Zanzibar ni nchi: Dr Bilali arudi kwao

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Nov 5, 2008
4,728
2,259
Wakuu naleta mada ya uchokozi wa mawazo.
Siasa za mwaka huu 2010 zinaenda kwa kasi ya ajabu.Matukio ya kura ya maoni Zanzibar yanaashiria kuvuruga muunganp na kuleta umoja huku Bara ikiwa njia ya kujihami.
Siyo siri kuwa mwelekeo wa Zanzibar ni hatimaye kujiondoa kabisa katika muungano na Tanganyika.
Kura ya maoni inathibitisha azma ya wa Zanzibari kujitenga.
Sasa je kwa sisi wabara kuna haja gani kuwa na makamu wa rais ambaye hatimaye atakuwa mtu wa nchi ya jirani?
Si vema Dr Bilali akarudi kwao?
 
Hii ishu ya zanzibar ku declare kuwa ni nchi kikatiba...is so tricky..nitaomba wanasheria humu watufafanulie.....kwani nihuavyo "muungano wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar ndio uliozaa Taifa jipya la Tanzania".......so technically mataifa yote mawili ya Tanganyika Na zanzibar[pemba na unguja]....yalisalimisha sovernity na kuunda moja ya Tanzania......ila ili kuepuka samaki mkubwa kummeza mdogo ...kwa mantiki ya mwalimu....Zanzibar waliachwa na mamlaka kwenye baadhi ya mambo yanayowahusu ....na yakaainishwa mambo yanayohusu Muungano yaani Tanzania...ni wazi walichopitisha baraza leo ni mawazo ya Aboud Jumbe ....ila safari hii yamekuja kivingine!!!

Uchambuzi wangu unanionesha kuwa masuala ya muungano yataendelea kuwa magumu kwani ni wazi Tanganyika watataka nao kurudisha mamlaka yao ambayo kwa sasa inaonekana wanayo kwa sababu ni nchi kubwa...lakini kimsingi kama wenzao wamerudisha nchi yao kikatiba basi .....kutakuwa na complication ya double loyalty.....na itabidi watumishi wa Zanzibar walio huku bara waeleze wazi msimamo wao na ikiwa watataka kubaki huku waendelee na kazi...lakini itakuwa vigumu kuendelea kuwaamini watu na kuwapa hadi umakamu wa rais wakati wao wameonesha kutokuwa imani na muungano.....nabashiri kuwa kwa hali ilivyo wanamkakati wa zanzibar wameshampiga bao kikwete na awamu ya pili ya uongozi wake tutarajie kuona bunge la zanzibar na serikali yake wakipitisha maamuzi mazito ikiwemo kuomba uwanachama wa UN...na kupeleka mabalozi nje kama nchi kamili....mfumo tuliokuwa nao wa muungano ndio uliokuwa unahalalisha kudumu kwa muungano nadhani ndio hata china wanatumua na hong kong...hongkong wanamamlaka kwenye baadhi ya mambo.....ukishatoa mamlaka kamili hakuna muungano tena...yaani Zanzibar itakuwa tu sawa na KENYA,UGANDA AU RWANDA.....ambao nao tupo kama nchi moja lakini hatuwezi kuwachagua wakawa mawaziri ...kwenye nchi yetu!!

MUUNGANO UNAPUMULIA OXYGEN!!
 
Kitovu cha muafaka baina ya Karume na Seif ni kurudisha Zanzibar! Na Zanzibar haitakuwa sehemu ya Muungano; bali itajiunga na Afrika Mashariki, kama nchi tofauti na huru kabisa!
 
