Zawadi hizi zirudishwe?

Mh!!! Mi nionavyo kwa waswahili wengi haya mambo ya zawadi huwa kama kifungamanisho fulani katika mahusiano ya watu, kwa maana kuwa kama jamaa anampatia zawadi demu wake anaamini kuwa hiyo inamfunga mwanamke kuwa naye ikitokea demu akabadilika kwa sababu moja au nyingine wengi hukimbilia kuchua zawadi zao.Nimewahi kushuhudia jamaa akikusanya zawadi alizompa demu wake sofa, TV na simu ya mkononi hii pia hutokea hata kwa baadhi ya akina dada wanaotoa zawadi kwa wapenzi wao inapotokea kutofautiana hukimbilia kuchukua zawadi zao kwa kisingizio kuwa hawezi kukubali kuona mtu aliyemghalimikia anatumia zawadi hizo na mtu mwingine...

So yawezekana watu hawaelewei nini maana ya zawadi kwa mpenzi...wanatakiwa kupewa darasa!!!

Huu ni ukweli mtupu! ni kukosa ustaarabu kudai kitu ambacho ulikitoa kwa moyo bila kulazimishwa.Watu wengine wamejikuta wakipata matatizo kisa ni zawadi zimewaponza.Kuna wanaume wamebaka na kujitetea ati wanadai haki yao baada ya kutoa takrima au zawadi.Huu si utetezi na ndiyo maana wahusika wamejikuta wakiishia pabaya.Lakini hebu pia tujiulize, katika mila za kiafrika, je kupeana zawaidi baina ya watu wa jinsi tofauti ni kitu kilikuwapo au tumeiga utamaduni wa kigeni bila kuelewa maana? Kama zawadi zilikuwepo zilimaanisha nini na je zilidaiwa au kurudishwa? Nijuavyo mimi kwa mila na desturi za makabila mbalimbali, zawadi zilitolewa kama kutaka uchumba na zilipopokelewa ilimaanisha kukubaliwa.Vinginevyo zilikataliwa.Na kama zilikubaliwa na kukubali uchumba basi uchumba ulipovunjika na zawaidi zilirudishwa. Lakini kisasa zawadi hazimaanishi uchumba.
Naweza kusahihishwa kama nimekosea.

Darasa kidogo kwa utoaji na upokeaji zawaida katika mazingira ya kisasa:-
Wote mtoaji na mpokeaji wajilaumu inapofikia hatua ya kudai/kudaiwa zawadi.Epuka kujilaumu kwa kuzingatia yafuatayo:
Mtoaji awe mwanaume au mwanamke kama unatoa zawadi kama kivutio/chambo ujue unacheza pata potea.Unaweza kupata au ukakosa na hivyo ujiandae kwa matokeo.Iwapo unatoa kwa maana hiyo basi weka wazi kuwa nitakudai endapo matarajio hayatafikiwa.( Na matarajio hayo uyaweke wazi uone kama hujakimbiwa kama mtu mwenye ukoma!).Wenye roho ndogo epukeni kutoa zawadi zenye thamani kubwa sana au za kudumu kama nyumba, magari n.k.Toeni perfume na vipodozi, simu za kiganjani, maua,offer za sinema, dinner,drinks, trips za majuu na ndani ya nchi n.k.Lol!
Mpokeaji - uliza kabla ya kupokea je hii zawaidi ina maana gani? jibu utakalopewa basi litakufanya upokee au ukatae kama utaona ina masharti.
 
Kama mkataba ni kurudishiana zawadi, basi hata zile zilizobakia ndani ya.... nazo achukue asiache,,,, ooops! sorry

Na ni kitu ambacho hakiwezekani..ndo maana mi siamini sana katika mapenzi ambayo yamejengwa katika misingi ya vitu badala ya utu.....utu kwanza, vitu baadaye.....
 
Na ni kitu ambacho hakiwezekani..ndo maana mi siamini sana katika mapenzi ambayo yamejengwa katika misingi ya vitu badala ya utu.....utu kwanza, vitu baadaye.....

Mapenzi ya sasa yamejengwa zaidi katika zawadi. Usipomnunulia mpenzi wako zawadi, mpenzi wako anakuwa na negative thoughts kuwa humpendi. Huwa kun imani kuwa unapomnunulia mpenzi wako zawadi ndivyo anavyokuthamini. Na ukisha jenga hii dhana ya zawadi mara kwa mara, ikatokea kipindi fulani umekaa sana bila kumpa zawadi basi huamini kuwa una mwingine.
Wengi niliowauliza wanaamini maisha haya ya zawadi zaidi kuliko utu. Watu wa miaka ya nyuma wa hawakuwa hivi. Hi ni kwa sababu ya ushindani wa hali ya kimaisha yanayotuzunguka. Mathalani, kijana hatathubutu kumkaribisha ndani kwake msichana wake kama hajakamilika ndani, likewise. kwa hiyo kuna imani kuwa vitu kwanza, utu baadaye!
 
the normative way ni kuwa haikupaswa kuwa hivo, sasa hivi kama unavosema naona individual rationality imekomaa kiasi cha kuerode kabisa 'ethics' za mapenzi

Na uzee huu,, nashukuru sijampata wa hivyo tulicho nacho tunaridhika.

ifike mahali kama ni kufanya jambo la maendeleo kama kustock chumba basi isiwe ni kumuimpress mtu bali ichukuliwe kama personal development

kwani hisi fursa sawa kwa wote zinakuwaje wajameni na je wanawake pia wanatoa zawadi kwa wapenzi wao wa kiume kwa kiwango hicho hicho wanachopewa?
 
Ndiyo! hata wanawake wanahonga, tena mbaya kabisa, wengine wanasafiri mbali sana kuwafuta wapendwa wao. Niliwahi kusema kuwa huwa hawa uvumilivu mkubwa kama wanaume, ni lazima wadai zawadi walizokununulia.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom