanze Ngoda, Mbopo,Ritz,Mwita25,MS , Omr na wenzao wote akiwemo Nape .Tuukate mzizi hapa hapa ushabiki wa vyama ni ujinga na kutupumbaza tuache issue nyeti kama hizi .
 
Naunga mkono hoja mpaka hapo!!!!!!!

Tumechoka matusi kil kukicha hakuna hoja ni Slaa , Mbowe , Chadema , Heche .Leo tupumzike wote kama watanzaia tujadili hili but nataka kwanza aanze Ngoda, Mbopo,Ritz,Mwita25,MS , Omr na wenzao wote akiwemo Nape .Tuukate mzizi hapa hapa ushabiki wa vyama ni ujinga na kutupumbaza tuache issue nyeti kama hizi .
 
By ABDULWAKIL SAIBOKO, 18th October 2011 Daily News
THE World Bank has called for introduction of cash transfer to people
as poverty is on rise among individuals in Tanzania despite general
economic growth.
The WB's report issued on Tuesday with a title; 'Tanzania: Poverty,
growth and public transfers' noted that poverty in the country was
widely spread.
"The report proposes that for the country to have a sustainable
economic development, two options should be enforced, one of which is
cash transfer and another is public works", said the WB Lead Social
Protection Specialist, Ms Anush Bezhanyan.
Ms Bezhanyan observed that cash transfer involves giving cash to
individuals who are unable to work in which the government is supposed
to dictate modalities of expenditure and make a follow-up to get
feedbacks.
"The government can, for example, direct the beneficiaries of the cash
transfer to use the monies in taking their children to school, and
then a follow-up must be made to see whether the target has been
achieved," she said.
On public works, Ms Bezhanyan said the government was required to
allocate some public works in people's localities from where the poor
would earn something in terms of cash.
Citing examples, she said Ethiopia was one of the African countries
which could provide best practice on how the two modes could
effectively transform lives of individuals, hence, lead to overall
economical growth.
WB's Consultant, Mr Jim Smith said 83 per cent of the poor are in
rural areas but there are many poor people in non-poor areas.
"Targeting specific areas basing on geographical locations is not
proper, the report shows that poverty in the country was evenly
spread," he said.
The report also shows that over 6.4 million people live below the food
poverty line, some 10 million people are facing severe seasonal food
insecurity and about 12.7million people are below the basic needs
line.
According to the report, the existing projects on poverty reduction
have a limited coverage which is less than one per cent of the poor
and there are inclusion and exclusion errors due to generalization
approach.
It suggests that "the government should move towards a single national
programme large enough to cover the country and big enough to make a
difference".
The Tanzania Social Action Fund (TASAF) System Manager, Mr Ladislaus
Mwamanga, said the fund has already started working on some of the WB
report's recommendations.
"We have already started cash transfer as a pilot project in three
districts whereby some 10 US dollars are disbursed to every household
per month," he said.
He said that the pilot project which began in 2008 covers Bagamoyo,
Kibaha and Chamwino districts in Cost and Dodoma regions respectively.
"Already 200 households have benefited and the project has already
received some 1.9 million USD from Japan Social Development Fund and
4.5 million USD from WB to support the project's implementation", he
said.
Nape mwenyewe BBC haipandi, sembuse FF na Rejao? Akiwa jukwaani atasema hata WB wametusifia kwa kukuza uchumi - CCM Oyee . Kazi kweli kweli.
 
Nimeona Mwita 25 yuko hapa na Omr mbona hawagusi hapa ?Au wao ni trivio issues ndiyo wanakomaa nazo ? Unazi bwana .
 
hawawezi tokea. Hayo ma-mtu ukitaka yajibu kitu basi mtaje Slaa
Ukimtaja tu Dr. Slaa utayaona makina Fox yakikurupuka hata bila ya Chup** wala bila hata kuvaa hijab utadhani yamefumaniwa na kuja kutoa Utumbo wao hapa.
 
Tuwangoje waje hapa tukate issue waache pumba zao si kila mtu ni mjinga .Angalau with serious issues pumba hupungua hapa jamvini kama sasa .
 
Uwapo Kanda ya Ziwa kuna kabila linalotumia neno "Ngoda" kumaanisha mtu asiyesikia kabisaa! Naona wakuu wangu kama mnapoteza nguvu bure.
 
