Zanzibar na hatima ya Muungano ni hatari... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar na hatima ya Muungano ni hatari...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Jun 25, 2012.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Tokea ulipoondoka utawala wa kwanza ambao ndio utawala uliopokea uhuru wa Zanzibar ,hali za kitawala zilizofuatia zimekuwa za kibabe ,kuanzia Karume ,Jumbe,Ali hassan Mwinyi,Salmini Komandoo , Karume ,tuwache hawa wapemba wawili Shein na Seif ,siwatii hisabuni kwa sasa ,ila ubabe tumeuona juzi na jana kuhusiana na wale wajiitao uamsho.

  Tawala hizo ni tawala za kibabe na kulikuwa hakuna kufurukuta ,ukitofautisha na ile ya Mfalme ambayo ilikuwa na mambo yake lakini si ya kibabe, natumai inafahamika nisemapo mambo ya kibabe,nguvunguvu ujeshijeshi ,kamata weka kolokoloni funga no question or comment n.k.

  Sasa nimekuwa nikifikiria sana hawa wanaoshangilia kuvunjika Muungano ,mimi sipo pamoja nao ,langu ni kuwa Muungano uboreshwe na matatizo yatatuliwe kwa amani kabisa na kwa nia safi.Bila ya kuwepo na agenda za siri ,mkubwa kuonekana kumtawala au kummeza mdogo.

  Serikali ya Muungano imekuwa ikiangalia mambo ya Zanzibar bila ya kuyaingilia au kuyasemea ,pengine hayahusiki na Muungano ,kuna wakati wa Karume watu kibao ambao walikuwa pamoja walitoweka na hawakujulikana wamezikwa kaburi gani ,kuna wakati wa akina Salmini na Karume mwana,watu walikuwa wakipigwa hovyovyo kusema kweli ilikuwa wakipigwa kwa zamu,yaani leo unakwenda kupigwa mtaa fulani kesho mtaa mwengine ,Serikali haikusema kitu na ikijua ikisikia, inasemekana hata vijana wakitoka Tanganyika ,haya yakitokea zaidi nyakati za uchaguzi ,mtekelezaji mkuu ni mgombea wa wakati huo hivyo hata utawala wake unakuwa wa kuwatia hofu wananchi ,uhuru unakuwa haupo.

  Sasa tuchukulie leo hii Muungano unapasuka watu wanagawana mbao ,sioni sababu ambayo itamzuia mtawala wa Zanzibar kuwa mbabe ,tena safari hii kwa kiwango kikubwa ,kama kuliweza kufanyika ubabe wakati wa Muungano itashindwaje leo hakuna muungano ,atakae kamata mpini atajipanga kikweli na majilabu yatakuwa ya kutisha na atakaefurukuta na kutokeza pua atakiona kilichomfanya kuku kishingo kutokuwa na manyoya shingoni.

  Serikali ya muungano imewatupa wananchi wa Zanzibar kwa kudharau na kuacha watawala waliopita kuwanyanyasa wananchi bila ya kuingilia kati , tuseme leo hii wananchi wameamua bora jini likujualo kwa maana Muungano uliopo hauwasaidii kitu ni kama haupo ,zaidi unajali maslahi binafsi ,hivyo ni bora ukavunjika ,lakini kama ukivunjika bado suala utakuwa ni kwa faida ya nani ,au itakuwa ni kupinduana kila kukicha ?

  Kuvunjika kwa Muungano ni hatari kwa upande wa Zanzibar ,huku Tanganyika hakuna historia ya ubabe iliyowahi kumtia hofu mwananchi wa kawaida ukilinganisha na Zanzibar.Zanzibar kabla ya 1964 ilikuwa shwari ,hayo ya waarabu walikuwa hivi au vile yalikuwepo lakini hakuna historia inayoonyesha kuwa mwananchi alikuwa akiishi kwa hofu na woga kama baadaya 1964 hadi leo.

  Nakaribisha hoja na maoni.
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nadhani kwa manufaa ya wote, na kuwa na Muungano mzuri na wenye tija, huu Muungano uvunjwe na ziwepo njia mbadala za kuutafuta Muungano wenye maslahi kwa wote.

  Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni mfano mzuri wa vipi nchi ziungane. Taratibu na kupitia kwa kina kwa maridhiano kila sehemu wanayodhani inafaa iunganishwe.

  Walivyofanya Nyerere na Karume, kuungana wao wawili na kuwashinikiza wengine waungane wakitaka wasitake ni makosa makubwa.

  Ni wakati muafaka kuridhiana namna ya kuuvunja na kila mtu awe huru na maamuzi yake. La sivyo, hakutakuwa na amani ya kweli kwa pande zote mbili.
   
 3. m

  mamajack JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  kila mara huwa najiuliza, nini hasa kinachofanya huu muungano watu waung'ang'anie wakati wameshindwa kutoa haki sawa kwa pande zote mbili??waache wazanzibar wafanye mambo yao,maana wanawatumia ili waemdelee kuiba,wenyewe walishasema hawataki muungano na wanazo hoja za msingi katika hili.kunamambo mengi sana aliyaanzisha mwalimu jk ambayo kama tungeyaendeleza probably tusingefika hapa tulipo.lakini kwa kuwa mengi yalikuwa yanabana ulaji wa mafisadi,yote yamezikwa,wamebakiza hili la muungano.nadhani kunamaslah binafsi katika hili.watu wameshauri kama kuuvunja ni dhambi basi muundo wake ubadilishwe,na hilo wanaona shida.
   
 4. W

  WaMzizima Senior Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni bora ukasome historia kidogo ubabe Zanzibar ulianzia tangu uchaguzi wa 1961 ambapo ZNP ilishinda kwa mbinde na ASP kudai faulo na hiyo ikajirudia tena 1963 pale ZNP/ZPPP waliposhinda tena na ASP kudai kuibiwa kura, ZNP ikawafukuza kazi na kuwanyanyasa wafuasi wa ASP serikalini na vilevile watu kuuwawa. Soma historia hayo yalikuwepo tangia enzi hizo kabla ya mapinduzi. Infact ni moja ya sababu kuu ya mapinduzi ni huo ubabe na unyanyaswaji uliokuwa ukifanywa na chama cha ZNP ambacho kilikuwa kimeelemea zaidi kwa waarabu na ASP kikiwa na wafuasi wengi weusi na washirazi.

  Ni wazi hivi sasa suala kuu ni muungano pindi ukivunjika basi yataanza mengine yetu macho. Si kweli eti Zanzibar palikuwa shwari kabla ya mapinduzi huo ni uzushi na wishful thinking, tuweke facts wazi.
   
 5. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Jadilianeni huko zenj mkimaliza nlete hoja zenu mezani. Kama muungano umewachosha mpige kura ya kuukataa. Malalamiko yenu yametuchosha wakati hakuna chochote cha maana tukipatacho kwenu kuwa sehemu ya muungano zaidi ya kuwalipia bili kibao
   
 6. C

  Cyriacus Member

  #6
  Mar 20, 2014
  Joined: Feb 4, 2014
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Imekuwa ikishangaza sana kwa Watanzania wengi wasio Wazanzibari kuhusu huu Muungano wetu!.


  Chuki, Vipigo, Kejeri, Mauaji na hata Kujeruhi watu wetu huko Zanzibar kwa kutumia vyombo vya Moto & Tindikali eti kwa sababu Muungano huu hauna tija kwa Wazanzibari!!.


  Sasa,
  Kwakuwa muda wa Wazanzibari kuomba TARAKA yao ni kama ulishapita hivi,
  Basi ni muda wetu Watanganyika nasi kudai taraka yetu!.


  Ingekuwa BORA sana Muungano huu ukifa kupitia haya Mabadiliko ya Katiba!.
   
 7. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2014
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hii ndio mbinu ambayo Warioba na hila zake wamekaa chini wakaona ndio inayoweza kuvunja Muungano?

  Muda wote wanatetea serikali 3, kumbe nyuma ya pazia ni haya unayojaribu kuyafikiria?