WASEMAVYO WA-TANGANYIKA JUU YA ZANZIBAR

Kufuatia habari hii ambayo imo humu.
Zanzibar Kuwa Nchi
Na Hassan Shaaban, Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inafanya marekebisho ya katiba ya mwaka 1984, ambayo yanaipa Zanzibar hadhi kamili kama nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano.
MAONI YAO WA-TANGANYIKA

Suala la kuwa Z'bar ni nchi au kinyume chake liliwahi kuzungumziwa na mahkama ya Rufaa katika kesi ya Jamhuri dhidi ya Said Machano na Wengine 14, [1994] na iliamuliwa kuwa ZANZIBAR SI NCHI. Kesi hii ilikuwa inahusisha jamaa walioripotiwa kujaribu bila mafanikio kupindua serikali (felonious treason). Kuna mambo ambayo ni lazima yawepo ili treason itokee, ikiwa ni pamoja na serikali inayohusishwa kuwa na mamlaka ya kuendesha NCHI. Kwa kuwa Zanzibar [...]Endelea hapa "WASEMAVYO WA-TANGANYIKA JUU YA ZANZIBAR"

Agosti 10, 2010 | Gawanyo Habari | 2 maoni

Mabadiliko ya Katiba Yapita kwa Sauti Moja

Na Salma Said,
WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi juzi usiku kwa sauti moja wamepitisha bila ya pingamizi marekebisho ya 10 ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Chini ya marekebisho hayo mapya Zanzibar itajulikana kwa jina la serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya umoja wa kitaifa kufuatia wananchi kutaka mfumo wa serikali ya umoja baada ya kura ya maoni iliyopigwa mwezi uliopita ambayo ilishinda kwa asilimia 66.4.

Mbali ya kifungu hicho kifungu cha 2 cha katiba kisemacho "kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za serikali rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania atashauriana na rais aweza kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa [...]Endelea hapa "Mabadiliko ya Katiba Yapita kwa Sauti Moja"

Agosti 10, 2010 | Gawanyo Kitaifa | Acha maoni

Dola ya Zanzibar lazima iheshimiwe.

Na. B.OLE,
Zanzibar ni dola kama zilivyo dola nyengine duniani, kwa maana hiyo hapana budi kuheshimiwa na kuachiwa mamlaka yake ili iweze kuongoza Taifa lake kwa manufaa ya Wazanzibar wenyewe.
Tokea Mapinduzi kumekuwa na majaribio chungu mzima ya ama kuimeza au kuifuta kabisa katika ramani ya ulimwengu.Mpaka leo nashindwa kuelewa, kwa nini baadhi ya watu wakawa hawapati usingizi kwa ajili ya kuifikiria dola ya Zanzibar hali ya kuwa wao sio Wazanzibar wala haiwahusu ?
Wazanzibar hawana budi kuelewa na kutafakari kwa undani juu ya suala hili ambalo kwa mawazo yangu naona ni nyeti na ambalo halina budi kufanyiwa kazi ili upatikane ukweli wa jambo hili.

Njia nyingi zilitumiwa kuisambaratisha [...]Endelea hapa "Dola ya Zanzibar lazima iheshimiwe."

Agosti 10, 2010 | Gawanyo Makala/Tahariri | Maoni moja

MABADILIKO YA KATIBA YA ZANZIBAR

Ningependa kutanabahisha juu ya Muswada wa mabadiliko ya Sheria ya zanzibar. Nimejaribu kuisoma lakini nimeona kama kuna haja ya kueleza kwa ufasaha zaidi juu ya mipaka ya Zanzibar Baharini. Imeelezwa tu na bahari yake. Hii itaweza kuleta utata mbele ya safari.

Jamani Tanganyika ndio iliyoleta chokochoko ya kushadidia hoja hoja ya kusema Zanzibar si nchi, wenyewe walipo amka wao wana hanhanha! Kipi kikubwa? Zanzibar ni nchi na ina katiba yake sasa kuibadilisha au kuirekebisha kuna makosa yeyote. Katiba ya Zanzibar si KAtiba ya Jamhuri ya Muungano ni yetu halisi wa hamna ushirika humu. Wa-Tanganyika mtaadhirika hapa.
Kama Jamhuri ya muungano imeundwa na nchi mbili huru basi hata [...]Endelea hapa "MABADILIKO YA KATIBA YA ZANZIBAR"