Mbona huyu mamluki hatokei tena? Kwa kweli bado tuna tatizo kubwa la uelewa miongoni mwa watanzania.
 
Lowassa itishe vyombo vya habari kwa ajili tu ya kumuomba rafiki ya msamaha kuhusu vimbwanga vya kundi lake Arusha badla ya kutuambi kwa Dowansi ni kitu gani.

Jamani mwa-CCM aliyeokoka na ufisadi ni yule aliyekufa, yule ambaye yu hai hata akijificha kwake kwa zaidi ya mwka siku akiibuka mnuko wa maneno yake ni pale pale.

Ndio maana wale wenzao wote akina rejao, selemani, faizafoxy, mwitaccm wote wamekimbia jamvi.
 
Ingekuwa ishu ya DC mfuga nguruwe kudhibitiwa asifanye uhalifu wa kisiasa wangeshambulia jukwaa kama viwavi jeshi.
 
Tumechoka matusi kil kukicha hakuna hoja ni Slaa , Mbowe , Chadema , Heche .Leo tupumzike wote kama watanzaia tujadili hili but nataka kwanza aanze Ngoda, Mbopo,Ritz,Mwita25,MS , Omr na wenzao wote akiwemo Nape .Tuukate mzizi hapa hapa ushabiki wa vyama ni ujinga na kutupumbaza tuache issue nyeti kama hizi .

Pole Lunyungu, naona walengwa wako wameingia mitini. Tutaendelea kuwabana tu kwa hoja zenye akili, hawana pa kuchomokea. Hii nchi ni yetu sote! Nukta
 
By ABDULWAKIL SAIBOKO, 18th October 2011 Daily News
The report also shows that over 6.4 million people live below the food
poverty line, some 10 million people are facing severe seasonal food
insecurity and about 12.7million people are below the basic needs
line.
According to the report, the existing projects on poverty reduction
have a limited coverage which is less than one per cent of the poor
and there are inclusion and exclusion errors due to generalization
approach.

I don't think the government in power has concrete plans to reduce poverty because they are banking on it (poverty) to win elections and remain in power.
 
Hapa hawawezi kutokea na zipo sababu, moja ni kuwa wanafaidika na mfumo unaotufanya tuishi katika umaskini na utashangaa wakijisfu kwa 'kupandisha uchumi', nadhani itabidi nipate maana nyingine ya kupanda kwa uchumi Tz, kama sasa sukari mama ntilie wanakorogea kabisa ili kutubana tunaoweka vijiko viwili kwenye kikombe, unga nao uko juu balaa, mafuta ya taa yamekuwa kama umeme kijijini.

Tunajisifu na kupokea tuzo za kijinga kabisa, fikiria tuzo ya iliyopotoshwa kwa makusudi na tbc, habari leo, tuzo hii alipokea rais kupongezwa kwa kuandikisha wanafunzi wengi shuleni ilhali ukweli ni kuwa kuna vijana wanaingia sekondari hawajui kusoma na kuandika. takwimu rasmi za serikal 2009 wizara ya elimu inasema 30% ya watz hawajuo kusoma na kwa mtihani wa mwaka jana pekee, 88% ya waliomaliza kidato cha nne walipata daraja la nne na sifuri huku daraja sifuri likitengeneza 68%
 
Ukimtaja tu Dr. Slaa utayaona makina Fox yakikurupuka hata bila ya Chup** wala bila hata kuvaa hijab utadhani yamefumaniwa na kuja kutoa Utumbo wao hapa.
Jumbe limefiki lakini kwa staili ya kuchekesha kweli. teh teh tehhhhhhhhhhhhhhhh
 

Pole Lunyungu, naona walengwa wako wameingia mitini. Tutaendelea kuwabana tu kwa hoja zenye akili, hawana pa kuchomokea. Hii nchi ni yetu sote! Nukta
Siyo kwamba wameamua kuwa 'guests' kwani naona 'members' kwa sasa ni wachache kuliko guests. Huku ni kama Petro alivyokuwa akifuatilia toka yesu alivyokamatwa mpaka alipomkana.

There are currently 33 users browsing this thread. (7 members and 26 guests)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom