WASEMAVYO WA-TANGANYIKA JUU YA ZANZIBAR
Kufuatia habari hii ambayo imo humu.
Zanzibar Kuwa Nchi
Na Hassan Shaaban, Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inafanya marekebisho ya katiba ya mwaka 1984, ambayo yanaipa Zanzibar hadhi kamili kama nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano.
MAONI YAO WA-TANGANYIKA
Suala la kuwa Z'bar ni nchi au kinyume chake liliwahi kuzungumziwa na mahkama ya Rufaa katika kesi ya Jamhuri dhidi ya Said Machano na Wengine 14, [1994] na iliamuliwa kuwa ZANZIBAR SI NCHI. Kesi hii ilikuwa inahusisha jamaa walioripotiwa kujaribu bila mafanikio kupindua serikali (felonious treason). Kuna mambo ambayo ni lazima yawepo ili treason itokee, ikiwa ni pamoja na serikali inayohusishwa kuwa na mamlaka ya kuendesha NCHI. Kwa kuwa Zanzibar [...]Endelea hapa
"WASEMAVYO WA-TANGANYIKA JUU YA ZANZIBAR"
Agosti 10, 2010 | Gawanyo
Habari |
2 maoni
Mabadiliko ya Katiba Yapita kwa Sauti Moja
Na Salma Said,
WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi juzi usiku kwa sauti moja wamepitisha bila ya pingamizi marekebisho ya 10 ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Chini ya marekebisho hayo mapya Zanzibar itajulikana kwa jina la serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya umoja wa kitaifa kufuatia wananchi kutaka mfumo wa serikali ya umoja baada ya kura ya maoni iliyopigwa mwezi uliopita ambayo ilishinda kwa asilimia 66.4.
Mbali ya kifungu hicho kifungu cha 2 cha katiba kisemacho "kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za serikali rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania atashauriana na rais aweza kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa [...]Endelea hapa
"Mabadiliko ya Katiba Yapita kwa Sauti Moja"
Agosti 10, 2010 | Gawanyo
Kitaifa |
Acha maoni
Dola ya Zanzibar lazima iheshimiwe.
Na. B.OLE,
Zanzibar ni dola kama zilivyo dola nyengine duniani, kwa maana hiyo hapana budi kuheshimiwa na kuachiwa mamlaka yake ili iweze kuongoza Taifa lake kwa manufaa ya Wazanzibar wenyewe.
Tokea Mapinduzi kumekuwa na majaribio chungu mzima ya ama kuimeza au kuifuta kabisa katika ramani ya ulimwengu.Mpaka leo nashindwa kuelewa, kwa nini baadhi ya watu wakawa hawapati usingizi kwa ajili ya kuifikiria dola ya Zanzibar hali ya kuwa wao sio Wazanzibar wala haiwahusu ?
Wazanzibar hawana budi kuelewa na kutafakari kwa undani juu ya suala hili ambalo kwa mawazo yangu naona ni nyeti na ambalo halina budi kufanyiwa kazi ili upatikane ukweli wa jambo hili.
Njia nyingi zilitumiwa kuisambaratisha [...]Endelea hapa
"Dola ya Zanzibar lazima iheshimiwe."
Agosti 10, 2010 | Gawanyo
Makala/Tahariri |
Maoni moja
MABADILIKO YA KATIBA YA ZANZIBAR
Ningependa kutanabahisha juu ya Muswada wa mabadiliko ya Sheria ya zanzibar. Nimejaribu kuisoma lakini nimeona kama kuna haja ya kueleza kwa ufasaha zaidi juu ya mipaka ya Zanzibar Baharini. Imeelezwa tu na bahari yake. Hii itaweza kuleta utata mbele ya safari.
Jamani Tanganyika ndio iliyoleta chokochoko ya kushadidia hoja hoja ya kusema Zanzibar si nchi, wenyewe walipo amka wao wana hanhanha! Kipi kikubwa? Zanzibar ni nchi na ina katiba yake sasa kuibadilisha au kuirekebisha kuna makosa yeyote. Katiba ya Zanzibar si KAtiba ya Jamhuri ya Muungano ni yetu halisi wa hamna ushirika humu. Wa-Tanganyika mtaadhirika hapa.
Kama Jamhuri ya muungano imeundwa na nchi mbili huru basi hata [...]Endelea hapa
"MABADILIKO YA KATIBA YA ZANZIBAR"
Agosti 10, 2010 | Gawanyo
Habari |
3 maoni
Hisia za watanganyika – mabadiliko ya katiba ZNZ
My take: sasa wanakataa ya kwamba