Agosti 10, 2010 | Gawanyo Habari | 3 maoni

Hisia za watanganyika – mabadiliko ya katiba ZNZ

My take: sasa wanakataa ya kwamba
 
...Nafikiri JK muungano utamfia mkononi....what will happen is ...mwaka huu lazima Maalim Seif Atashinda uchaguzi....watu wa unguja this time will rally behind MAALIM....na Pemba always watampa Maalim....na motive ya kuiba kura mwaka huu itakuwa hakuna...CCM ZANZIBAR KWAHERI!!!!!!

naona zanzibar hata huyo mgombea SHEIN wana msideline..juzi kwenye ufunguzi wa baraza la wawakilishi hakuwapo....ukizingatia yeye ndie mgombea .....MAALIM alikuwapo.....ni wazi hata ccm zanzibar wamekubali kumuachia maalim urais...

huyu Bilal huku amekuja kuwachora tu!!!
 
Mimi nadhani bado tupo ktk matatizo ya matumizi ya maneno haya mawili - NCHI na TAIFA. wapo wanaosema Nchi ni sehemu ya Taifa kwa kutumia vigezo kama wimbo wa Taifa na bendera ya Taifa. Na pia wapo wanaosema Taifa ni sehemu ya Nchi wakitumia vigezo ktk matumizi ya lugha yetu..kama vile - Nchini Tanzania kuna bla bla bla..pia Nchi yetu na kadhalika.

Philemon Mikael,
CCM hawezi kushindwa uchaguzi ujao na mbinu zote hizi za kuunda Zanzibar kama nchi ni kuwapa kura CCM..Nasikitika kusema ndugu zangu wanapigwa changa la macho wazi na hawaoni mbali. Wee tazama viongozi wamekwisha jijengea nafasi zao za viti vya kiutawala mapema kabla ya hata ya nchi yenyewe kupitishwa.

Kilichofanyika ni kupeana vyeo vya KULA kisha wataendelea na mpango huo huku CCM wakiongoza kwani hao kina Seif walitokea wapi?.. Je mmesahau kwamba hata hao Hizbu waliingizwa CCM ilipoundwa kuondoa Upinzani wa kisiasa. It's all Politics mkuu wangu hakuna jipya.
 
Hii ishu ya zanzibar ku declare kuwa ni nchi kikatiba...is so tricky..nitaomba wanasheria humu watufafanulie.....kwani nihuavyo "muungano wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar ndio uliozaa Taifa jipya la Tanzania".......so technically mataifa yote mawili ya Tanganyika Na zanzibar[pemba na unguja]....yalisalimisha sovernity na kuunda moja ya Tanzania......ila ili kuepuka samaki mkubwa kummeza mdogo ...kwa mantiki ya mwalimu....Zanzibar waliachwa na mamlaka kwenye baadhi ya mambo yanayowahusu ....na yakaainishwa mambo yanayohusu Muungano yaani Tanzania...ni wazi walichopitisha baraza leo ni mawazo ya Aboud Jumbe ....ila safari hii yamekuja kivingine!!!

Uchambuzi wangu unanionesha kuwa masuala ya muungano yataendelea kuwa magumu kwani ni wazi Tanganyika watataka nao kurudisha mamlaka yao ambayo kwa sasa inaonekana wanayo kwa sababu ni nchi kubwa...lakini kimsingi kama wenzao wamerudisha nchi yao kikatiba basi .....kutakuwa na complication ya double loyalty.....na itabidi watumishi wa Zanzibar walio huku bara waeleze wazi msimamo wao na ikiwa watataka kubaki huku waendelee na kazi...lakini itakuwa vigumu kuendelea kuwaamini watu na kuwapa hadi umakamu wa rais wakati wao wameonesha kutokuwa imani na muungano.....nabashiri kuwa kwa hali ilivyo wanamkakati wa zanzibar wameshampiga bao kikwete na awamu ya pili ya uongozi wake tutarajie kuona bunge la zanzibar na serikali yake wakipitisha maamuzi mazito ikiwemo kuomba uwanachama wa UN...na kupeleka mabalozi nje kama nchi kamili....mfumo tuliokuwa nao wa muungano ndio uliokuwa unahalalisha kudumu kwa muungano nadhani ndio hata china wanatumua na hong kong...hongkong wanamamlaka kwenye baadhi ya mambo.....ukishatoa mamlaka kamili hakuna muungano tena...yaani Zanzibar itakuwa tu sawa na KENYA,UGANDA AU RWANDA.....ambao nao tupo kama nchi moja lakini hatuwezi kuwachagua wakawa mawaziri ...kwenye nchi yetu!!

