Zawadi kwa maharusi

Zawadi kwa maharusi

CharmingLady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
18,304
Reaction score
12,999
Habari za mchana wa leo wanajamvi.....

Katika utamaduni wetu Watanzania tumezoea kupeleka zawadi mbalimbali kwa maharusi, zawadi hizo zinaweza kuwa ni pesa au vitu vya thamani. Ila kuna uvumi umeenea kuwa kuna watu ambao huwa wana nia mbaya na maharusi na kuishia kuweka vitu vya ajabu katika mabox mazuri kisha kuyafunga na gift papers safi na kuwapatia maharusi.

Mara baada ya maharusi hao kufungua zawadi na kukuta vitu vya ajabu wamekuwa wakidhurika na vitu hivyo, nafikiri wengi wetu tumewahi kushuhudia ama kusikia jambo hili. Na hii imesababisha maharusi wengine kutaka zawadi zote zifunguliwe toka katika gift papers na ZIWEKWE WAZI ili kuepuka madhila haya!

Nimewahi kushuhudia wanandoa flani wakifungua zawadi katika bahasha, cha ajabu waliambulia Sh. 20. Ile ya rangi ya Silver, sijui kama bado zipo au lah. Walijiuliza sana kuwa mtoa zawadi hiyo alikuwa na lengo gani???? Ila Mungu ni mwema hawakudhurika iwapo mtoaji alikuwa na lengo baya.

Kwa imani zetu tofatui tofauti hebu tujadili ni jinsi gani ya kuepuka mambo kama haya yasitokee katika jamii zetu, Inaweza kuwa ni wewe, ndugu yako ama rafiki yako anaweza kukutana na hii changamoto una ushauri gani kwake........ KWa wale waliokumbana na haya madhila walichukua hatua gani??? Tupe Uzoefu wako..........

KARIBUNI KWA MJADALA
 
dawa ni kufunga harusi then mnapitiliza fungate,bila kusubiri zawadi za watu lakini kama unategemea zawadi kutoka kwa watu ili kupunguza bajeti ya kununua vitu hilo haliepukiki.
 
dawa ni kufunga harusi then mnapitiliza fungate,bila kusubiri zawadi za watu lakini kama unategemea zawadi kutoka kwa watu ili kupunguza bajeti ya kununua vitu hilo haliepukiki.
cha msingi ni kuziombea tu.nan hapendi zawadi?hata obama anapokea zawadi au wewe nimambo safi?
au ww ni mtoto wa billgate.ndo shida yenu wabongo.......loading error..........
 
Maombi ya namna hii ndiyo kiboko hawatii hata mguu,mimi hawakujaribu..."Bwana wa Majeshi muumba Mbinguni na Nchi kambariki kila atakaye toa zawadi, na mkono wako ukawe juu ya wenye hila ukawalipe uovu wao kichwani mwao mpaka kizazi cha nne katika jina la Yesu Kristo wa Nazarethi ameni"
 
Hapo inabidi MC awe na full Upako wa kukemea..... Ila kuna watu wa ujasiri wa KIFISADI wanaenda tu kupeleka zawadi zao za ajabu! Kwani hujawahi kusikia mchawi anakwenda kuroga kanisani??
 
Hakuna cha mambo Safi wala nn,huu ni majadala wa wazi ww unaesema tatizo la wabongo mi nahisi ww ndo una matatizo.
 
hizi zawadi hizi
kuna mdada alipewa zawadi ikiwa imefungwa kwenye box zuri kabisa
alivoenda kufungua akakuta pedi zilizotumika..na yai
 
hizi zawadi hizi
kuna mdada alipewa zawadi ikiwa imefungwa kwenye box zuri kabisa
alivoenda kufungua akakuta pedi zilizotumika..na yai

kwenye harusi yenu wewe na Mentor tuwaletee zawadi gani?
 
Last edited by a moderator:
Bora sisi Wachagga zawadi zetu unapewa full mjengo na mzazi/wazazi...siku ya harusi unakabidhiwa hati ya nyumba kwa mbwembwe nyingi...

Ninyi mnaosubiria zile za kwenye maboksi subirini kutiliwa unga wa kimeta huko...
 
cha msingi ni kuziombea tu.nan hapendi zawadi?hata obama anapokea zawadi au wewe nimambo safi?
au ww ni mtoto wa billgate.ndo shida yenu wabongo.......loading error..........

Tatizo siku hizi vijana wanafunga harusi ili wapate Zawadi, hawana lengo jingine.!
 
mkuu tunao amini katika maandiko yanasema moyo ukiharibika hata utiwe nini hauwezi badilika! mtu akiamua kufanya uovu/ubaya huwezi mzuia ila biblia inapigilia mstari wa mwisho kwa kusema laana isiyo na sababu haimpati mtu! hivyo maharusi kama hawana shida, ugomvi, bifu na mtu hawana cha kuhofu.
 
Bora sisi Wachagga zawadi zetu unapewa full mjengo na mzazi/wazazi...siku ya harusi unakabidhiwa hati ya nyumba kwa mbwembwe nyingi...

Ninyi mnaosubiria zile za kwenye maboksi subirini kutiliwa unga wa kimeta huko...

ah ah ah ah ila usisahau kuiweka wakfu hiyo nyumba maana wazazi wengine wameshaichinjia mbuzi na mazindiko!!
 
Back
Top Bottom