  Sasa hapo ndipo mtakapo ijua CCM ni nani hasa linapokuja suala zito la namna hii.

  Two government system reformed ndio habari ya Mujini.
   
 8. VOICE OF MTWARA

  VOICE OF MTWARA JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2014
  Joined: Dec 20, 2012
  Messages: 2,463
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145

  mawazo ya kilevi ya akina wasira haya
   
 9. Jacobus

  Jacobus JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2014
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 3,580
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Ndivo wanavotaka kwa kung'ang'ania serikali mbili. Inatulazimu tudai kura ya maamuzi kuhusu uwepo wa muungano ikiwa watafanikiwa kupindua maoni ya wananchi wengi kupitia rasimu ya katiba. Hii itakuwa haki yetu ya kudai kura hiyo na si katiba mpya tena.
   
 10. m

  mzee wa kijiwe JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2014
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 916
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 180
  Wakati watanzania wakijadili mfumo upi wa serikali utakaodumisha muungano. wapo baadhi ya watu wanaoukataa mfumo wa serikali tatu kwa maelezo kwamba mfumo huo utavunja muungano. Hii ni hoja dhaifu sana. hakuna muungano wowote duniani utakaodumu milele hata ndoa ina mwisho wake.

  Wakati mwingine kifo kinavunja muungano au talaka. waasisi wote wa muungano wenye hekima lazima narudia ni lazima siku ya kwanza kabisa kabla hata ya kuungana waonyeshe jinsi ya kutengana kwa amani.

  Hii ndiyo hekima ya juu kabisa kumbuka Mungu mwenyewe alisema hafi kifo kitakapo watenganisha. kumbuka kifo kinamkuta mshirika mmoja wa muungano na mwingine anaendelea na maisha labda hata kujiunga na taasisi mpya ya ndoa. Hili ndilo kosa letu watanzania.

  Tunalazimisha muungano hata pale mshirika mwenza hataki tena. Tunapojadili jambo hili ni vema tukaangalia kwa makini njia nzuri za amani kabisa za kuuvunja muungano huo.

  Serikali tatu zinatoa fursa nziri zaidi za kutengana bila kupigana na kuumizana. Tusijidanganye serikali mbili ni njia ya kinafiki ya kuishi ndani ya muungano.

  Hata pale makubaliano ya msingi yanapovunjwa. huu sio muungano. tuamue sasa aina ya muungano tunao uhitaji na tujadili kwa uwazi kabisa junsi ya kuachana kwa amani.

  CC KWA UKAWA HASWA MTIKILA

  Nawasilisha.
   
 11. J

  Jamie Nsuri Senior Member

  #11
  Apr 9, 2014
  Joined: Jan 16, 2014
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna Muungano Usiovunjika. Sijaelewa mantiki ya kuchagua kichwa cha habari km hiki (we don't state the obvious) km unazungumzia serikali 3 ni suluhisho la matatizo huku unasema Tuzungumze namna ya kuachana kwa amani huku unasema serikali 3 ni njia nzuri ya kuendeleza muungano mm nimeshindwa kukuelewa ndugu. Tuuvunje ndicho usemacho ila hutaki kuwa muwazi au? Funguka.
   
 12. manyimbo

  manyimbo JF-Expert Member

  #12
  Apr 9, 2014
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 509
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  inaelekea wewe mzito kweli kuelewa.
   
 13. t

  tpmazembe JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2014
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 2,474
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  yaani kuna watu hawajaelewa hata mada nyepesi kama hii? mtoa mada anamaanisha muungano sio lazima udumu milele,maana kinachoangaliwa katka muungano ni maslahi ya kila upande. kama upande hautarishika na muungano huo ya nini kugombana,kuuwana ,kumwagiana tindikali,kufanya maandamano tunaachana kwa amani. kumbuka muungano ni kitu tofauti sana hasa huu wa kwetu ambao uko documented. Hata nyerere akasema waznz wenyewe hakiamua kutoka ndani ya muungano bila kushawishiwa na nchi zingine hata wapiga mabomu bali atawapa nchi yao. kwa nini kuungana ndio uwe uhasama. mbona wenzetu kenya na uganda wanatupenda sana hata ukikutana na mkenya au mganda mnaongea kama ndugu ila mtanganyika huko znz anaonekana na waznz kama mnyonyaji au tapeli au mwizi kwa nini. kama hawataki basi. wajenge uchumi wao tukutane AU au eac au sadic au UN. basi
   