MUUNGANO UNAPUMULIA OXYGEN!!

PM
nadhani maelezo yako yanahitaji marekebisho hapo nilipohighlight. Nadhani bado ni mapema kwani uchaguzi ni Oktoba na lolote laweza tokea.
 
State is synonymous with Country. United Republic of Tanzania has now paralysed!
 
Unahatarisha Muungano wewe!
Mkuu Masanilo,muungano umekuwa na sikio la kufa siku nyingi.
Mshtuko wako na wengine wengi tungeuelewa kama hatua za makusudi za kunzisha dola ya Zanzibar yenye mamlaka yake kamili zingedhibitiwa,ili muungano udumu.
Hata waswahili husema huwezi kuwa na mafahali wawili katka zizi moja.
Sioni mantiki ya kuendeleza kukumbatia Zanzibar ambayo mpyo wake haupp katika kuuendeleza muungano.
Watanzania bara lazima tudai uwakilishi ulio na umuhimu kwetu kwa kukataa uongozi wa kiwaridhisha waZanzibar ambao hawatutakii mema.
Sasa umuhimu wa kuwa na Mzanzibari,Dr Bilali,mtu wa nchi nyingine,kama makamu wa rais,uko wapi?
Wao wanapouvuruga muungano bila kuchukuliwa hatia yoyote sisi wengine hatuoni muelekeo.
Hivyo inabidi Dr Bilali arudi kwao
 
Wako WALIOAPA kuilinda na kuitetea KATIBA ya JMT? Kwa kweli wao ndio WASALITI na WAHAINI sio Wazanzibari kama alivyoandika Mwanakijiji.
 
so technically mataifa yote mawili ya Tanganyika Na zanzibar[pemba na unguja]....yalisalimisha sovernity na kuunda moja ya Tanzania.....

Boo hoooo!!!!!!

Zanzibar never surrendered its sovereignity. Ndiyo maana wana serikali, wana KMKM, wana bendera, wana wimbo wa taifa, hawana sarafu tu ili kuwadanganya watanganyika walinde mipaka yao kwa kupeleka JWTZ Zanzibar.
 
Waachieni waende zao. Kuondoka kwa Zanzibar, kutasaidia kwa watanzania bara kujitambua na kuwa focused na Tanganyika yetu, maana sasa hivi tunajiendea tu. Kutaletea kuwa na utaifa na uzalendo kwa Tanganyika yetu, afterall, bado tutakuwa nchi kubwa kushinda nchi zote 4 (Zanzibar ikiwemo) ya jumuia hii ya kulazimisha ya afrika mashariki ambalo lengo lake ni kuiba raslimali za Tanganyika. Viongozi wa sasa tulionao , akili yao ni ndogo na finyu kuweza kuongoza vema Jamhuri ya Muungano. Kwanza Zanzibar ni mzigo, pamoja na matatizo mengine wanakuwa alloctaed 4.5% ya budget ya Jamhuri, wakati wao hawafiki aslimia 2% ya idadi ya Watanzania!
 
Sasa je kwa sisi wabara kuna haja gani kuwa na makamu wa rais ambaye hatimaye atakuwa mtu wa nchi ya jirani?
Si vema Dr Bilali akarudi kwao?

