Zanzibar yagoma kulipa Sh40 bilioni TANESCO

fangfangjt

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
571
139
Zanzibar yagoma kulipa Sh40 bilioni Tanesco


Salma Said, Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imekataa kulipa deni la umeme la Sh 40 bilioni kwa TANESCO baada ya kupandishiwa kiwango.Waziri wa Ardhi, Maji, Makazi na Nishati wa Zanzibar , Ali Juma Shamuhuma alisema baada ya kiwango kuongezeka, serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatakiwa kulipa kwa asilimia 168 badala ya asilimia 21 kwa uniti.

Shamhuna alikuwa akichangia katika majumuisho ya mjadala juu ya ripoti ya Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambapo Shamuhuna alisema, “hatukubali kulipa deni la Sh 40 bilioni kwa kiwango cha asilimia 168 asilani.”

Tanesco ilipandisha viwango vya malipo kwa wateja wake tangu mwaka jana kwa asilimia 21, kwa upande wa Tanzania bara ambapo kwa Zanzibar shirika hilo la umeme limepandishwa kwa asilimia 168 na kusababisha malalamiko makubwakutoka kwa wateja.Shamhuna alisema kuendelea kwa Tanesco kudai deni hilo kunakwenda kinyume na agizo la Rais Jakaya Kikwete kwamba pande zote mbili za Muungano zilipe viwango sawa vya asilimia 21.

Waziri huyo ambaye alikuwa akichangia na kupigiwa makofi na wajumbe wengine alisema ili kuepukana na utegemezi wa umeme kutoka Tanesco ambao unaigharimu SMZ fedha nyingi, serikali umeanza kuchukua hatua za kuzungumza na wawekezaji wazoefu ili kuzalisha umeme kutokana na jua na gesi utakaojitegemea.

Shamhuna aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba mradi kama huu umefanikiwa Dubai na Malaysia unaweza kuzalisha kati ya Megawati 50 na 100 ambao unatosheleza mahitaji ya sasa ya Zanzibar ya Megawati 50.



Hata hivyo, akizungumzia kuhusu madai ya baadhi ya Wajumbe wa baraza la Wawakilishi wanaotaka Zanzibar izalishe umeme kwa kutumia mawimbi ya bahari, Shamhuna alisema utafiti unaonyesha kuwa ni mradi mkubwa wenye gharama kubwa na pia haujafanikiwa katika nchi nyingi duniani.

wakichangia mjadala huo wajumbe wengine wa baraza hilo wamesema suala hilo linahitaji kuangalia vyema na serikali ya muungano kwani haiwezekani serikali hiyo kukaa kimya na baadhi yao kutaka fedha hizo kutolipwa kwani haitowezekana.
 
Zanzibar ni nchi jirani kama hawataki kulipa TANESCO iwakatie tu umeme, mbona Tanganyika tumenunua umeme kutoka Zambia na tunalipa????
 
Hata kama wakikubali kulipa hela itatoka bara.............maana wao hawana hela asilani....yaleyale
 
hii nchi ya ajabu sana, DOWANS wamedai TANESCO wakataka kulipa haraka sana, sasa hivi SMZ inadaiwa na TANESCO hata kulipa hawataki mnategemea shirika mtaendesha vipi? basi acheni kulipa wafanyakazi wa TANESCO pamoja na wakurugenzi wake, lasivyo pesa yote itatoka kwenye mifuko ya wananchi moja kwa moja kulipia madeni ya watu wengine......na cha ajabu unakuta kuna vigogo hapa hapa bara tena wengi hawajalipa bill zao za umeme kwa miaka mingi tu lakini hakuna wakuthubuti kwenda kukata umeme huko!
 
akaaa! mie sijaona mdaiwa analeta jeuri kama hao.. dawa ni moja tu KATA UMEME
 
Nakumbuka kipindi management ya makaburu walipokuwa wanaendesha TANESCO Zanzibar walikuwa wakilipa bila zengwe mambo ya siasa yaliwekwa pembeni kabisa nashangaa sana nchi yenye Rais,wimbo wa taifa,jeshi na nk haina uwezo wa kulipa umeme wanakataa kwa jeuri kisa muungano bora katiba mpya ije mambo ya kipuuzi kama haya yakomeshwe kabisa.
 
Back
Top Bottom