Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,976
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ilinusurika majaribio 14 ya kupinduliwa, likiwamo lililosababisha kifo cha muasisi wa Mapinduzi, Sheikh Abeid Amaan Karume, Aprili 7, 1972.
Kwa mujibu wa wazee waliokuwapo wakati wa kuasisiwa kwa Muungano, majaribio hayo yalishindikana na mmoja wa wazee hao, aliyewahi kuwa Katibu wa Kwanza wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Afro Shiraz, Baraka Mohamed Shamte alisema kama si Muungano, baadhi ya majaribio hayo yangefanikiwa na kungeendelea kutokea mapinduzi zaidi ya mara sita.
Kama isingekuwa Muungano, tungepinduana zaidi ya mara sita, alisema Shamte ambaye pia ni mtoto wa marehemu Muhammad Shamte, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Zanzibar iliyopinduliwa.
Alifafanua kuwa wafuasi wa utawala uliopinduliwa uliokuwa chini ya Sultan ambao walikuwa ndani na nje ya Zanzibar, ndio waliofanya majaribio hayo 14 katika kipindi kifupi cha kati ya mwaka 1964 na 1972.
Kwa habari zaidi soma HabariLeo.