Mkuu nikukumbushe tu kuwa Balali atakuwa Makamu wa raisi wa Jamhuri ya muungani. Tanzania bara bado haina uongozi...
 
Muungano ukivunjika, wabara tutarudia jina la Tanganyika? mmh! Hivi kubadili jina la nchi consequence zake zikoje? kiuchumi inatulea madhara?
 
Wakuu naleta mada ya uchokozi wa mawazo.
Siasa za mwaka huu 2010 zinaenda kwa kasi ya ajabu.Matukio ya kura ya maoni Zanzibar yanaashiria kuvuruga muunganp na kuleta umoja huku Bara ikiwa njia ya kujihami.
Siyo siri kuwa mwelekeo wa Zanzibar ni hatimaye kujiondoa kabisa katika muungano na Tanganyika.
Kura ya maoni inathibitisha azma ya wa Zanzibari kujitenga.
Sasa je kwa sisi wabara kuna haja gani kuwa na makamu wa rais ambaye hatimaye atakuwa mtu wa nchi ya jirani?
Si vema Dr Bilali akarudi kwao?

Hatujawahi kuona watu wa bara wanagombea uraisi au umakamu huko zanzibar, bali tunachoona kila mara ni wale wa zanzibar kupata hizo nafasi huku bara.
 
Acheni Zanzibar wajitenge ili kanuni ya historia aliyosema Mwalimu Kambarage itimie. Baada ya kujitenga watagundua kumbe siyo wamoja, kuna Wazanzibar na Wapemba. Dhambi ya ubaguzi itaendelea kuwatafuna hadi waone kumbe hata Zanzibar kuna wazanzibara na wanzanzibari. Wazanzibara wakiondolewa Zanzibar, Wazanzibar wataendelea kubaguana hadi mwisho. Wapemba nao itakuwa hivyohivyo, wataona kuna wapemba koko na wapemba weupe. Ubaguzi utaendelea hata wale weupe watajiona si wamoja, kuna wapemba wa Saudia, wapemba wa Oman na wapemba wa kireno. Watanganyika watendelea kuwa wamoja kwa kuwa hawatakuwa wametenda hiyo dhambi ya ubaguzi. Fanyeni haraka wazinzibar na wapemba kujitenga ili kanuni ya historia itimie.
 
... asieamini afwatilie for reference yaliyotokea Yugoslavia na wapi dhana ya ubaguzi imewafikisha. Serbs, Croats na Albanians na vijikabila chungu mzima vilikwenda mtindo huo na matokeo yake ni vijinchi vya kikabila na hata ki-udini!!
Nimecheka sana hii ya levels za Upemba na Uzanzibari. Hivi wale wa class ya WATUMWA labels zao vipi?
 
Mkuu nikukumbushe tu kuwa Balali atakuwa Makamu wa raisi wa Jamhuri ya muungani. Tanzania bara bado haina uongozi...

Sasa kama kwa kujitangaza nchi, Zanzibar haitakuwa inawajibika kwa serikali ya Muungano, hiyo JMT si itabaki ya bara tu? Kwa hali hiyo kwa nini tuwe na Makamu (ambaye atakuwa pigo moja tu la moyo kutoka urais) kutoka nchi nyingine? Itabidi vile vile iwekwe wzi kuwa mbunge nayetoka nchi moja asipewe nafasi ya uongozi katika serikali ya nchi nyingine! Itakuwaje raia wa Zanzibar apewe uwaziri katika JMT ambayo haina jurisdiction katika nchi yake?

Amandla......
 
Wako WALIOAPA kuilinda na kuitetea KATIBA ya JMT? Kwa kweli wao ndio WASALITI na WAHAINI sio Wazanzibari kama alivyoandika Mwanakijiji.

kwani hao Wazanzibari hakuna walioapa kulinda na kuitetea Katiba ya JMT? as a matter of fact wote kuanzia Karume na wenzake wameapa hivyo hivyo!!! ndiyo maana nimewaita ni wahaini.
 
Back
Top Bottom