Zanzibar strikes again !

Zanzibar strikes again !

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,764
[h=1]Baada ya Kuufyata sasa afyetuka baada ya kuzomewa[/h]
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeshauriwa kuwa na uraia kwa watu wake pamoja na kuvipa hadhi vikosi vyake maalumu ili viweze kumiliki silaha za kivita chini ya mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Ushauri huo ulitolewa jana na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakati wakichangia makadirio na matumizi ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Vikosi Maalumu iliyowasilishwa na Waziri wake, Haji Omar Kheir, Chukwani mjini Unguja jana.

Akichangia bajeti hiyo, Mwakilishi wa Koani, Mussa Ali Hassan alisema wakati umefika kwa vikosi vya SMZ kupewa hadhi ya kumiliki silaha za kivita badala ya kumiliki silaha za kawaida kama ilivyo sasa kwa mujibu wa sheria.
Hassan alisema kuna vikosi vya SMZ ambavyo havina tofauti na askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), ambavyo vilishiriki kupambana na majeshi ya Idd Amini yalipovamia Tanzania mwaka 1978.
Alisema ni wakati mwafaka na unaofaa kwa SMZ kununua silaha kama mizinga, vifaru, helikopta za kivita na boti za kijeshi pamoja na silaha nzito kama RPG.

Wajumbe wengine, Amina Idd Mabrouk (Viti Maalumu), Jaku Hashim Ayoub(Muyuni), Raha Suleiman (Viti Maalumu), waliitaka Serikali kuangalia masilahi ya askari wa vikosi vya SMZ ikiwamo kuwapatia vitendea kazi pamoja na kuwajengea makazi bora.

Wawakilishi hao kwa nyakati tofauti walidai kuwa nyumba nyingi za makazi ya askari ni chakavu na hazistahili kukaliwa na askari ambao wanalinda nchi huku wananchi na viongozi wakiishi kwenye makazi bora.

Pia waliitaka SMZ kutambua umuhimu wa kuwalipa posho na marupurupu stahiki kwa muda wa kazi wa ziada askari wa vikosi vya SMZ pamoja na kuwaingiza katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF).

Akizungumzia uraia, Mwakilishi wa Chambani, Mohamed Mbwana Hamad alisema: “Huwezi kuwa na nchi bila ya kuwa na raia.” Alitaka Wazanzibari kupewa uraia wao katika mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kusema ni jambo la kushangaza Wazanzibari kuitwa wakazi na si raia.

Alisema Wazanzibari wote wanatakiwa kupewa hadhi ya uraia na wageni ndiyo wanaostahili kuwa na vitambulisho vya ukaazi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, hatua ambayo itaipa hadhi nchi na kutambulika kitaifa na kimataifa.
 
very serious niliwahi waambia watu kuwepo kwa makomandoo wa zenj wanaofanya kazi zenj ..ni shida kwa wawekezaji na raia sasa....ujambazi na matendo mengine ila wakiota pembe wataiface bara....sasa hao wawakilishi wanapima maji kwanza ..ikiwa mbaya waambiwe wameteleza..halafu raia waanze kelele nyingi za kutaka uhuru...Taratibu serikali ya waziri wa mambo ya nje JK wakizidi wapa uhuru.
 
Ni hatari sana Zanzibar ni nchi lakini wananchi wake sio raia ni wakaazi tu, Kuna haja Zanzibar kufanya Mapinduzi makubwa sana kujivua kutoka kwa watanganyika kwa nguvu zote ata kama hawatak. Ni aibu miaka 50 toka uhuru wazanzibar siyo raia ndani ya nchi yao
 
Zanzibar ni nchi na raia wake wanaitwa wazanzibar wakaazi, haa haaa! Wanadai vikosi vyenye silaha nzito wakati hata wizara ya mambo ya nje wanategemea dar!
 
Znzbar komaeni kuwa huru,nasisi huku tunalia na Tanganyika yetu na itapatkana tu.
 
wakati wa mkapa hakukuwA na uasi kutoka zanzibar isipokuwa awamu ya sheikh jakaya kikwete.....
 
Ukishajua, then ...! Jadili hoja suala la vyama halina mantiki kwenye hii hoja

Hata mimi nilitaka kujua ni wa vyama gani? Lakini kuna mdau kasema wa ccm apa. Ni muhimu kujua, hoja itajadiliwa vizuri sasa. Kama ni wa ccm, hawa jamaa, ni WANAFIK, tena sana, babu Ali sheni anatakiwa awakemee mbwa wenzake, vipi wanadai uraia wa wazanzibari wakati wakifika dodoma wanakuwa wameolewa? Vipi wanataka Zanzibar iwe na vifaa vyake vya ulinzi ikiwa wakifika dodoma hawataki zanzibar iwe huru? Makhanatha wakubwa hawa...
 
Jamani msiumane meno, endeleeni na mjadala mi naenda zangu kulala.
 
Kuchangia bajeti hawawezi wataweza kununua hata short gun moja?

Kuna kitu nyuma ya zanzibar hatujajua
 
Hata mimi nilitaka kujua ni wa vyama gani? Lakini kuna mdau kasema wa ccm apa. Ni muhimu kujua, hoja itajadiliwa vizuri sasa. Kama ni wa ccm, hawa jamaa, ni WANAFIK, tena sana, babu Ali sheni anatakiwa awakemee mbwa wenzake, vipi wanadai uraia wa wazanzibari wakati wakifika dodoma wanakuwa wameolewa? Vipi wanataka Zanzibar iwe na vifaa vyake vya ulinzi ikiwa wakifika dodoma hawataki zanzibar iwe huru? Makhanatha wakubwa hawa...

Duh! Hapo umekwenda mbali. Rais unamwita mbwa!!.

Sent from my GT-I9192 using Tapatalk
 
Haya kuna ile hadithi ya punda aliyetaka kwenda njia mbili,akaishia kufa.Sasa sijui hawa wenzetu wanataka nini?Wakija bara serikali mbili,wakiondoka serikali tatu.Mh!:shock:😕
 
Back
Top Bottom