figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,474
- 54,801
Maazimisho yatafanyika Golden Tulip Airport Hotel Zanzibar kuanzi tarehe 05 hadi 06 Novemba 2021 siku ya Ijumaa na Jumamosi.
Je, rais Samia ni rais wa Wote?
Maalim Seif alifariki dunia saa tano asubuhi 17.02.2021 akiwa katika Taasisi ya Magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa kwa takribani wiki mbili.
Maalim Seif alifariki dunia akiwa ametumikia wadhifa wa makamu wa kwanza wa rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa chini ya siku 100 - akiwa sehemu ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyoundwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa mwaka 2020.
Kabla ya kifo chake, katika hatua isiyo ya kawaida, chama chake cha ACT Wazalendo kilitoa taarifa kwa vyombo vya habari iliyoeleza kwamba Maalim na baadhi ya wasaidizi wake na watu ndani ya familia yake walipata maambukizi ya ugonjwa wa korona.
Maalim Seif Sharif Hamad, mbali na kuwa Makamu wa kwanza wa Rais visiwani Zanzibar pia alikuwa mwenyekiti wa chama cha kisiasa cha ACT Wazalendo na gwiji katika maswala ya kutetea demokrasia nchini Tanzania.
Zaidi, soma; TANZIA - Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad afariki dunia