Baada ya Kuufyata sasa afyetuka baada ya kuzomewa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeshauriwa kuwa na uraia kwa watu wake pamoja na kuvipa hadhi vikosi vyake maalumu ili viweze kumiliki silaha za kivita chini ya mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
wakati umefika kwa vikosi vya SMZ kupewa hadhi ya kumiliki silaha za kivita badala ya kumiliki silaha za kawaida kama ilivyo sasa kwa mujibu wa sheria.
ni wakati mwafaka na unaofaa kwa SMZ kununua silaha kama mizinga, vifaru, helikopta za kivita na boti za kijeshi pamoja na silaha nzito kama RPG.
Huwezi kuwa na nchi bila ya kuwa na raia. Alitaka Wazanzibari kupewa uraia wao katika mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kusema ni jambo la kushangaza Wazanzibari kuitwa wakazi na si raia.
hatua ambayo itaipa hadhi nchi na kutambulika kitaifa na kimataifa.
Mkuu Mwiba, asante kwa hii!.
Maadam hayo ni maoni tuu ya Wawakilishi, yataendelea kubaki ni maoni tuu!.
Maadamu wamezungumzia kwa mujibu wa sheria!, nashauri anzeni na sheria kwanza ndipo utekelezaji ufuate!.
Kwa mujibu wa sheria, Jeshi ni la JMT!, hao wa huko Zanzibar ni vikosi tuu kama migambo au Ultlmate security, mwisho wa uwezo wao kisheria ni kumili silaka ndogo za kujilinda na sio silaha za vita!. Kama mnataka kuvibadili vikosi vigeuke jeshi, anzeni na kuibadili sheria kuwa Zanzibar nayo iwe na jeshi lake!.
Vivyo hivyo kwenye uraia, uraia bi wa Nchi, JMT!, huko Zanzibar ni ukaazi tuu!. Maadam Mwakilishi katamka vizuri, "huwezi kuwa na nchi bila kuywa na raia!", Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT hivyo haiwezi kuwa na raia wake!, raia wote ni wa JMT!, ili Zanzibar iweze kuwa na raia wake, inabisi kwanza iwe nchi!m ndipo ipate raia lakini sivyo kama ilivyo sasa ni "nchi jina tuu!" lakini sii nchi lolote!, sii nchi chochote!, ila kama shida yenu ni jina tuu!, then naiwe!, kitambulisho cha ukaazi wa Zanzibar kiitwe "Kitambulisho cha Raia Wa Nchi ya Zanzibar!", kama tulivyokupeni bendera si mnapeperusha!, na wimbo wa taifa si mnapiga!, kujiita raia wa Zanzibar ruksa, ila vifaru, RPG, mizinga ya kujiandaa kupigana vita na nani?.
Enyi waume mnaomiliki silaha!, inapotokea mkeo nae anaomba na yeye amiliki silaha! na nyite mlale nazo chini ya mito kuna usalama kweli hapo?!.
Mke kazi yake ni kula bure, kulala bure, kuvishwa, kupendezeshwa, umeme bure!, mishahara bure na asilimia 4.5 % ya misaada yote bure na nimesikia sasa ajira ni asilimia 21!%, Mungu akupe nini tena!.
Hongereni!.
Pasco