Zanzibar: Rais Mwinyi awaaambia raia wavumilie anapoenda kuchukua maamuzi magumu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amewataka wananchi wavumilie anapokwenda kuchukua maamuzi magumu ili kukomesha ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma Zanzibar

Amesema hayo eleza hayo alipokuwa akitoa shukrani kwa viongozi wa CCM na jumuiya zake pamoja na wazee na mabalozi wa chama hicho. Amesema katika maendeleo ya watu hatokuwa na utani

Aidha ametaja kuwa kwa takriban mwezi mmoja aliokuwa madarakani, kila sehemu akigusa kuna harufu ya ufisadi kwa hiyo hatoangalia kama huyu ni mtoto wa fulani, ndugu wa fulani atakapoamua

Katika maamuzi magumu atakayochukua, hatafukua makaburi wala kumtafuta mchawi baada ya maamuzi hayo kila senti ya fedha za umma itaheshimiwa

 
Anawashukuru hao viongozi wa CCM kwa kazi gani ya maana waliyoifanya?

Ok, itakuwa ile ya kumtongoza Seif na viongozi wenzake wa ACT mpaka wakakubali kujiunga SUK licha ya viboko walivyowatandika kwa kutumia majeshi.
 
Anawashukuru hao viongozi wa CCM kwa kazi gani ya maana waliyoifanya?

Ok, itakuwa ile ya kumtongoza Seif na viongozi wenzake wa ACT mpaka wakakubali kujiunga SUK licha ya viboko walivyowatandika kwa kutumia majeshi.
Mtoto mdogo umejaa chuki hivyo ukizeeka utakua mchawi
 
Atukane upinzani tu mnashangilia.

Akiponda wa chama kilekile mwasema kana kwamba anamtukana raisi.

Mimi naona husomeki
Sisomeki au wewe hujui kusoma?

Rais kimsingi kasema kwa mwezi mmoja kaona kila sehemu imejaa ufisadi.

Maana yake rais aliyepita hakufanya kazi yake kudhibiti ufisadi, alizembea.

Usichoelewa nini hapo?

Unataka kucholewa picha?
 
Najiuliza hivi serikali iliyokuwepo ilikuwa ya chama gani?
Huwa wanajisahaulisha na wanadhani watz wote wanaishi kwa "za kuambiwa!!" Nikikumbuka yale maneno yaliyosemwa mikoa yote... "inhiii... mkoa huu naupenda kuliko mikoa yote!!" Na bado watu wakaamini kuwa mkoa wao ni pendwa kuliko mingine yote daaah sisi hawa!!!
 
nasema haa maskan kwetu tupo pamoja.majengo yote ya kihistoria yakarabatiwe yawe open to the public itaongeza tourist destination.
 
Back
Top Bottom