 14. t

  tenende JF-Expert Member

  #14
  Apr 17, 2014
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  NAUONA UBABE WA CCM kulazimisha sera za chama chao kutawala katiba kugeuka kuwa chanzo cha kuvunja muungano...
  Chama kinaeneza chuki na uhasama wa kidini na kikabila kupitia bunge la katiba, nyumba za ibada na vyombo vya habari..
  ... chama kinatishia watu kuwa vita na mapinduzi ya serikali yatatokea iwapo watu watapingana na matakwa ya CCM,... Swali la kujiuliza;.. je, ni nani atapindua kama si wao wenyewe?
  ... CHAMA hiki kinapumbaza watu kama mtetemela kwa pesa n.k.
  SERA YA CCM NI SERIKALI MBILI. kwa sera hii si kubana matumizi wala kulinda amani ya nchi.. Ni msimamo wa kuidhibiti ZANZIBAR isiwe huru kufanya mambo yake ni msimamo wa kuamua mshindi wa uchaguzi nje ya sanduku la kura.. Kwa mfano, ...chaguzi za 1995, 2000, 2005, na 2010 za ZANZIBAR katika nafasi ya urais wakati wote matokeo hutangazwa na kuzua utata wa nguvu za BARA!..
  CHINI YA SERA HII HAKUNA UCHAGUZI HURU ni UBABE!
  Rasimu ya katiba wameikataa na sasa wanahangaika kupitisha sera za CCM ziwe ni mwongozo na DIRA ya taifa!... Sera ambazo katibu mkuu KOLIMBA aliziona na kusema, .."CCM haina DIRA WALA MWELEKEO"... sasa naona wazi chama kinavyoua muungano na kujifia.
  SERA ZILIZOSHINWA KUIKOMBOA NCHI ZINAPINGANIWA ZIENDELEE KUKANDAMIZA NCHI!
   
 15. chipanga

  chipanga JF-Expert Member

  #15
  Apr 17, 2014
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 661
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 60
  Muungano ukivunjika Tanganyika ndo itapoteza zaidi, huondo ukweli.
   
 16. t

  tenende JF-Expert Member

  #16
  Apr 17, 2014
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Zanzibar itakosa vitunguu!
   
 17. Olaigwanani lang

  Olaigwanani lang JF-Expert Member

  #17
  Nov 15, 2015
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 480
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Jamani Watanzania wote, hali halisi ya kisiasa kule visiwani mnaishuudia, ninachojiuliza hivi wabunge wale wa Muungano watakwenda kuapishwa Dodoma au? na pia Wizara za Muungano atataeuliwa nani toka Zanzibar kwani inasemekana uchaguzi na matokeo yake yamefutwa.

  Je, hali hii inauweka Muungano katika hali gani?

  SI NDIO MWISO WAKE NA WANAOUVUNJA NI VIONGOZI WA CCM YENYEWE.
  EBU TUSHEE MAWAZO YENU YOTE KUHUSU HILI.
   
 18. L

  Lab JF-Expert Member

  #18
  Nov 15, 2015
  Joined: Aug 16, 2015
  Messages: 401
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 60
  hio wizara itaachwa, kwani lini viongozi wa kiafrica wakafuata katiba? katiba na sheria ni kwa ajili ya kuibia wananchi wao na si kuongoza wananchi
   
 19. D

  Dr Almas Member

  #19
  Nov 15, 2015
  Joined: Aug 13, 2015
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ni vema ukasoma sheria na katiba za Nchi kuliko kusoma magazeti yaliyojaa propaganda za wanasiasa
   
 20. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #20
  Nov 15, 2015
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Tanzania bora liende
   
Loading...